Kwa wanunuzi wa bidhaa mtandaoni hapa nazungumzia Aliexpress na Alibaba huu ni uzi maalum wa kujifunza kuagiza bidhaa kupitia mtandao huu hususan Aliexpress. Mjuavyo Aliexpress ni mtoto wa Alibaba
Alibaba imebase kwenye kuuza bidhaa za jumla huku aliexpress wakibase kuuza bidhaa za rejareja na mojamoja kwa mteja
Ndio mtandao unaokuwa kwa kasi na umekuwa na wanunuzi wengi kupita hata Amazon na Ebay
Kupitia uzi huu nimeanzisha hili tuweze kupeana elimu na maarifa kuhusu manunuzi kupitia hizi site kama walivyofanya wenzetu walivyoanzisha uzi wao tukajifunza kuhusu Ebay
Natumai wataalam na wenye uzoefu mpo humu na mtajibu maswali ya wengi wetu tunaopenda kufahamu zaidi na kujifunza kuhusu aliexpres
Na maswali mengi yatabase kwenye kila kitu
Mfano mpaka bidhaa imfikie muhusika, gharama, system ya malipo, muda, na uimara wa bidhaa n.k
Karibuni sana wadau