Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kuna kitu hapo hakipo sawa.Kupigwa upigwe wewe alafu kuhojiwa unataka wakahojiwe wengine ??
Yani aliyekuwa anakuendesha unamficha mazima kabisaaa alafu nyumbu wanaona hili ni sawa?
.
Mazingira ya kisiasa wakati huo yalikuwa yameweka upuuziaji wa issues za matishio waliyokuwa wanakumbana nayo wapinzani.
Lisu aliwahi kutoa taarifa kwa umma kuhusu kufuatiliwa na watu asiowajua na hali hiyo kwa mwenye weledi (polisi) alipaswa kukaa na mlalamikaji wakaweka.mtego kumnasa anayemfuatilia.
Pia ukosoaji wa Lisu ulipelekea prkpaganda nyingi hasi dhidi yake. Kama Jeshi la Polisi wangekuwa wanaheshimu na kulinda katiba na sheria wangetumia weledi wao kung'amua kwwmba inawezekana maadui wa Taifa wakamdhuru Lisu kisha nchi ikaingia doa. Wangemuwekea ulinzi hata usioonekana lakini mhusika angejulishwa.
Kitendo cha yeye kushambuliwa kisha CCTV zikaondolewa eneo la tukio, maana inayojengeka hapo ni kwamba tukio lilipangwa likafeli.
Ningekuwa Kingai ningeanza na wahusika wa CCTV kujua kulikoni waliziondoa.
Je endapo angekuwa amekufa kwenye tukio hilo, bado polisi wangeng'ang'ania kutaka marehemu afufuliwe wapate maelezo ya tukio zima?
Nina mashaka sana na usalama wetu wa ndani ya nchi. Hususani mtu anapokuwa na mawazo mbadala yanayoweza kuwafungua macho na mtazamo wananchi ili waweze kuendelea vyema anaweza kuundiwa zengwe hata la ujqmbazi akauawa na shuvhuli ikaishia hapo.
Tusiendelee kushabikia unyumbu na magamba bali tuishabikie nchi iyohitaji kila.mtu kutumia nafasi yake kikamilifu kuiletea maendeleo yake.
CCM inajifichama ndani ya dola ndo maana baadhi ya wateule wa kisiasa kupitia CCM wametokea kwenye majeshi yetu ambapo wenye akili wanelewa hiyo ni rushwa ya kisiasa.....