Halafu huyu jamaa anayejiita Hesabu900 ni bonge la mshamba. Mayor ni diwani tu (ward councilor). Na yeye ni binadamu kama wengine na anavutiwa na pisi kali pia. Mayor alikuwa anakuja workshop kupiga misele kama raia wengine tu japo alikuwa na body guard. Kwa hiyo pisi kali kama Khumbu akikutana nayo kitaa lazima aiimbishe. By the way South africa kuwa na gari sio issue, kila mtu mwenye kipato au mwenye kazi ana gari. Hata hao anaowaita wauza mitumba wa Karume wanauza mitumba huku wamepaki magari ya maana pembeni. Mwambieni aache ushamba, Khumbu kuwa na gari sio big deal, angeweza hata kujinunulia mwenyewe kama angetaka. South africa wanatengeneza magari na kuna hela ya kutosha mpaka vijijini huko. Huko vyuma havijakaza kama huku bongo. Kifupi South africa kuwa na gari sio issue. Karibia kila familia ina gari. Hiyo exposure anayoiongelea sijui ni ipi kama anaona mayor kutembelea V8 ni kitu cha ajabu kwa nchi kama South africa. Shame on him!