Jifunze njia nzuri ya kufanya manunuzi kwenye mtandao (Ebay, Amazon, Bestbuy)

Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. Baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo.

Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni;

1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address

2: Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania)

3: Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3: KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4: KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?

Hii iko hivi....

1: Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted.

2: Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.com. Hii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.

Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao

Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2: COMGATEWAY
Link: Shop the US Online and Ship Internationally | comGateway - Hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na huona wana policy nzuri sana, cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani, hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3: BORDERLINX
Link: Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx - Hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... Wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..Hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4: SHIPITO
Link: USA Address & Mail Forwarding Shipito.com | English - Hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5: STACKRY
Link: Stackry - US shopping, global shipping - Hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi.

STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU , Please evaluate kindly.

Nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila I think there are limits..

Help Mwl.RCT
Hizi shule za bure namna hii ukipita bila ya kushukuru ni dhambi kubwa. Shukrani sana mkuu.

Sasa sisi slow learners ni shida kidogo, ninaomba kujiridhisha hapa. Kwahiyo, kama nimeelewa, kuna hatua /taasisi tatu utapaswa kufanya nao kazi, mfano: AMAZON = MYUS.COM=DHL. Hapa nipo sahihi?

Kuna mahali umesema kuna ada ya kijiunga na huduma ya DHL? Yani nitalipa ada kisha nitalipa gharama za kusafirisha mzigo, sivyo? Bila ya kutaja kampuni, gharama ya kusafirisha mzigo kama simu yaweza kufikia kiasi gani kwa makadirio?

Shukrani sana
 
Welcome! Our services include:

  • Web design
  • Logo design
  • Online business or company registration
  • Airline and Bus ticketing (Domestic & International)
  • Passport and Visa Registration
  • Studying abroad programs
  • Online imports and export services
  • And other IT related services
 
Here some EcoActs plastic poles 3.3inch x feet 8 cost 24,500, which are suitable for farm fencing making, gardens making and road signs, our poles they do not rot, terminate free, long lasting, strong and durable, more info contact through 0757671874 email amtatina@ecoact.co.tz
IMG_20211102_094639_072.jpg
 
Mzigo unachajiwa kulingana na kg na thamani,unalipia kwanjia za kawaida bila usumbfu card za visa au ukiingia kwenye menu ya Tigo au M-pesa unachagua jina la kampuni unalipia
Kg sh ngap mfn vipodoz?
 
Samahan Wana jf nilikuw naombaa msaada kwa mweny uelew kuhus biashar ya kuagiza mzigo kutoka china mfano vyombo , blender,pazia na vingne naombaa kupat msaada natak nianze kuagiza
 
Samahani, naomba kujua hizi ni bei kweli? Na kuna changamoto gani unaweza pata ukinunua gari kupitia hapa?
Screenshot_2021-12-12-22-08-18-07_a04944f99a062af0791c9039e89fa6b9.jpg
 
Habari zenu wakuu, Katika kuhitaji kwangu TV na Fridge ila kutokana na ufinyu wa budget ikaniwia ugumu kuvipata vyote Kwa hapa kwetu Tanzania maana bei za hapa zimechangamka Sana

Nilijaribu kuulizia Zanzibar ila sikupata Msaada na kujikuta nachungulia Kwa majirani zetu Kenya, ndipo nilipokutana na hawa mabwana Instagram wakijiita Alibaba online store Kenya, nikacheki bei zao nikaona ziko vizuri kusema ukweli

Nikawacheki DM na kutaka kujua ni utaratibu upi wanatumia Katika uuzaji wao vifaa nchini kwetu Tanzania, wakasema wanafanya delivery Kila siku na delivery ni bure, na unafanya malipo kwanza Kisha unapewa tracking number unakuwa una track mzigo wako

Nikawauliza kama Wana branch Tanzania ili niende nikajiridhishe kabla ya kutuma pesa yangu na kupotelea kusikojulikana ila wakasema hawana, na wanaingiza vitu vingi tu Tanzania, nikaona ngoja nije Kwa ndugu zangu kutaka ushuuda au chochote kile ambacho kinaweza kunisaidia kabla sijafanya maamuzi

Nimejaribu kumtafuta yule jamaa alileta Uzi Kuwa yuko Kenya na anataka kutusaidia wa Tanzania kutuagizia vitu kutoka Kenya Kisha tunampoza kidogo ili akanichekie hiyo ofisi ya hao jamaa na apate uhakika kama kweli wanatuma vitu Tanzania Kwa ukweli ila bado sijafanikiwa kuongea nae, hivo wakati namsubiri nimeona muanze kunisaidia hapa jukwaani

Screenshot_20220218-094847.jpg
 
Sasa mkuu si uwafate alibaba wenyewe kwenywe website yao
 
Back
Top Bottom