Jeshi la polisi laanza operesheni ya kubandua namba za magari za 3D

Jeshi la polisi laanza operesheni ya kubandua namba za magari za 3D

Punguza ujuaji, tulishatangaziwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita. Hizo namba ni lazima zifuate vipimo na specifications kama ilivyopangwa na TBS. Sasa wewe unachukua namba zimetengenezwa na kampuni iliyopewa kibali mfano Masasi signs unaongezea urembo wako ili iweje. Unakiuka vigezo vilivyowekwa na unatumia vikampuni vya mtaani ambavyo havina vibali vya mamlaka husika. Tujifunze kufuata sheria na taratibu, hizo 3D namba ni rahisi sana mtu kutemper nazo.
Bado hujaeleza zina shida gani??
Japo umemwambia Mjuaji..
Maana kama 3D ina tatizo labda inasababisha Ajali pia tujue
 
Kwa kuwa zinabanduka,zinaweza kutumia vibaya Kwa uharifu au kukwepa Askari wa usalama Barabarani.
Nadhani shida iko hapo
Vibao mbona vinabdilishwa sana mbona hatuachani navyo kwa sababu na vyenyewe vinauwezo wa Kufunguliwa na spana?

Watu wanabadili sana..
Miaka fulani ya 2000s watu walikuwa wanapiga sna Taxi bubu mchana anaweka plati ya njano usiku anaweka nyeupe na anaingia mzigoni..

Mbona hawakuzipiga marufuku Matumizi ya pleti ili namba ziandikwe kwenye Gafi upande wa kushoto mwa dereva..

Maana mpaka sasa sijaona point ya Kupiga marufuku 3D
 
Kwa mfano gari yanye namba T 838 ZZZ na ikawa imewekewa plate number ya 3D, ikiibiwa na kubadilishwa kuwa T 888 ZZZ ni kitu rahisi sana, kwani unabandua hiyo 3 unaweka 8 ndani ya sekunde chache tu.
Kwani mbona watu wanaiba Gari na wanabadili Plate nzima??
Hiyo sio sababu hata kidogo..
Watu wanaiba gari inapachikwa Palte ya trekta au ya gafi yiyote mbovu ngoma inasonga..

BAdo sioni sababu
 
Vibao mbona vinabdilishwa sana mbona hatuachani navyo kwa sababu na vyenyewe vinauwezo wa Kufunguliwa na spana?

Watu wanabadili sana..
Miaka fulani ya 2000s watu walikuwa wanapiga sna Taxi bubu mchana anaweka plati ya njano usiku anaweka nyeupe na anaingia mzigoni..

Mbona hawakuzipiga marufuku Matumizi ya pleti ili namba ziandikwe kwenye Gafi upande wa kushoto mwa dereva..

Maana mpaka sasa sijaona point ya Kupiga marufuku 3D
Ni vizuri ukatuelimisha umuhimu wa hizo number tuna,
Binafsi nadhani kuna udhaifu wa namna zinavyotengenezwa.
Design inaweza kuwa bora zaidi iwapo plate/ubao wa number ubonyezwe kutengeneza hizo number/herufi kuliko kubandika kwenye ubao either Kwa gundi au screws.
Ni vigumu Kwa number zilizobonyezwa kwenye plate kubanduliwa au kubadilishwa Kwa vyovyote.
 
Kwani zina athari gani?
Sisi Tanzania hatujafikia kuwa na namba ukubwa huo wa 3D. Kama Kenya wao wana 4D kabisa ni manamba makubwa.

Yule mchapishaji wa namba Masasi aliwahi kuomba serikalini awe anachapisha unene huo wa 3D,alikataliwa.
Kwa hiyo hata hawa walivyoanza kuziboard kwa ukubwa wa 3D ni kama wanamharibia pia Masasi. Na yeye kaenda kukandamiza,wanaharibu kazi yake
 
3 D ndio nini na ina madhara gani??
1709120790156.png

Hii ndio 3D number plate katika picha. Kifupi 3D inamaanisha kitu chochote kilichokuwepo katika picha katika vipimo vitatu. Upana x urefu x Kina. Namba plates zetu za awali zilikuwa na vipimo viwili, yaani urefu x upana.

Madhara: Sijui kama 3D inamadhara yeyote, nafikiri ni suala la polisi kushirikishwa tu katika hili. Na ni suala la muda tu kabla hawajaruhusu 3D. Binafsi sioni kwanini wajipe kazi ya kukamata magari hayo.

Faida: 3D huonekana kwa uzuri zaidi kama unavyoiona katika picha.
 
Ni vizuri ukatuelimisha umuhimu wa hizo number tuna,
Binafsi nadhani kuna udhaifu wa namna zinavyotengenezwa.
Design inaweza kuwa bora zaidi iwapo plate/ubao wa number ubonyezwe kutengeneza hizo number/herufi kuliko kubandika kwenye ubao either Kwa gundi au screws.
Ni vigumu Kwa number zilizobonyezwa kwenye plate kubanduliwa au kubadilishwa Kwa vyovyote.
Sasa mimi nimeuliza Kwanza nipewe madhara wewe unataka miseme umuhimu wa 3D..?

Mkuu wewe ni.Mgeni mjini na Plate namba kubadilishwa haijalishi imetoka wapi ila huwa zinabadilishwa sana waru wakiamua lao
 
3 D ndio nini na ina madhara gani??
Kuhusiana na madhara ni kwamba wataalamu wanavyosema ni kwamba katika mfumo wa kuzisoma hizo namba huwa zinaleta changamoto kwa matrafiki Barabarani kulingana na mashine wanazotumia wao, hizi za kawaida zinasomeka kwa urahisi hata gari ikiwa umbali mrefu na hata msomaji akiwa angle tofautitofauti, lakini kwa namba za 3D inakuwa shida kidogo
 
Back
Top Bottom