Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Bahati mbaya kicheko hicho kitamuumiza zaidi baadae mana Pale kuna Makamo mkiti na Mkiti ambao wana misimamo mikali sana...Halima aliwahi kusema watu hao wawili yaani Lisu na Heche kama wajumbe wa kamati kuu ndio wanaowakanyagia ili wasirejee sasa kama wamepewa rungu inakuaje??
 
Mimi hapa ndio simuelewi Lissu. Hivi kweli anaamini kuwa kama kungekuwa na fomu zozote Ndugai angezificha? Hiyo si ndio ilikuwa nafasi ya kumuumbua aliye zisaini na kukivuruga kabisa CDM? Kauli kama hizi za kichonganishi ndio zinanifanya nikose imani nae. Kwangu mimi wakina Halima na Esther ni bora mara kumi ya Msigwa na Slaa ambao ni rafiki zake. Hawa wanawake katika muda wote huu hawajawahi kukitukana chama chao wala viongozi wao. Lakini hao anao wakumbatia walifanya juhudi za wazi kukichimba chama chake.

Ningekuwa yeye ningetangaza ruhusa kwa yeyote ambae kwa sababu yeyote alikuwa nje ya chama kurudi kwenye familia. Mbona waliweza kumkubali mpambanaji Aidan? Kwa hawa wanashindwa nini?

Amandla...
Mkuu mbona ametoa conditions kuwa wakitubu na kueleza ukweli waliendaje endaje bungeni basi watasamehewa. Ameweka msingi kwenye neno "UKWELI" kama kigezo cha msamaha. Anayeamua sio yeye ni Mkutano Mkuu kwahiyo kasema kina Mdee wanafahamu wanachopaswa kufanya ni kuomba upya uanachama huko, na wakikiri watasamehewa.

Otherwise sishauri awarudishe, loyalty ni muhimu kuliko kura.
 
Mjumbe wa kamati kuu, na Lisu ni Mjumbe na Mwenyekiti, chama siyo mali yake, yeye hana kauli ya mwisho.
Nani amesema chama ni mali yake, all lissu anataka ni taratibu zifuatwe. Hao walipata ubunge in who name?

Taratibu za chama hazikufuatwa why? Nani alihusika ku sign?

KAma chama akifuati katiba yake, kitaweza kufuata katiba ya nchi kweli?
 
Unachanganya kuwa loyal kwa mtu na kudharaulika. Mtu anaweza kudharauliwa na kadamnasi lakini watu wake wakawa bado wako loyal kwake.

Amandla...
Ndio nasema hao Covid 19 wasipokua Loyal kwa Lissu watadharau na chama. Hata Mbowe kama angeshinda watu nao wangekiacha chama huwezi separate mwenyekiti kuheshimiwa na chama kuheshimiwa.

Sasa kama wanaweza mkejeli tu mwenyekiti unadhani wataweza heshimu kamati kuu au wanachaka wa kawaida?

Loyalty is greater than votes
 
Lissu inatakiwa awe na busara tu kwan hajui magufuli regime ilikuaje ?aache mihemko aisee nao ni wahanga kama yeye
Wameambiwa waende mkutano mkuu ndio wenye maamuzi, waache kona kona mbona simple tu. Ila mimi binafsi siungi mkono haya maana kitaweka precedence mbaya sana.
 
Mkuu mbona ametoa conditions kuwa wakitubu na kueleza ukweli waliendaje endaje bungeni basi watasamehewa. Ameweka msingi kwenye neno "UKWELI" kama kigezo cha msamaha. Anayeamua sio yeye ni Mkutano Mkuu kwahiyo kasema kina Mdee wanafahamu wanachopaswa kufanya ni kuomba upya uanachama huko, na wakikiri watasamehewa.

Otherwise sishauri awarudishe, loyalty ni muhimu kuliko kura.
Lissu atajuaje kama wanasema ukweli au uongo? Au tayari anaujua ukweli na anachotaka ni watu wakiri tu? Wakiri nini? Hiyo sio justice hata siku moja.

Wote tunajua kuwa wajumbe wengi wa hiyo mikutano wanafuata muelekeo wa Mwenyekiti wao. Wengi ni loyal kwa tafsiri yako.

Kwa mtazamo wangu, Lissu anageuza kichuguu kuwa mlima Kilimanjaro. Kwangu mimi anaonyesha kuwa ni petty na vindictive. Na ni mtu anaesikiliza sana umbeya na fitna. Anawezaje kuwashikilia bango wakina lakini akawa kimya kwa watu kama:
1. Slaa ambae aliandika mpaka kitabu ambamo alituhumu kuhusika kwa CDM kwenye mambo ya utekaji. Na kuwa hamna haja ya mikutano ya hadhara baada ya uchaguzi.
2. Msigwa ambae anasimama kwenye jukwaa kuwaaminisha wananchi kuwa CDM imeoza na haistahili kupewa dhamana ya kusimamia dola.
3. Yule mbunge aliyedai kuwa CDM ndio walimpiga risasi.
4. Waitara ambae wakati akiwa Naibu Waziri Tamisemi aliwa hujumu sana katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
5. Lijualikali aliyelia Bungeni kuhusu uozo wa CDM na ambae mpaka sasa hivi anaendesha vita dhidi ya CDM.
6. Upendo Peneza ambae nae alianza na moto wa kuichafua CDM ingawa sasa amepoa.

Kwangu mimi hawa wamesababisha maumivu zaidi kwa chama kuliko wakinq Halima.

Anapaswa kusamehe kwa dhati na aache kuwasikiliza wapambe ambao wana agenda zao. K.m. wakati anazungumzia jinsi anavyomheshimu Mbowe anachomokea tuhuma za mamia ya mamilioni kuingizwa kwenye uchaguzi.

Alipozungumzia kuponya majeraha amezungumzia yale ya loyalists wake tu. Mambo kama watu kuenguliwa bila sababu. Hakuzungumzia kabisa lugha⁶ za matusi na uongo zilizotumiwa na wapambe wake!

Amandla...
 
Uko nchi gani Mkuu? Walishafukuzwa mda sana, wabunge wasio na chama, wamelindwa na mfumo tu.

Bunge linajua bado ni Wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA, na je walifukuzwa kwa barua au kuna legal document yoyote ilitolewa na CHADEMA
 
Anawezaje kuwashikilia bango wakina lakini akawa kimya kwa watu kama:
Kuna yeyote hapo ameomba kurudi chadema? Mbona kaulizwa kuhusu Dr Slaa na akasema ndio alihusika kumleta Lowassa na Mbowe asilaumiwe, na alisema hayo akiwa kwenye mdahalo wa uenyekiti, na wakati huo Dr Slaa yupo jela na mind you alikua Team Lissu, So unaweza ona ambayo Lissu yupo direct kwenye ukweli.
Wote tunajua kuwa wajumbe wengi wa hiyo mikutano wanafuata muelekeo wa Mwenyekiti wao. Wengi ni loyal kwa tafsiri yako.
Sio kweli, 48% wamemchagua Mbowe so wanaweza mkatalia misimamo yake.
Kwangu mimi hawa wamesababisha maumivu zaidi kwa chama kuliko wakinq Halima
Recency bias, mtu kama Dr Slaa alifanya hayo miaka 10 iliyopita ila Mdee bado anafanya hayo mpaka leo hii, nani hapo anastahili clemency akiomba kurudi chadema?

Hata Msigwa it's obvious ameenda CCM sababu ya kuwa frustrated na Mbowe na ndio maana hata interview zote ameonyesha kumkubali Lissu na hivyo Lissu akiwa mwenyekiti kuna chances akarudi.

Hao kina Mdee vipi? Wamewahi kuwa apologetic kwa chama zaidi ya kejeli na dharau mind you wametupeleka hadi mahakamani!! Unawasamehe vipi?

Ni hivi hawa sio wa kuwasamehe, haiwezekani kina Ruge na Sharifa wapambane na BAWACHA kipindi hiki cha dhiki alafu oktoba waenda tena kina Mdee bungeni!! Itakua injustice, hao wahuni wote wasirudishwe na wakirudishwa wakae benchi tu hakuna free lunch
 
Wameambiwa waende mkutano mkuu ndio wenye maamuzi, waache kona kona mbona simple tu. Ila mimi binafsi siungi mkono haya maana kitaweka precedence mbaya sana.
Hapana ila wale jua walifosiwa na utawala wa wakati huo ebu fikiria mmoja alikamatwa akatolewa kwa shart la kuingia bungen wangefanyaje sasa
 
Hapana ila wale jua walifosiwa na utawala wa wakati huo ebu fikiria mmoja alikamatwa akatolewa kwa shart la kuingia bungen wangefanyaje sasa
Ndio waje kukiri sasa kama walivyoambiwa na Lissu!! Wasipoongea ukweli hakuna mjumbe atakubali warudishwe.
 
Halima Mdee ameonyesha emoji mbili za kucheka 😃😃 kupitia mtandao wa X katika taarifa inayomuonyesha Lissu akiongelea kuhusu msimamo wake dhidi ya wabunge hao 19

Pia soma >Tundu Lissu: Nipo tayari kuwapokea wabunge 19 wa Viti Maalum walioingia bungeni bila baraka za chama
View attachment 3213007
FAM alishindwa na TAL atashindwa and he knows it

TAL amewaongopea sijui kuwafukuza na blah blah kibao

Hawafukuziki kama mnavyojitapa hapa

Kundi maalumu la wanawake,halafu sio wepesi ni women heavy weights CDM repercussions zake wakifukuza these women ni severe,

watatandaza sumu kwamba wanawake wapo marginalized CDM and people will believe that shit,pia kuna ACT which complicates things even further!

Uchaguzi ni just few months away,CDM cant afford to empower ACT by giving these women to ACT,maana ACT will just be number one opposition party in TZ for free

These women are powerful and they know how to win elections,most of them will go back to the parliment kupitia ACT

This is a blunder waiting to happen.
 
Kuna yeyote hapo ameomba kurudi chadema? Mbona kaulizwa kuhusu Dr Slaa na akasema ndio alihusika kumleta Lowassa na Mbowe asilaumiwe, na alisema hayo akiwa kwenye mdahalo wa uenyekiti, na wakati huo Dr Slaa yupo jela na mind you alikua Team Lissu, So unaweza ona ambayo Lissu yupo direct kwenye ukweli.
Amesema hivyo lakini bado yuko nae. Tatizo kubwa la Dr. Slaa sio kumleta Lowassa bali ni kukichafua chama alipokuwa nje ya chama. Anapaswa kuomba msamaha au kusema kuwa aliyokuwa akisema yote ni kweli na CDM ina au ilikuwa na kikundi cha utekaji. Hilo Lissu hajalizungumzia kabisa.
Sio kweli, 48% wamemchagua Mbowe so wanaweza mkatalia misimamo yake.
Recency bias, mtu kama Dr Slaa alifanya hayo miaka 10 iliyopita ila Mdee bado anafanya hayo mpaka leo hii, nani hapo anastahili clemency akiomba kurudi chadema?
48% ya Baraza Kuu sio 48% ya Mkutano Mkuu. Mimi sielewi hicho mnachosema anakifanya Halima mpaka sasa. Hivi kuhudhuria kwake Bunge kunaondoaje uhalali wa CHADEMA? Mbona Aidan aliendelea kuhudhuria hata baada ya kuambiwa asihudhurie? Na juzi amesimamia uchaguzi wa Bawacha kwa umahiri mkubwa. Angeshikiwa bango ili afukuzwe kwenye chama kama wakina Halima hasara ingekuwa kwa Chadema. Kuna madiwani wa CHADEMA bado wanahudhuria vikao vya Halmashauri zao. Wote hao hamuwaoni, mnawaona wakina Halima peke yao? Kwangu mimi wote ( wakina Halima, Dr. Slaa n.k.) wanastahili kusikilizwa kama wataomba msamaha bila kuwekewa masharti ambayo hawataweza kutimiza.
Hata Msigwa it's obvious ameenda CCM sababu ya kuwa frustrated na Mbowe na ndio maana hata interview zote ameonyesha kumkubali Lissu na hivyo Lissu akiwa mwenyekiti kuna chances akarudi.
Msigwa angehamia chama kingine cha upinzani nisingekuwa na tatizo nae. Amehamia kule kule kwa washindani wao wakubwa kwa sababu tu anamchukia Mbowe. Huyu akigombana na Lissu si atarudi CCM au atakuwa anawapelekea siri za CDM. Hivi ingekuwa Sugu ameshindwa halafu akahamia CCM mngeimba wimbo huu? Si mngesema alilamba asali. Kwa nini hamsemi hilo kwa Msigwa?
Hao kina Mdee vipi? Wamewahi kuwa apologetic kwa chama zaidi ya kejeli na dharau mind you wametupeleka hadi mahakamani!! Unawasamehe vipi?
Wametoa wapi kejeli. Wameenda mahakamani kupinga kufukuzwa kwao. Hapo tatizo liko wapi?
Ni hivi hawa sio wa kuwasamehe, haiwezekani kina Ruge na Sharifa wapambane na BAWACHA kipindi hiki cha dhiki alafu oktoba waenda tena kina Mdee bungeni!! Itakua injustice, hao wahuni wote wasirudishwe na wakirudishwa wakae benchi tu hakuna free lunch
Nani amesema kuwa wakina Halima wakisamehewa wapewe pia nafasi za uongozi? CDM watakuwa na haki kabisa ya kuwaweka kwenye probation ambapo hawataruhusiwa kugombea nafasi yeyote na watabaki kuwa wanachama wa kawaida.

Amandla...
 
Amesema hivyo lakini bado yuko nae. Tatizo kubwa la Dr. Slaa sio kumleta Lowassa bali ni kukichafua chama alipokuwa nje ya chama. Anapaswa kuomba msamaha au kusema kuwa aliyokuwa akisema yote ni kweli na CDM ina au ilikuwa na kikundi cha utekaji. Hilo Lissu hajalizungumzia kabisa.
Yuko naye wapi? Dr Slaa alitoa maoni yake huko pembeni ila sijawahi ona popote yupo na Lissu publicly au mikutano ya chadema na hata jana alipotaja timu ya ushindi hakumtaja Dr Slaa. Huwezi chagua supporters wako, ila sio partners wako.

Ila siku akitaka kurudi chadema obvious lazima aende mkutano mkuu na akajieleze hayo.
48% ya Baraza Kuu sio 48% ya Mkutano Mkuu
Lissu alichaguliwa na mkutano mkuu, na uanachama wa Mdee unarudishwa na Mkutano Mkuu PEKEE!! sasa hiyo 48% ya mkutano mkuu inaweza pinga au kubali so sio kweli watafuata kila anachosema Lissu.
wanastahili kusikilizwa kama wataomba msamaha
Mbona ndio Lissu kasema, waombe msamaha na kukiri kosa kwani kipi kigumu.
Hivi kuhudhuria kwake Bunge kunaondoaje uhalali wa CHADEMA? Mbona Aidan aliendelea kuhudhuria hata baada ya kuambiwa asihudhurie? Na juzi amesimamia uchaguzi wa Bawacha kwa umahiri mkubwa. Angeshikiwa bango ili afukuzwe kwenye chama kama wakina Halima hasara ingekuwa kwa Chadema. Kuna madiwani wa CHADEMA bado wanahudhuria vikao vya Halmashauri zao. Wote hao hamuwaoni, mnawaona wakina Halima peke yao? Kwangu mimi wote ( wakina Halima, Dr. Slaa n.k.) wanastahili kusikilizwa kama wataomba msamaha bila kuwekewa masharti ambayo hawataweza kutimiza.
Kwani Mdee wamefukuzwa kisa kwenda bungeni au MCHAKATO waliotumia? Mie naamini kabisa maridhiano yalipoanza chadema walishakubaliana kina Aida na madiwani waende bungeni so hata wabunge wa viti maalum wangepelekwa muda huo. Sasa wao mchakato waliotumia ni forgery na ni criminal charges kabisa ni tofauti na Aida ambaye alikua na uhalali kisheria! Hao kina mdee walikua na uhalali gani? Hawajadhaminiwa na chama, hawajakua endorsed na kamati kuu na hata walipofukuzwa bado walibakizwa bungeni bila kuwa na udhamini wa chama!! So ni mambo mawili tofauti kabisa KISHERIA.
 
Msigwa angehamia chama kingine cha upinzani nisingekuwa na tatizo nae. Amehamia kule kule kwa washindani wao wakubwa kwa sababu tu anamchukia Mbowe. Huyu akigombana na Lissu si atarudi CCM au atakuwa anawapelekea siri za CDM. Hivi ingekuwa Sugu ameshindwa halafu akahamia CCM mngeimba wimbo huu? Si mngesema alilamba asali. Kwa nini hamsemi hilo kwa Msigwa?
Hata Msigwa akirudi Lissu hana mamlaka ni Mkutano Mkuu, na obvious lazima aombe radhi na kueleza kwanini alihama!! Wakimuelewa watamrudisha so hao kina Mdee hakuna shortcut ni lazima wakiri
 
Wametoa wapi kejeli. Wameenda mahakamani kupinga kufukuzwa kwao. Hapo tatizo liko wapi?
Wewe ulisema walienda kisa kutishiwa na JPM, sawa mbona hawakusema hayo Baraza Kuu? Wamefukuzwa wanaenda kukishtaki chama maana kwenye hati ya mashtaka bodi ya wadhamini chadema ilishtakiwa. Sasa mnafanya forgery na bado mnaishtaki taasisi mnategemea nini.
 
Mimi hapa ndio simuelewi Lissu. Hivi kweli anaamini kuwa kama kungekuwa na fomu zozote Ndugai angezificha? Hiyo si ndio ilikuwa nafasi ya kumuumbua aliye zisaini na kukivuruga kabisa CDM? Kauli kama hizi za kichonganishi ndio zinanifanya nikose imani nae. Kwangu mimi wakina Halima na Esther ni bora mara kumi ya Msigwa na Slaa ambao ni rafiki zake. Hawa wanawake katika muda wote huu hawajawahi kukitukana chama chao wala viongozi wao. Lakini hao anao wakumbatia walifanya juhudi za wazi kukichimba chama chake.

Ningekuwa yeye ningetangaza ruhusa kwa yeyote ambae kwa sababu yeyote alikuwa nje ya chama kurudi kwenye familia. Mbona waliweza kumkubali mpambanaji Aidan? Kwa hawa wanashindwa nini?

Amandla...
Kwani hujui kuwa walishajadliwa kuanzia kamati kuu, Baraza kuu na mkutano mkuu na kote huku wakaridhika kuwa wamefanya makosa na adhabu ya kuwavua uanachama iliwastahili...?

Unataka kuaminisha watu kuwa watu wote kwenye ngazi zote hizo walioridhia adhabu yao hawana akili waliwaonea tu hawa kina mama...?

Na unajua Mwenyekiti mpya kasema nini..?

Ameulizwa na kujibu kuwa, hana mamlaka ya kuwarudisha hata kama watamfuata na kumlilia kwa sababu walifukuzwa na chombo kikuu (Baraza kuu) na hilo ndilo lenye hukumu la kuwarudisha tena likiona inafaa...

Hata hivyo, alitoa maoni yake, kusema kuwa utawasamehe vipi watu ambao hawaoni wala kukiri makosa yao? Akamalizia kusema waje, wafungue mioyo yao, wafanye kitubio na waseme kwa uwazi;

1. Walienda endaje bungeni..?

2. Walitoa wapi fomu za Tume (NEC) maana zilizoletwa kwa GS zipo mpaka leo..?

3. Nani aliwasainia hizo fomu maana GS John Mnyika anasema hakuwahi kufanya huo uhuni..?

4. Nusrat Hanje alitokaje gerezani na ghafla tu kuonekana ktk uchochoro fulani huko Dodoma mbele ya Job Ndugai - Spika wa Bunge (by then) akiapa kuwa mbunge wa viti maalumu? Alijaziwa fomu na nani, wakati gani na wapi..?

## Wewe ungekuwa ndiye Tundu Lissu usungekuwa na msimamo huu pia..?

## Huoni kuwa huu ni msimamo dhabiti wenye lengo la kutibu uhuni na ufisadi wa kimadaraka ndani ya CHADEMA..??
 
Back
Top Bottom