Niliwahi kumfuata mke wa rafiki yangu na kumwambia aache tabia ya kuchepuka, ni kjmdhalilisha mumewe na yeye mwenyewe. Alinijibu "yanakuhusu nini? Au na wewe unanitaka? Kamwambie basi mume wangu kama unajiona unahuruma sana.
Nilimwomba radhi na kukaa kimya. Tayari kabeba mimba ya mchepuko.
Miaka ilipita, tabia kama ngozi, ikaonekana. Mume alinitaka ushauri. Nilishindwa kushauri zaidi ya kumwambia avumilie huenda atabadilika. Hakubadilika licha ya mume kumsihi aache.
Hatimaye mume alinyoosha mikono. Ndoa ikafika mwisho.
Naamini sikuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya rafiki yangu.