Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka mitano imepita tangu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu kushambuliwa, Jeshi la polisi limesema bado linaendelea kumsubiria mwanasiasa huyo na dereva wake.

Lissu ambaye anaishi nchini Ubelgiji alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Mkutano wa Bunge.

Baada ya shambulio hilo, Lissu alipelekwa Hospitali ya rufaa ya Dodoma kabla ya kuhamishiwa Nairobi nchini Kenya siku hiyo hiyo alikoanza kufanyiwa operesheni na baadaye kuhamishiwa nchini Ubeligiji anakoishi mpaka sasa.

Katika mtandao wake wa Tweeter leo Jumatano Septemba 7, 2022 Lissu ameadika risasi 16, miaka mitano na operesheni 25 baadaye, bado nimewakomalia na mapambano yanaendelea miaka mitano, nabaki kujiuliza maswali.

“Ni kwanini Serikali na Jeshi la Polisi hadi leo hawafanyi uchunguzi na kwanini nimenyimwa, nimenyimwa haki zangu za msingi ikiwemo matibabu,”

Mwingine aliyetoa ujumbe unaofanana na Lissu ni Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ambaye aliandika, “IGP na DCI ni vyema mkatumia siku ya leo, kutoa maelezo kwa umma ni kwanini hadi sasa waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu hawajakamatwa na lini mtaridhia wachunguzi”

Mwananchi Digital ilipomtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema uchunguzi wa kesi yeyote ya jinai unaweza kuendelea hadi pale waliofanya tukio hilo watakapopatikana.

“Watakapopatikana ndipo itajulikana nia ilikuwa ni nini kama Jeshi la Polisi lilivyowahi kusema uchunguzi wa tukio la Tundu Lisu bado tunaendelea nao kwa kukusanya ushahidi kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Tulishasema pia aje pamoja na dereva wake ili tupate maelezo yao kwani yatatusaidia kusonga mbele katika uchunguzi wetu,”amesema Misime.

Akizungumza na Mwananchi, Lissu amesema hata kama nchi haiko salama sio sababu ya yeye kutokurudi, kwani kurudi nchini kunahitaji maandalizi ikiwemo fedha.

“Huu ni mwaka wa tano kuishi nje sio jambo dogo, kufanya maandalizi kunahitaji muda na fedha pia, Rais aliahidi kunilipa fedha za matibabu lakini hazijalipwa hadi leo licha ya kusema niandike madai yangu,”amesema Lissu.

Chanzo: Mwanainchi.
-%20KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Duh!

Kwa hiyo victims ndio mashahidi wakuu, endapo wangevuta na uchunguzi nao ungejifia hapo...
 
Kuhusu malipo si aliwah kutuambia kwamba serikali ya Samia imemlipa fedha zake zote
 
Mengine unaachana nayo tu ilimradi uzima upo
Ni kwa maslahi ya Taifa kwa kufikia mwisho wa hili, ambalo ni tukio la kutisha zaidi kuwahi kutokea kwenye Makao Makuu ya Nchi yetu.

Kushambuliwa kwa Mbunge wa JMT akiwa Bungeni sio jambo dogo,ni jambo lililotia dosari Nchi yetu ya amani na upendo.

Lazima tupate closure kwenye hili, hata kama waliotenda watakuwa wamezikwa pembeni ya Ziwa.
 
Jeshi la polisi limesema bado linaendelea kumsubiria mwanasiasa huyo na dereva wake ili wawakamate na kuwahoji namna tukio lilivyotokea
Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo ninavyozidi kupata ufahamu namna hawa Wapinzania wanavyoshughulikiwa ili wadhalimu waendelee kuwatafuna jasho la Watanzania.

Inashindikana nini kwa jeshi la Polisi kuomba kupata maelezo ya mhanga wa tukio kutoka Ubeligiji bila kuathiri usalama wake? Interpol inaweza kutumika kuomba jeshi la polisi Ubeligiji wakaweka mazingira ya mahojiano baina ya Lisu na Polisi Tz kupitia hata njia za kidijitali au akatumwa afisa upelelezi kule akachukua maelezo kiaha akarudi nayo ili kazi iendelee.

Nilishaanza kuamini uhusika wa mamlaka kwenye hii kadhia. Afrika isiwaue thinktanks wake. Isiue wapinzani wake bali iweke mazingira ya kupambanisha fikra kwa maendeleo ya Afrika.
 
Back
Top Bottom