Ukweli ni kwamba Mwanza ni mji baada ya Dar es Salaam,mimi naishi Mwanza na ninafanya kazi Arusha, hii miji miwili inataka kama kufanana lakini Mwanza inaendesha mambo makubwa kuliko Arusha kuanzia uchumi wa watu na mengineyo..pia ina watu wengi zaidi kuliko Arusha,idadi tu ya watu ni tosha kuifanya ikue kiuchumi,nowdays Arusha imekosa watalii na imebaki kama kijiji cha ujamaa,ni vile tu watu hupenda kuvutia kwao lakini Mwanza ni zaidi ya Arusha,hata watu wenye pesa Mwanza ni matajiri wakubwa sana lakini kamwe huwezi kuwasikia na mambo ya hovyo mitaani,Hapa Arusha kijana ana milion 100 tu ni kero mitaani,kutwa kucha na Difender barabarani au Subaru na miungurumo mikibwa,ile ni ushamba japo wao wanaona ni kama ujanja lakini ni ushamba na akili za kimasikini. Mwanza ina jumla ya wilaya nne zilizoingia zote mjini.. Misungwi, Magu, Nyamagana na Ilemela, ni mji mkubwa wa madini,uvuvi na kilimo pia biashara zingine maana Mwanza inahudumia kanda ya ziwa yote ukijumuisha Tabora,Shinyanga,Musoma,Simiyu na Kagera japo Kagera huchanganya Mwanza na Kampala kibiashara lakini wote hao center yao ni RockCity.
Tchao