DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hahaha amesema hivyo ili kukufanya uelewe kwa urahisi mkuu, haimaanishi kama kwa siku binadamu anaconsume.
[emoji23][emoji23][emoji23]JF ni jukwaa la great thinkers,Sasa kuna Sababu gani ya kusema jambo kwa kuzunguka??.
 
Hata upungufu wa akili nao sidhani, mimi nadhani tunakosa utu, uzalendo na kujaliana. Tunapenda kufaidi na kunemeka ktk hali ya ubinafsi zaidi!
Ukiacha maziwa na mito, nchi hii maji yamejaa kila mahali ardhini. Mto kama Ruvu unaonywesha Dar historia yake inafahamika toka enzi; baada ya cycle fulani ni lazima uwe na upungufu wa maji.

Kwa hali kama hiyo unahitaji kusuburi ili uje "kufanya maombi"? Mungu akupe nini zaidi wakati akili za kutawala mazingira yako alishakupa? Tena ni juzi tu msimu wa masika mwaka huu huu mvua zilitapakaa kila kona ya nchi hii hadi tukaomba "atupe mvua za kiasi"?

Tuna akili sawa sawa kweli?
 
Kuna vitu mkuu ukijiuliza na kutathmini umri wa taifa letu unabaki kuguna bhasi tu. Kwa miaka yote hii utoaji wa huduma muhimu za kijamii kama maji, elimu, umeme bado ni kizungumkuti. Labda tumelaaniwa bila kujijua!
 
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Nakubaliana nawe kwa mengi uliyoyaandika. Ila pale penye ukubwa pana hitilafu kidogo. Nadhani ukubwa unaozungumzia ni kina cha hayo maziwa. Lake Baikal lililopo huko Urusi linaongoza kwa kuwa na kina kirefu zaidi hapa Duniani. Ni kweli Lake Tanganyika ni la pili. Ila kwa ukubwa wa eneo hali ni tofauti.
 
Ukubwa halisi wa kitu hupimwa kwa ujazo(volume) na si eneo. Hilo ndilo linafanya Baikal kuongoza kwa ukubwa duniani. Ndilo linafanya Tanganyika au Nyasa kuwa makubwa kuliko Victoria.
 
Takwimu iliyonishangaza ni hii ya nyasa kulizidi victoria karibia mara tatu na ushee!
Jamani nikiangalia kwa macho mbona inakataa?

Sent using Jamii Forums mobile app
... in its simplest definition, volume (V) = length (L) x width (W) x height (H); V = L x W x H. Now, since L x W = Area (A) then; V = A x H.

Lake Victoria: large A but small H hence small V.
Lake Nyasa: small A but large H hence large V.
Note: a small change in H has drastic effect on change of V.
 
Shukrani kwa kurahisisha. Nafikiri hata hii elimu ya kukaririshana kuwa ziwa Victoria ni kubwa inatakiwa kurekebishwa.
 
Nimekuelewa sawasawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani kwa kurahisisha. Nafikiri hata hii elimu ya kukaririshana kuwa ziwa Victoria ni kubwa inatakiwa kurekebishwa.
... uko sahihi. Hata hivyo, ukubwa wa Ziwa Victoria unaozungumziwa kwenye elimu yetu umezingatia zaidi ukubwa wa eneo (surface area) badala ya ujazo (volume). Ni suala la kuamua jamii inapaswa ipate ujumbe gani; ukubwa wa eneo au ujazo?
 
Upo sahihi ila nia yake ni kulipa sifa na msisitizo zaidi jambo aliloliongea. Kama kwa siku lita 100 na tutakunywa kwa miaka kibao, je hizo lita 3 kwasiku maanake tutakunywa maelfu ya miaka.
Sawa bhana.
 
Jamani! Hivi mkuu katika bajeti yako ya matumizi ya familia hapo nyumbani, huwa unatenganisha watoto na wakubwa?

Kwanza lazima uje mtoto ana matumizi extra kuliko mtu mzima, iwe kwa maji ama chakula.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo mtoto anatumia lita mia moja kwa Siku??.Hivi kwa familia yenye watu kumi kwamba watatumia lita 1000???.
 
Back
Top Bottom