Jibu la Halima Mdee kuhusiana na msimamo wa Lissu juu ya Wabunge 19 (COVID 19)

Wamekutuma eti.
Mbowe is no longer the chairman.
 
Sasa ulitaka Kigaila na Mwalimu wasubiri nini wakati tayari wameishateuliwa watu wengine kushika nafasi zao?
Mbonà Kigaila hakuaga kabisa, alitoweka kimya kimya. Pia Salum Mwalimu aliomba asiteuliwe ukatibu Mkuu!! Walijishtukia kabla hawajafikiwa.
 
Hahaha hujielewi wewe na Lisu wako, Simpangii lakini asilopoke. Wabunge wa viti maalum chadema mnaowaita covid19, wanatambulika ndani ya chama labda Lisu ajitoe akili tu kutafuta umaarufu.
Wameshafukuzwa mbona na baraza kuu, sio wanachama
 
Mbonà Kigaila hakuaga kabisa, alitoweka kimya kimya. Pia Salum Mwalimu aliomba asiteuliwe ukatibu Mkuu!! Walijishtukia kabla hawajafikiwa.
Mwalimu hakutukanwa kama Kigaila. Kigaila karibu washikane mashati na Lema Arusha. Kigaila alisingiziwa kuwa anawanyima vitambulisho wajumbe wa Lissu. Kigaila ameambiwa mara kibao kuwa haaminiki kwa sababu ya mke wake. Ilikuwa wazi kabisa kuwa Lissu asingeendelea nae. Na watafanya kila juhudi kumpaka matope. Lakini mlitaka asimame kinafik na kuwaaga? Mwalimu protegee wake amemrithi.

Sasa unakiri kuwa kulikuwa na ajenda ya kuwashughulikia. Wanachofanya wakina Lissu ni ku alienate watu wenye uwezo mkubwa na commitment kwa chama kwa sababu ya petty grievances. Ita backfire tu. To paraphrase them " mkimaliza kuwashughulikia wakina Kigaila na Mwalimu mtaanza kushughulikiana wenyewe". Na ndio, kulikuwa na mpango wa kumshughulikia Mrema lakini kuna mtu akawa na pupa. Sio vizuri wanavyofanya. Wanaendeleza yale waliyomfanyia Mbowe kwa watu wanao amini ni watu wake badala ya kujaribu kushirikiana nao. Halafu wanazungumzia kutibu majeraha!

Amandla...
 
Acha uongo ndugu yangu.
Chadema haipokei ruzuku kupitia wabunge wa Covid 19. Wawepo au wasiwepo ruzuku ya Chadema ipo pale pale. Soma sheria na kuelewa.
 
Kuropoka kwake ndio kumempa uwenyekiti, kukaa kimya kwa mbowe kumemnyima uenyekiti, lisu akikaa kimya, watamtukana amepoa
 
Mimi hapa ndio simuelewi Lissu.
Na mimi hapa ndio sikuelewi Fundi Mchundo! Kwa kawaida mstaarabu akivuliwa nguo huchutama!
Hivi kweli anaamini kuwa kama kungekuwa na fomu zozote Ndugai angezificha?
Thubutu, Ndugai ilibidi azifiche kwa sababu ama alijua au alishirikishwa katika njama hizo toka awali.
Hiyo si ndio ilikuwa nafasi ya kumuumbua aliye zisaini na kukivuruga kabisa CDM?
Hapana, lengo halikuwa kuivuruga Chadema tu, lengo kubwa lilikuwa kuzipa legitimacy CCM na bunge lake fake. Ndugai hakuwa na namna.
Kauli kama hizi za kichonganishi ndio zinanifanya nikose imani nae.
Mbona hili linaeleweka hata kwa kipofu...uliyekuwa humtaki awe, amekuwa. Kwa wingi wa wenye imani nae kwa sasa, upende usipende, ndiye mwenyekiti
Kwangu mimi wakina Halima na Esther ni bora mara kumi ya Msigwa na Slaa ambao ni rafiki zake
Sidhani kama hata unaelewa unachokisema. Kwa taarifa yako, hao Covid-19 walishavuliwa uanachama kwa usaliti wao lakini Msigwa na Slaa walijiondoa Chadema kwa sababu na kujiunga na CCM in protest!
Ningekuwa yeye ningetangaza ruhusa kwa yeyote ambae kwa sababu yeyote alikuwa nje ya chama kurudi kwenye familia.
Hapana, sikubaliani na wewe. Kama wanaipenda Chadema waombe kwanza msamaha halafu waombe upya uanachama.
Mbona waliweza kumkubali mpambanaji Aidan? Kwa hawa wanashindwa nini?

Amandla...
Kwani Aidan kosa lake nini? Je kugombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema na kushinda ni kosa?
 
Low IQ
 
Kwani lissu anajibizana nao au yeye aliulizwa na mwandishi ??
 
Nawashauri covid19 warudi kundini ili kukijenga chama. Mzee rudi tafadhali, napenda umachachari wako.
 
Chadema inapokea RUZUKU kutokana na hao wabunge tunowaita Covid19. Halafu yeye anajidai HAWATAMBUI, akae kimya.
Chadema haipokei ruzuku kutokana na Covid-19. Chadema inapokea ruzuku kutokana na idadi ya Watanzania walioipigia kura...wewe ndio unatakiwa ukae kimya.
 
Na watafanya kila juhudi kumpaka matope. Lakini mlitaka asimame kinafik na kuwaaga? Mwalimu protegee wake amemrithi.
Aaah sasa kwanini hakuaga kama alikua msafi? Yaani alikimbia mara tu uchaguzi unaanza!!

Wala hakuna mpango wa kuwashughulikia ila kuna mpango wa "enquiry" kivipi wake za Mwalimu, Kigaila, na Mrema walienda bungeni!!

Sasa unakimbiaje kama unaongea ukweli.

Kigaila is a disappointment
 
Acha uongo, kwamba wanawake wapokee wabunge 19 alafu oktoba nani atapata fursa ya kuingia bungeni? If anything hao wakifukuzwa ina maana viti zaidi ya 20 vitakua free kwa BAWACHA.
 
Hao hawapaswi kurudishwa hata mmoja kwenye uchaguzi ujao
 
Labda nikusaidie tu kidogo, kinachowapa Ruzuku Chadema siyo hao wabunge wa viti maalum walioko bungeni. Bali ni asilimia za kura za wabunge ambazo Chama kilipata kwenye uchaguzi mkuu. Hivyo hata kama kusingekuwa na mbunge hata mmoja wa Chadema lakini provided wamefikisha asilimia kuanzia Tano ya kura za wabunge waliogombea majimboni, still wangepata Ruzuku.

Asilimia hizo ndizo huwa pia zina kokotolewa kupata idadi viti maalum vya wabunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…