Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Kupigwa upigwe wewe alafu kuhojiwa unataka wakahojiwe wengine ??

Yani aliyekuwa anakuendesha unamficha mazima kabisaaa alafu nyumbu wanaona hili ni sawa?

.
Kuna kitu hapo hakipo sawa.

Mazingira ya kisiasa wakati huo yalikuwa yameweka upuuziaji wa issues za matishio waliyokuwa wanakumbana nayo wapinzani.

Lisu aliwahi kutoa taarifa kwa umma kuhusu kufuatiliwa na watu asiowajua na hali hiyo kwa mwenye weledi (polisi) alipaswa kukaa na mlalamikaji wakaweka.mtego kumnasa anayemfuatilia.

Pia ukosoaji wa Lisu ulipelekea prkpaganda nyingi hasi dhidi yake. Kama Jeshi la Polisi wangekuwa wanaheshimu na kulinda katiba na sheria wangetumia weledi wao kung'amua kwwmba inawezekana maadui wa Taifa wakamdhuru Lisu kisha nchi ikaingia doa. Wangemuwekea ulinzi hata usioonekana lakini mhusika angejulishwa.

Kitendo cha yeye kushambuliwa kisha CCTV zikaondolewa eneo la tukio, maana inayojengeka hapo ni kwamba tukio lilipangwa likafeli.

Ningekuwa Kingai ningeanza na wahusika wa CCTV kujua kulikoni waliziondoa.

Je endapo angekuwa amekufa kwenye tukio hilo, bado polisi wangeng'ang'ania kutaka marehemu afufuliwe wapate maelezo ya tukio zima?

Nina mashaka sana na usalama wetu wa ndani ya nchi. Hususani mtu anapokuwa na mawazo mbadala yanayoweza kuwafungua macho na mtazamo wananchi ili waweze kuendelea vyema anaweza kuundiwa zengwe hata la ujqmbazi akauawa na shuvhuli ikaishia hapo.

Tusiendelee kushabikia unyumbu na magamba bali tuishabikie nchi iyohitaji kila.mtu kutumia nafasi yake kikamilifu kuiletea maendeleo yake.

CCM inajifichama ndani ya dola ndo maana baadhi ya wateule wa kisiasa kupitia CCM wametokea kwenye majeshi yetu ambapo wenye akili wanelewa hiyo ni rushwa ya kisiasa.....
 
Nimesoma hii kitu kwa aibu kubwa sana! Kama ni kweli msemaji wa Jeshi kasema hayo maneno basi ni hatari kubwa sana, kuna tatizo kubwa mno mno ktk chombo hiki na kinahitaji kuvunjwa na kuunda Jeshi jipya la polisi!
 
Unaamini taarifa za Lisu ? Kwani ametoa taarifa mara ngapi kwamba Tanzania itashitakiwa MIGA , je ilishitakiwa? Lisu ametoa taarifa mara ngapi kwamba anarudi Tanzania, he amerudi?

Unaanza na CCTV wakati dereva wa Lisu yupo amefichwa?
Ukifuatilia posts zangu humu jukwaani utaelewa mimi ninapingana na Lisu kwenye mengi sana. Nina kadi hai ya CCM na ninaijua siasa kwa sababu nimeishiriki tangu nikiwa mdogo.

Linapokuja suala la UTU huwa naiweka siasa pembeni na kupambania utu kwanza.

Haya mambo ya MIGA na mawazo tofauti na ideleogies za CCM yasitumike kujustify madhila dhidi ya utu wa Watanzania wenzetu. Jirani anayenitukana sitoacha kumsaidia anapopatwa na dharura inayogusa utu wake. Njia ya kumfundisha mtu ambaye kutwa kuchwa anakuharibia ni kusimama naye wakati wa taabu zake ataelewa na kukuelewa.

Hivyo mkuu mambo ya MIGA yanahusikaje kwenye kumhukumu #TunduLisu?
 
Kupigwa upigwe wewe alafu kuhojiwa unataka wakahojiwe wengine ??

Yani aliyekuwa anakuendesha unamficha mazima kabisaaa alafu nyumbu wanaona hili ni sawa?

.
Nadhani walifanya jambo la maana sana kumficha, lasivyo waliowakosakosa wangemmaliza ili kuficha ushahidi. Pia huenda walimshuku/walimjua aliyetenda hilo na wakaona kabisa ni ngumu kuchukuliwa hatua kutokana na cheo chake, kwaiyo ikabidi kujificha kuliko kugombania kisu na aliyeshika mpini.​
 
Kupigwa upigwe wewe alafu kuhojiwa unataka wakahojiwe wengine ??

Yani aliyekuwa anakuendesha unamficha mazima kabisaaa alafu nyumbu wanaona hili ni sawa?

.
Wewe ni mmojawapo wa wasiojulikana,acha kumtishia Lissu zama zimeshabadilika.
 
Unaamini taarifa za Lisu ? Kwani ametoa taarifa mara ngapi kwamba Tanzania itashitakiwa MIGA , je ilishitakiwa? Lisu ametoa taarifa mara ngapi kwamba anarudi Tanzania, he amerudi?

Unaanza na CCTV wakati dereva wa Lisu yupo amefichwa?

..nyinyi mmelishwa propaganda.

..kwa taarifa yako serikali ilishtakiwa miga.

..jiulize kwanini serikali iliachana na madai ya usd 191 billion dhidi ya acacia.

..jiulize kwanini ripoti za mruma na osoro zimefichwa hakuna anayezirejea.
 
Unaamini taarifa za Lisu ? Kwani ametoa taarifa mara ngapi kwamba Tanzania itashitakiwa MIGA , je ilishitakiwa? Lisu ametoa taarifa mara ngapi kwamba anarudi Tanzania, he amerudi?

Unaanza na CCTV wakati dereva wa Lisu yupo amefichwa?
Sukuma gang unataka kabila la Wasukuma liendelee kutukanwa mpaka lini wakati kule kuna watu wengi wenye akili timamu ila ninyi mliozaliwa gamboshi muda wote mnafikiria mauaji tu na damu za watu pumbavu kabisa.
 
Jeshi la polisi limesema bado linaendelea kumsubiria mwanasiasa huyo na dereva wake ili wawakamate na kuwahoji namna tukio lilivyotokea.

Lissu ambaye anaishi nchini Ubelgiji alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Mkutano wa Bunge.

Baada ya shambulio hilo, Lissu alipelekwa Hospitali ya rufaa ya Dodoma kabla ya kuhamishiwa Nairobi nchini Kenya siku hiyo hiyo alikoanza kufanyiwa operesheni na baadaye kuhamishiwa nchini Ubeligiji anakoishi mpaka sasa.

Katika mtandao wake wa Tweeter leo Jumatano Septemba 7, 2022 Lissu ameadika risasi 16, miaka mitano na operesheni 25 baadaye, bado nimewakomalia na mapambano yanaendelea miaka mitano, nabaki kujiuliza maswali.

“Ni kwanini Serikali na Jeshi la Polisi hadi leo hawafanyi uchunguzi na kwanini nimenyimwa, nimenyimwa haki zangu za msingi ikiwemo matibabu.”

Mwingine aliyetoa ujumbe unaofanana na Lissu ni Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ambaye aliandika, “IGP na DCI ni vyema mkatumia siku ya leo, kutoa maelezo kwa umma ni kwanini hadi sasa waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu hawajakamatwa na lini mtaridhia wachunguzi.”

Mwananchi Digital ilipomtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema uchunguzi wa kesi yeyote ya jinai unaweza kuendelea hadi pale waliofanya tukio hilo watakapopatikana.

“Watakapopatikana ndipo itajulikana nia ilikuwa ni nini kama Jeshi la Polisi lilivyowahi kusema uchunguzi wa tukio la Tundu Lisu bado tunaendelea nao kwa kukusanya ushahidi kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Tulishasema pia aje pamoja na dereva wake ili tupate maelezo yao kwani yatatusaidia kusonga mbele katika uchunguzi wetu,”amesema Misime.

Akizungumza na Mwananchi, Lissu amesema hata kama nchi haiko salama sio sababu ya yeye kutokurudi, kwani kurudi nchini kunahitaji maandalizi ikiwemo fedha.

“Huu ni mwaka wa tano kuishi nje sio jambo dogo, kufanya maandalizi kunahitaji muda na fedha pia, Rais aliahidi kunilipa fedha za matibabu lakini hazijalipwa hadi leo licha ya kusema niandike madai yangu,”amesema Lissu.
Mbona Kama vichekesho, yaani wawakamate wahanga wa tukio la uhalifu na kuwahoji?;

Kwamba police wanahisi huyo Lissu na dereva wake lile tukio wamejitengenezea sio la kweli au
 
Mungu wao aliyetoa maelekezo ya kuuwawa lisu kafa mwenyewe, walioratibu zoezi Bashite kipilimba na wenzake wapo ni kuanza nao hata kwa njia za jadi
 
Tushitakiwe MIGA alafu Lisu akae kimya?

..kwa hiyo Lissu ndio chanzo chako pekee cha habari?

..mbona hapa JF na ktk vyanzo mbalimbali taarifa za kesi ya acacia dhidi ya Tz zilikuwepo?

..unafahamu kwanini serikali iliachana na madai ya usd 191 billion dhidi ya acacia?

..umewahi kujiuliza kama tungelipwa kitita cha usd 191 billion leo tungehitaji tozo au royal tour?

Cc Nguruvi3, Proved
 
Back
Top Bottom