Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Jinsi ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Nimezungumza huko juu kwamba zoezi hili la kukamua, ni mila tu na desturi iliyorithiwa toka kwa wavamizi wa Kiarabu na sio maagizo au mafundisho ya Dini flani.
Huko Uarabuni sio Waarabu wote wanaotekeleza hili zoezi.

Kama ni fundisho la Dini mtu aje na Aya au Hadithi ya kuthibitisha hoja hii.

Jamiiforum ni jukwaa lenye kuhudhuriwa na watu waliostaarabika. Na ni jukwaa lenye heshima na mchango mkubwa wa kujifunza maarifa mbalimbali.

Mtu kuandika Mada na kuiweka humu bila chanzo cha habari inachukuliwa kama ni Pororojo au Udaku flani tu.

Kama ni Siri za Dini basi zisiletwe humu, zibakie hukohuko kwenye kwenye Siri za Dini

Hapa habari zenye mashiko na za kuaminika ni zile tu zinazo ambatana na chanzo husika cha hiyo habarMriri

Nimezungumza huko juu kwamba zoezi hili la kukamua, ni mila tu na desturi iliyorithiwa toka kwa wavamizi wa Kiarabu na sio maagizo au mafundisho ya Dini flani.
Huko Uarabuni sio Waarabu wote wanaotekeleza hili zoezi.

Kama ni fundisho la Dini mtu aje na Aya au Hadithi ya kuthibitisha hoja hii.

Jamiiforum ni jukwaa lenye kuhudhuriwa na watu waliostaarabika. Na ni jukwaa lenye heshima na mchango mkubwa wa kujifunza maarifa mbalimbali.

Mtu kuandika Mada na kuiweka humu bila chanzo cha habari inachukuliwa kama ni Pororojo au Udaku flani tu.

Kama ni Siri za Dini basi zisiletwe humu, zibakie hukohuko kwenye kwenye Siri za Dini

Hapa habari zenye mashiko na za kuaminika ni zile tu zinazo ambatana na chanzo husika cha hiyo habari.
Hili tuliite povu au uzumbukuku?

Unasema habari inaletwa bila chanzo, ulivyoelezwa kuwa chanzo cha yaliyotajwa hapo juu ni Hadithi za mtume(directly) na Qur'an(indirectly) hukuelewa?
Au unahitaji hizo hadithi uzipinge na zenyewe?
 
Wewe usiye zumbukuku basi tuwekee hapa hiyo hadithi tuisome kama inaamrisha kukamua mavi ya maiti.
Napenda watu wenye Hekima kama wewe.
Mi nasema tena na tena na narudia tena kwamba.

[emoji117]Hakuna andiko la Dini yoyote lililo ruhusu hicho kitendo.

Mimi siwezi kupinga maandishi yaliyo andikwa iwe Aya au hadithi.

Basi nasubiri hiyo Aya au hadithi ya mtume ni amini kuwa wewe sio Zumbukuku.
La sivyo ni vema tu ukaacha kuropoka mambo usiyo yajua.
 
Chondechonde ndugu zanguni.
Hizi tofauti za kiimani zisitufanye kuvunja ushirikiano wetu. Tubishane, lakini tuendelee umoja kama binadamu na kama watanzania.
Imani tumeletewa. Na tukianza kuzifuatilia zote zina kasoro za kuibia maswalu ya kujiuliza. Rai yangu.
hamna tofauti ila msibani hatuli tena
 
Unazngua bhna na hii comment yako ya ukorofi yaan nia yako wahusika wachukie wakujibu kwa jazba muanze kupanik na kutukanana eti kisa dini umeshindwa kusoma tu na kupita uwaache wenye Imani yao wajadili Kama wengine walivyofanya?, hiyohyo dini yako unayoiona ipo sahihi zaidi Ina watu waovu kupita maelezo Sasa dini ni Nini hapo?? Sio vizur kujitoa fahamu mkuu
Hayo Mavi wanayokamua ni ya muhimu sana maana Kazi mojawapo huwa yanatumika kumuita Jini makata
 
Unazngua bhna na hii comment yako ya ukorofi yaan nia yako wahusika wachukie wakujibu kwa jazba muanze kupanik na kutukanana eti kisa dini umeshindwa kusoma tu na kupita uwaache wenye Imani yao wajadili Kama wengine walivyofanya?, hiyohyo dini yako unayoiona ipo sahihi zaidi Ina watu waovu kupita maelezo Sasa dini ni Nini hapo?? Sio vizur kujitoa fahamu mkuu
Mzee kwani unadhani nimedanganya/nimetunga?
 
Unazngua bhna na hii comment yako ya ukorofi yaan nia yako wahusika wachukie wakujibu kwa jazba muanze kupanik na kutukanana eti kisa dini umeshindwa kusoma tu na kupita uwaache wenye Imani yao wajadili Kama wengine walivyofanya?, hiyohyo dini yako unayoiona ipo sahihi zaidi Ina watu waovu kupita maelezo Sasa dini ni Nini hapo?? Sio vizur kujitoa fahamu mkuu
usishughulike nae huyu Citizen B namjua vzr anachuki sana na Uislamu

Note:ukicomment ujinga sitokujibu@Citizen B
 
Kama Allah anafanya haya hapa , tuuchukulieje uislamu
19.83 Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashet'ani kwa makafiri wawachochee kwa uchochezi?
Mkuu nini hii? Hivi inawezekana mungu akawa anatabia za ajabu ajabu hivi?
Lakini hapana, Mungu ninaemwabudu mimi ni Mungu mwenye upendo na huruma sana. Kila mara huniepusha na hatari za mashetani.
 
Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua​

1.Kuoshwa (Kukoshwa).
Mazingatio kabla ya kuosha maiti.

(a)Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
  • Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
  • Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia

(b)Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.

(c)Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
1. Muoshaji awe muislamu.
2. Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
3. Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
4. Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa ‘gloves’.
5. Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.

(d)Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:

1. Nia
2. Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.

Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.

iii.Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.

iv.Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.

v.Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.

vi.Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.

vii.Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi.
- Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.

viii.Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.

ix.Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.

x.Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.

xi.Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).

xii.Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka zitakate.
- Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong’oka
ziambatanishwe na sanda.

xiii.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.

xiv.Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.

xv.Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.

xvi.Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.

xvii.Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa).

Source: Bongoclass.com kupitia mafundisho matukufu ya Qur'an pamoja na sunnah za Mtume(s.a.w)
Tufuate sunna za bwana Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake)
 
Back
Top Bottom