Jinsi matapeli wa mjini wanavyotumia "harusi" kupiga pesa; inauma sana

mbinu ya kipumbavu kabisaa hiiii,,, mi naistukiaga mapema...naweka ushabiki wote pembeni najituliza tuliiiii
Mkuu wewe ni mimi kabisa. Huwa sishiriki mashindano ya rejareja kama haya. Hata kanisani wachungaji hupenda kuyatumia wakati wa kuchangisha michango mbalimbali. Mimi nabaki kuwa mtazamaji tu!😂😅🤣
 
Ili usiweze kuchanga mchango wa harus hakikisha hauwekwi wala kujiunga kwenye kikundi chochote cha kusaidiana kwenye shida na raha au toka utokewe,iwe kazini,mtaani,makanisani (uwe mwenyewe tu kwenye mambo zako)
Unaweza usijiunge na kikundi chochote lakini, from no where, ukajikuta unaletewa kadi mkuu.
 
Kinachofanya kuwe na gharama kwenye HARUSI ni nini mpaka muhusika achangiwe?. Sichangii HARUSI. Naamini muhusika alipaswa kujipanga namna sherehe yake itakavyokuwa kulingana na uwezo wake.
Sio uungwana unapiga hesabu zako za bajeti alafu unatafuta watu wakukufikisha kwenye lengo. Hata kama sio utapeli sio uungwana pia.

Sasa pesa ni kuchangie na muda wangu siku ya tukio niwepo ? Kivipi sasa.
 
Ni ajabu mtu anaanda harusi ya 60M lakini anatumia only 20M huku 40M inayobaki anatanulia mjini. Hii sio sawa hata kidogo mkuu.
 
Siwezi kuchangia harusi na sijawahi, yaani uamue kuoa kwa sherehe kubwa kwa kutegemea hela za wengine huo ni wazimu. Nilioa sikuchangisha mtu na sichangii mtu. Kuna jamaa yangu hadi leo ana madeni makubwa kwa kutegemea michango ya harusi.
 
Hayo madeni yaliingiaje wakati yeye ndiye aliyekuwa anachangisha fedha mkuu?
Yeye kwenye harusi ali plead kama milioni tano ili kuweka ulimbo wa kuwavuta watu wachangie. Kamati ikaweka bajeti kama milioni 45. Mwisho wa siku wachangiaji wakachanga chini ya kiwango na huku walishakodi maukumbi,MC na watu wa chakula. ilibidi akakope kausha damu kmmk.
 
Du! Kiherehere hakijawahi kumuacha mtu salama aisee!😂😅🤣
 
Siwezi kuchangia harusi na sijawahi, yaani uamue kuoa kwa sherehe kubwa kwa kutegemea hela za wengine huo ni wazimu. Nilioa sikuchangisha mtu na sichangii mtu. Kuna jamaa yangu hadi leo ana madeni makubwa kwa kutegemea michango ya harusi.
Upo sahihi kabisa mkuu. Juzi Ronaldo alimaliza harusi yake mwenyewe bila kuwasumbua watu. Hata mama yake hakuhusishwa na wala hakushiriki.

Kuchangishana hii michango ya kibwege ni chanzo cha umaskini. Kama mtu huna uwezo kwanini ufanye harusi ya gharama kubwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…