Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Kwa vile lengo lilikuwa kuonyesha kuwa dola ilitumika kwenye tukio lenyewe, wanaleta ngonjera kibao. Mara ulinzi uliondolewa, mara CCTV camera ziling'iolewa n.k. hizo zote ni visa vya kutunga ionekane dola ilihusika. Usisahau CDM wana uzoefu huo. Wakati wa Kikwete hao hao walijilipua kwa bomu kule Arusha na mtu akafa wakanyoosha mdomo kwa dola . Kwa DM lolote wanaweza kufanya. Hivi kama dereva yuko huko akiogopa kubambikwa kesi kwa nini mwanzo wasema anatibiwa kisaikolojia? Na kwa nini kauli aliyoitoa baada ya shambulizi pale Dodoma iwe tofauti na aliyotoa Ubeljiji alipohojiwa na DW Tv? Inabidi mtu ajivue ufahamu asipoona walakini katika hayo.
 
Je CCTV Camera hazikuondolewa??? Je eneo hilo la tukio hakuna ulinzi masaa 24???? Je ni hatua gani stahiki zilizochukuliwa na Serikali kuhusu tukio hilo??Msiwe mnajifanya mna akili sana mnatenda mambo kimakusudi halafu mnakuja na ngojera za kijinga pumbavu zenu tena kunguru ninyi,mlaaniwe mpaka mwisho wa dunia.
 
Mbona Lissu alitangaza kwamba alishalipwa stahiki zake zote?
Mbona mnatuchanganya?
 
Rubbish
 

Hapo umeanza kuandika kile unachokifahamu, yaani taaluma yako ya kufurumisha matusi. Umefika upeo wako wa kutoa hoja. Hizo CCTV camera zilikuwepo lini au kwa vile Mbowe kasema zilikuwepo zikatolewa na we waamini? Kumbuka Mbowe huyo huyo alisema waliolipua bomu kule arusha anawafahamu lakini hatawataja kwa vyombo vya dola ya TZ akataja watu ambao angeweza kuwatajia. Ngonjera za hawa CDM ni maelfu kwa maelfu. Kumbe wamejilipua wenyewe wanasingizia watu wengine. Kama mtu una akili zako sawa sawa hutaki kujiuliza kwa nini dereva afichwe kwa gharama kubwa jifikirie upya. Au hujiulizi kwa nini wadanganye eti dereva anatibiwa kisaikolojia wewe unaona sawa kudanganya jitahidi kuvaa upya ufahamu wako. Au hujiulizi kwa nini dereva abadilike wakati akihojiwa na DW Tv na kuongea kitu tofauti na alichoongea Dodoma mara tu baada ya tukio wewe waona ni sawa wakati zilishaanza kujengwa hija kuwa dereva alipelekwa Nairobi kufundishwa cha kusema pindi akihojiwa na polisi yote waona hakuna issue nikupe pole yako. Ndio maana hoja hizi zinapokosa majibu unarudi kwenye taaluma yako.
 
Acha ujinga wewe,Mbowe ni nani katika kile ninachokifahamu,upumbavu wenu wa kukumbatia akili za watu ndiyo unaowafanya muwe wajinga kwa sababu ukimpenda mtu hata kama anakosea makosa yake unayazima kwa sababu tu unampenda na ukimchukia mtu hata kama hana dosari unampa dosari kwa sababu tu humpendi.Huu ujinga utaendeleza kuwaachia makovu kwa sababu mnafikiria kwa kutumia makalio,matusi huja pale tu mtu anapozidisha kejeli na ukumbuke amani haija ila kwa ncha ya upanga.Unatumia elimu kama kisingizio cha kuonea watu eti kwa sababu wana elimu wavumilie maonezi na kejeli,hilo halikubaliki hata siku moja,mlitaka kumuua Tundu Lissu kwa kisingizio cha siasa chafu zilizoanzishwa na mwendazake na mnataka maridhiano ili muendelee kutukejeli,acheni ujinga.
 

Sasa mbona huongelei wala kujibu hoja yoyote? Kama huna hoj sio lzima uingie humu jamvini. Imagine kama una mke au watoto wnaona upuuzi ulioandika ukimaanish kujibu hoja uliwoikuotu (quite). Mbona unatakaa uonekane kioja mbele ya watu wanaowajibika kukuheshimu?
 
Umekuja na mihemko,soma vizuri hoja yangu na kama hoja yangu hujaielewa nenda kasome hivyo vifungu vya Katiba nilivyokuwekea vitakusaidia angalau kidogo,ila ukisimamia kwenye hoja yangu kwa vile unanidharau utabeza tu,basi kasome vizuri uulize Wataalam waliopo kwenye Chama chako watakuelimisha.
 
Angekuwa Mwenyekiti wa mtaa kutoka CCM katobolewa na toothpick muda huu kungekuwa na mtu au watu wanamechezea kifungo.

Bias ni kansa
 
Security camera zinaweza kufungwa lakini hakuna DVR/NVR ya kuhifadhi data za matukio yaliyopita na pengine anaweza tu kufunga kwa nia ya kutishia watu wenye nia ovu waghairi kutekeleza kitendo chochote kiovu baada ya kuona jicho la CCTV kumbe hazifanyi kazi ipasavyo.

Mtu kuondosha kamera mahali alipokuwa amezifunga lakini akabaini zilikuwa zimelengeshwa nje ya eneo linalotunza usalama wa faragha za mwingine pasipokuwa na kibali ndipo hondosha ili akafuate taratibu vizuri. Kwa kuwa ni kosa na mhusika anapokana kwamba alishawahi kuweka ni ngumu kuthibitisha kwamba zilikuwepo kama hakuna 'counter surveillance cameras' zilizofungwa eneo jingine kwa mtu mwingine ili kusaidia kurejea siku ya tukio endapo kinachodaiwa kweli kilitokea kwa hiyo hao wanaodai kwamba huo ulikuwa ushahidi hawawezi kuthibitisha maana walitakiwa waende mahakamani kudai mahakama iamuru mtu huyo binafsi atoe nyaraka inayotakiwa
 
Baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi zikaondolewa kwa vile zilikuwa hazijafungwa vizuri.
 
..Nategemea jeshi la Polisi litafungua uchunguzi wa shambulizi dhidi ya Tundu Lissu.
Yaani wajichunguze.? Labda sio polisi ya CCM.

Sidhani kama itatokea, ni mtu mjinga tu ndio atashindwa kupata connection ya wapanga mkakati hadi washambuliaji waliomshambulia Lissu.

Tukio lilifanyika kishamba sababu lilipangwa na washamba kwa mihemko binafsi ndio maana ukifuatilia kauli za baadhi ya wawili fulani kwa nyakati tofauti waliligusia hili bila kujua wameacha loop ya wanaotafakari kuujua ukweli.
 
Kwani hawawezi kufanya uchunguzi bila uwepo wa Tundu Antipas Lissu. Ina maana kama mtu akiuawa uchunguzi haufanyiki kwa vile muathirika hayupo?
Hivi swali hili polisi huwa wanalitolea majibu gani kweli...?

Maana polisi wetu wanaropoka kana kwamba wao tu ndiyo wanajua sheria huku wengine wote wakiwa ni wajinga...!
 
Mara ulinzi uliondolewa, mara CCTV camera ziling'iolewa n.k.
Kwani wewe unadhanije?

Kwamba siku ya tukio lile baya kabisa ulinzi wa Govt Quarters za Area D Dodoma ulikuwepo na Wala haukuondolewa..?
hizo zote ni visa vya kutunga ionekane dola ilihusika.
Yaani CHADEMA wanatunga visa kuwa Tundu Lissu alipigwa risasi huku ukweli ukiwa hakuwahi kupigwa risasi zozote, au....?
Usisahau CDM wana uzoefu huo. Wakati wa Kikwete hao hao walijilipua kwa bomu kule Arusha na mtu akafa wakanyoosha mdomo kwa dola.
Kama haikuwa hivyo, hebu tuambie, mpaka sasa ni mwana CHADEMA gani alikamatwaga na Kisha kufunguliwaga mashitaka na kukutwa na hatia na Kisha kufungwa jela fulani Kwa kulipua bomu hilo huko Arusha...?
Kwa DM lolote wanaweza kufanya. Hivi kama dereva yuko huko akiogopa kubambikwa kesi kwa nini mwanzo wasema anatibiwa kisaikolojia?
Kwani wewe unafikiri nini?

Tukio lile lilimuathiri kisaikolojia au lilimjenga kisaikolojia yule dereva...?

Kwamba, hufikiri kuwa ni kweli TANPOL wanaweza kulitumia tukio hilo kum - criminalize dereva ili kuisafisha serikali na tuhuma hizi...?

Ni mjinga pekee asiyeweza kuiona possibility ya serikali ya CCM Kwa kuwatumia Polisi kufanya hivi. And likely wewe ni miongoni mwa wajinga hao...!!
Na kwa nini kauli aliyoitoa baada ya shambulizi pale Dodoma iwe tofauti na aliyotoa Ubeljiji alipohojiwa na DW Tv?
Alitoa kauli gani zinazotofautiana Kwa mfano? Hebu leta nukuu ya kauli hizo kama kweli zipo na zinatofautiana ili tujadili hayo....
Inabidi mtu ajivue ufahamu asipoona walakini katika hayo.
Mimi nadhani wewe unafikiri Kwa kutumia kiungo kingine na siyo kichwa chako...!

Na kwa ujumla sitakuwa nimekukosea heshima kusema kuwa, wewe ndiye mbumbumbu wa mwisho kabisa kwa sababu unatumia hisia zako tu kujiandikia badala ya kutumia facts zilizo mbele yako zikikukodolea macho...!!

Tumia kichwa chako vizuri kufikiri ndugu..
 
..Lissu anarudi nchini wiki ijayo.

..sijui jeshi la polisi watakuja na kisingizio gani cha kutofanya uchunguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…