Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Hata ukitukana wasukuma haitakusaidia kitu
Akili za kishamba hizo,yule jamaa wenu wa Chato alijifanya kuwa yeye ndiye Mtanzania pekee na kundi lake la akina Sabaya,Musiba,Mahera,Ndugai na Makonda,cha ajabu amekufa Tanzania ikabaki huru kama ilivyokuwa mwanzo kabla yake,mambo ya utekaji na risasi za hadharani hatuzisikii tena.
 
“......Huu ni mwaka wa tano kuishi nje sio jambo dogo, kufanya maandalizi kunahitaji muda na fedha pia, Rais aliahidi kunilipa fedha za matibabu lakini hazijalipwa hadi leo licha ya kusema niandike madai yangu,” amesema Lissu
Huyu jamaa si aliutangazia umma wa dunia kwamba tayari serikali ya Tanzania imemplipe madai yake yote, mbona anakanusha tena?

Alifikiri urafiki waliokuwa wanaufanya na ahadi hewa zingetokea kirahisi tu kwa utashi wao?

Kuna siku wanaomdhihaki JPM ambaye hayupo kujitetea kutokana na yote anayozushiwa watatamani dunia ipasuke iwameze maana haki ndipo itakapo dhihirika kwa vitendo dhidi yao
Hakuna kitu kama hicho badala ya kuwakumbuka Nyerere na Mkapa umkumbuke mwendazake,hii ni ajabu kabisa.
 
Sasa km Mwana sheria anafanyiwa uhuni km huu!! tena mchana kweupeeee!! sheria zake hazikumsaidia kwa nchi inayo fuata sheria!! uanasheria hauna Maana!! mtoto wa shule usisomee sheria katu!
 
Wee ndio tutakufukuzia kwenu burundi siku si nyingi! Warundi mliohamia hapa ndio mliokuja na ubaguzi
Mbowe kwao Kericho Kenya unasemaje hilo? Ndiko ndugu zake wengi na wajomba zake wako kule na ana nyumba Kericho Kenya
 
Mambo ya MIGA yanakusaidia kumjua alivyomnafiki na muongo muongo huyo Lisu wako
Kwamba hajapigwa risasi kama mvua!?
Uchunguzi wa bunduki iliotumika nao mpka lisu ahojiwe?
Tuonyesheni basi yaliopo kwenye zile cctv.
Ni aibu mpaka sasa polisi hawana lolote la kusema kuhusu lile tukio!

Kwamba huu ndo weledi wa jeshi tunalotegemea kulinda usalama wetu?
 
Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka mitano imepita tangu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu kushambuliwa, Jeshi la polisi limesema bado linaendelea kumsubiria mwanasiasa huyo na dereva wake.

Lissu ambaye anaishi nchini Ubelgiji alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Mkutano wa Bunge.

Baada ya shambulio hilo, Lissu alipelekwa Hospitali ya rufaa ya Dodoma kabla ya kuhamishiwa Nairobi nchini Kenya siku hiyo hiyo alikoanza kufanyiwa operesheni na baadaye kuhamishiwa nchini Ubeligiji anakoishi mpaka sasa.

Katika mtandao wake wa Tweeter leo Jumatano Septemba 7, 2022 Lissu ameadika risasi 16, miaka mitano na operesheni 25 baadaye, bado nimewakomalia na mapambano yanaendelea miaka mitano, nabaki kujiuliza maswali.

“Ni kwanini Serikali na Jeshi la Polisi hadi leo hawafanyi uchunguzi na kwanini nimenyimwa, nimenyimwa haki zangu za msingi ikiwemo matibabu,”

Mwingine aliyetoa ujumbe unaofanana na Lissu ni Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ambaye aliandika, “IGP na DCI ni vyema mkatumia siku ya leo, kutoa maelezo kwa umma ni kwanini hadi sasa waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu hawajakamatwa na lini mtaridhia wachunguzi”

Mwananchi Digital ilipomtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema uchunguzi wa kesi yeyote ya jinai unaweza kuendelea hadi pale waliofanya tukio hilo watakapopatikana.

“Watakapopatikana ndipo itajulikana nia ilikuwa ni nini kama Jeshi la Polisi lilivyowahi kusema uchunguzi wa tukio la Tundu Lisu bado tunaendelea nao kwa kukusanya ushahidi kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Tulishasema pia aje pamoja na dereva wake ili tupate maelezo yao kwani yatatusaidia kusonga mbele katika uchunguzi wetu,”amesema Misime.

Akizungumza na Mwananchi, Lissu amesema hata kama nchi haiko salama sio sababu ya yeye kutokurudi, kwani kurudi nchini kunahitaji maandalizi ikiwemo fedha.

“Huu ni mwaka wa tano kuishi nje sio jambo dogo, kufanya maandalizi kunahitaji muda na fedha pia, Rais aliahidi kunilipa fedha za matibabu lakini hazijalipwa hadi leo licha ya kusema niandike madai yangu,”amesema Lissu.

Chanzo: Mwananchi
Bashite anatafutiwa kesi
 
Lisu na mkubali sanaaa
Ila kile kitendo cha kuuza ramani ya ndege yetu kanada... Kwakweli siku penda basi tuu

..Magufuli alipokuwa waziri wa ujenzi alivunja mkataba kibabe.

..mkandarasi akashtaki na kushinda, lakini Magufuli na serikali wakapuuzia kumlipa.

..Baadae serikali ikaenda kununua ndege kwa fedha cash. Hapo ndipo mdai akaenda kukamata ndege yetu.

..Aliyetoa ramani za ndege ni Magufuli aliyekuwa akitamba kwamba amenunua kwa fedha taslimu huku akijua kuna watu huko nje wanatudai.

..Ndege iliyokamatwa South Africa, Mzungu alishinda kesi ktk mahakama za hapa nyumbani. Waliomtetea walikuwa mawakili Watanzania. Na waliohukumu ni majaji Watanzania.

..Waliotuponza ni wale waliopuuzia hukumu za mahakama na kusababisha wadai wetu waanze kuwinda mali zetu huko nje.
 
..hiki ulichoandika ni UONGO.

..kama dereva ametoroka basi Polisi wa Tz waripoti kwa INTERPOL ili dereva huyo akamatwe na kurejeshwa Tz.

..Kwasababu Polisi wa Tz hawajachukua hatua hizo maana yake ni kwamba hawamhitaji dereva wa Lissu.
Kumbe dereva yuko Tanzania? Basi polisi hawajui hilo. Ila haijasemwa dereva katoroshwa bali dereva amefichwa huko Ubeljiji na waliomficha ni wale wale walioshambuliwa. Mwanzoni alipokuwa Nairobi walisema kuwa anatibiwa kisaikolojia, Waulize na huko Ubeljiji anafanya nini na kwa nini wawe tayari kumgharamia kiasi hicho? Wewe kama unaona ni kawaida wenzako tunaona kuna kitu. Nakukumbusha kuwa kwenye 2012-2013 hao jamaa walijilipua kwa bomu kule Arusha kwa lengo la kutafuta kiki. Mwanasiasa mmoja Kristofa Mtikila alipouambia umma wa Tanzania kuwa lile bomu walilitega wenyewe alitangazwa adui wao mkubwa kuliko CCM. Mpaka mauti yalipomkuta. Tulishuhudia njia nyingi sana za kutafuta kiki wakati ule ikiwa ni pamoja na kujishambulia, kujiteka, n.k.
 
..kuna kutokuaminiana baina ya polisi na wahanga wa hili tukio.

..upo ushahidi wa dola kutumia nguvu bila sababu dhidi ya Cdm na kuwafungulia kesi za uongo.

..kilichofanya dereva akimbie hapa Tz ni hofu ya kubambikiwa kesi au kusingiziwa kwamba amehusika na tukio lile.

..vilevile yako mazingira yanayoonyesha kwamba dola imehusika na tukio lile. Na hivyo inawezekana kabisa ikajaribu kum-victimize dereva.

..mazingira ya dola kuhusika yanatokana na tuhuma kwamba ulinzi wa serikali uliondolewa eneo la tukio siku ambayo Lissu alishambuliwa.

..jambo lingine ni tuhuma kwamba Cctv zilizokuwa installed eneo la tukio, na inawezekana zilikuwa zinafanya kazi, ziliondolewa na watu wa serikali, na umma haujaelezwa kilichoonekana ktk footage.

..Sasa ikiwa polisi wanahitaji kuongea au kumkamata dereva ziko taratibu za kufanikisha zoezi hilo.

..Polisi walipaswa kushirikiana na wenzao wa Nairobi ktk kipindi cha miezi 4 ambayo Lissu na dereva walikuwa Nairobi.

..Pia walipaswa kumfikia dereva au Lissu kupitia Interpol au polisi wa Ubelgiji. Huo ndio utaratibu wa kupata ushahidi, au kukamata watuhumiwa walioko nje.

NB:

..Hata kama tukio hili limepangwa na mtu wa Cdm, bado haieleweki WALINZI wa serikali walikwenda wapi?

..Je, tukio lilifanywa na mtu wa Cdm au mwingine yeyote kwa kushirikiana na mamlaka zinazopanga ulinzi ktk nyumba za viongozi wa serikali area D Dodoma.

..Kuhusu Mtikila kutuhumu Cdm kulipua kwa bomu mkutano wao, suala hilo lilipaswa kuchunguzwa ili kuwabaini waliohusika.

..Mpaka muda huu tulipaswa kujua lilikuwa bomu la aina gani. Ni watu au vyombo gani wana-access au wanatumia mabomu hayo. Cdm walipataje bomu hilo, etc etc.
 
Kumbe dereva yuko Tanzania? Basi polisi hawajui hilo. Ila haijasemwa dereva katoroshwa bali dereva amefichwa huko Ubeljiji na waliomficha ni wale wale walioshambuliwa. Mwanzoni alipokuwa Nairobi walisema kuwa anatibiwa kisaikolojia, Waulize na huko Ubeljiji anafanya nini na kwa nini wawe tayari kumgharamia kiasi hicho? Wewe kama unaona ni kawaida wenzako tunaona kuna kitu. Nakukumbusha kuwa kwenye 2012-2013 hao jamaa walijilipua kwa bomu kule Arusha kwa lengo la kutafuta kiki. Mwanasiasa mmoja Kristofa Mtikila alipouambia umma wa Tanzania kuwa lile bomu walilitega wenyewe alitangazwa adui wao mkubwa kuliko CCM. Mpaka mauti yalipomkuta. Tulishuhudia njia nyingi sana za kutafuta kiki wakati ule ikiwa ni pamoja na kujishambulia, kujiteka, n.k.
Hata ujifariji lakini ukweli uko pale pale.
 
Hivi hakuna mahakama anaweza kushtaki duniani jaman ni mpaka Tanzania?

Kwani mahakama za kimataifa haziwezi kumsaidia Lissu kuchukua maelezo yake na dereva wake na kutuma wataalamu wa upelelezi kuchukua maelezo kwa muroto na Sirro.
 
Back
Top Bottom