Jeshi kama jeshi linajua linafanya nini.1 mpaka 800 ni wachache? Jipeni matumaini ila muda huo ni lazima tuwe makini
Tutawagawana hao wakijaribu kutuletea fyokoHalafu ujue vijana 800 ni sawa jeshi la nchi kwa baadhi ya nchi hapa duniani
Bro habari. Walitumika vipi kuvuruga uchaguzi... Ndio walikua wanalinda polling stations nchi nzima?Hawa ndio walitumika kuvuruga uchaguzi,acha wapate malipo yao.
Kwa akili yako unadhani ISIS na vikundi vingine walifukuzwa JKT kwa utovu wa nidhamu?Nimesoma habari moja kuwa JKT imesitisha mikataba na kuwafukuza vijana zaidi ya 800 baada ya kuandamana Ikulu wakinishinikiza kuajiriwa...
Itakua waliwapima hao mia 8 wakawa UNFIT wakawakata ...Kama Kurudishwa wangerudishwa wote 2400 mmechagua watoto wa maskin hao 800 mnawaita waasi hao watoto wa wakubwa ndio mmeona wanafaa haya bwana mtaji wa maskin
Mkuu umeongea point sana, pia akiota kinyama wanamuita UNFIT.Mtu anaweza kugoma jeshini hafai mwanajeshi hagomi
Walikula chakula chenye sumu au walifia kwenye kozi wajenzi wanavumbi sana kifuani ndio mana wanawakwepa... wanawatumia kwenye ujenzi wanawaharibu baadae wanawaita UNFIT
Kwahiyo hata wakiwa watovu wa nidhamu wavumiliwe eti kwasababu ya gharama? Dogo umesoma kwa kiwango gani au na wewe darasa la Musukuma?βTunasikitika kufuta mikataba ya vijana 854 wa JKT kutokana na kufanya vitendo vya uasi.βMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania - Jenerali Venance Mabey
---
Wanawatumia vibaya sana bila vifaa vya kulinda afya ... vijana waamke wasikutegemee sana JAKATAMkuu umeongea point sana, pia akiota kinyama wanamuita UNFIT.
Halafu hizo OP zinazojenga hawawezi kwenye mafunzo ya ukomando kisa vumbi la cement
JKT siyo sehemu ya kutoa ajira, tunarudia kila mara hamuelewi dah
RTS ni nini chief?Kugoma jeshini ni swala ambalo halikubaliki. Pili JKT siyo sehemu ya kwenda kuajiriwa unaenda kufundishwa stadi mbalimbali za maisha, ukakamavu na uzalendo.
Zipo OP kadhaa hapo nyuma wamerudishwa majumbani je mpaka sasa umeona vipi? Mpaka kufikia hatua unarudishwa ishafanywa tathimini kubwa sana. Walichokipata ni intro tu vitamu uanzia RTS na kuendelea.
Hao vijana wengi sio raia wa TanzaniaKuna wakati gharama haiangaliwi, hasa linapokuja swala la majeshi au tuseme ulinzi na usalama. Hao vijana hawatoshi kuwa askari kwa gharama yoyote ile.
Sure mkuu .....kinachowaponza ni ...wakiwa course huwa wanawaponda sana police ........kuna wimbo utaskia "haiwezekan kurut kupigwa na police"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. So ndoto zao ni kuwa soldiers [emoji23][emoji23]Miaka 3 mkuu sio 6 weeks
Aisee ktk ujinga wanafanya service man ni huu yaani woote uwa wanawaza kuingia Jwtz tu ssa watachukua wangapi wataacha wangapi ata polisi,maliasili wakienda kambini kufanya usaili mijitu inakimbia kujificha eti wanasubiri JW waje wafanye usaili dadek acha WANYOOKE na WATANYOOKA TU
Jeshi haliajiri linaandikishaππ. (Enlist not employment)Uliwahi kuajiriwa jeshini?
Kama hukuwahi nyamaza tu
Kuna watu wanaonewa na wakubwa wao mpaka mtu anakosa uvumilivu anakoki silaha jeshi lisikie kwa watu, kama upo huko basi uko position ya juu huonewi ndio maana uko comfortable
Na hili mimi ndio nimelisema pia sehemu Fulani humu. Watu walikua 2400 kazi zimepungua nyie 800 mnapelekwa sehem nyingine hata misheni haijakamilika(Ikulu haijaisha) halafu unagoma unalazimisha upelekwe RTS kweli walipelekwa huko ila walichokutana nacho wameomba warudi nyumban wenyeweKatika swala hili nimeona watu wengi wakijadili kwa mlengo wa kuwaonea huruma hao vijana waliotimuliwa JKT
Tukirudi nyuma, hii haikuwa ahadi ya kwanza kwa vijana wa JKT. Kuna wale waliojenga ukuta wa mererani nao pia walipewa ahadi Kama hii.
Tukitumia mfano huo wa waliojenga ukuta wa mererani tunaweza kujua Kama hao vijana walikurupuka au wameonewa
Kwanza inabidi tukubaliane kuwa jeshini au Taasisi yoyote wa namna yao ya kuajili watu wao. Haiwezekani ahadi itoke tu (tena kisiasa) halafu siku hiyo hiyo woooote wasajiliwe! Sidhani Kama huo ni utaratibu! Jeshi Kama jeshi wana vigezo vyao na taratibu zao lakini zaidi nao wanaajili kulingana na bajeti na uhitaji
Wale walioahidiwa baada ya kujenga ukuta wa mererani, sio kwamba baada ya kumaliza ujenzi wa ukuta basi kesho yake waliajiliwa na majeshi mbalimbali, HAPANAAA!
Kilichofanyika baada ya mkataba wao wa kujitolea kuisha wao waliendelea kubaki kwenye makambi mbalimbali ya JKT wakati wale ambao hawakuwa kwenye orodha ya ahadi ile walirudi nyumbani baada ya mkataba
Waliendelea kutumiwa bila malipo yoyote kusubilia utekelezaji wa ahadi waliyopewa mara pale kutakapokuwa na uhitaji na majeshi yetu na bajeti zitakaporuhusu kuajili nguvu kazi nyingine
Wapo walioshiriki kujenga hiyo hiyo ikulu katika hatua za mwanzo, wengine walijenga ukuta kule Kizuka TPDF na walikaa zaidi ya miaka mitatu baada ya ahadi ya Rais bila kuajiliwa na jeshi
Kulipotokea uhitaji wengi wao hadi sasa wamekwisha ajiliwa!
Nini nataka kusema?
Kuna watu walibeza kauli ya Ndugai juzi bungeni kuhusu vijana ya kutokuwa na uaminifu, lakini ile kauli si ya kubeza
Vijana wengi siku hizi ni wajuaji sana na wako speed mno!
Hawana subira wala hawana muda wa kutafakari kitu katika mapana yake
Wale vijana waliojenga ukuta wa mererani, Kuna vijana watatu nawafahamu walifikia hatua ya kutaka kukata tamaa!
Kwanza walikuwa graduate na mmoja wao alikuwa na mke na mtoto hivyo alifikia hatua ya kuona anapotezewa muda!
Katika kumpa moyo, swala pekee nilikuwa namuuliza ni "Kama unahis hawatawaajili, kwanini wamewabakiza kambini na wengine wameondolewa??
Hao vijana walikurupuka na hawafai kuwa wanajeshi.
Kwangu Mimi wangetimuliwa baada ya kugoma kurudishwa nyumbani kushinikiza kwamba waliahidiawa ajira na Rais ningekuwa upande wao kwa asilimia zote kwasababu ni ngumu sana jeshi kuja kuwachukua mtaani na kuwapa ajira, lakini hawakufukuzwa kambini! Walibakishwa kuendelea kusubiri ahadi wakati wale wengine wasio na ahadi walisharudi makwao
Ni kawaida majeshi kuwatumia sehemu mbalimbali pale wanapowahitaji ilimradi tu wako mikononi mwa jeshi na hakuna aliyesema ahadi waliyopewa ni batili!
Kwa hiyo wao walitaka wabaki hapo hapo chamwino hata Kama hamna kazi za kufanya??
Au walitaka kwasababu Rais katoa ahadi waajiriwe siku hiyo hiyo hata Kama hakuna uhitaji?? Wakiajiliwa wakakosa mshahara si utakuwa mgogoro mwingine!??
Tuwajengee vijana uwezo wa kupambanua mambo kwa kina kabla ya kuchukua hatua kwa mihemuko
Hata kazi waliyokua wanafanya haijaisha mkuu mbona watu wengi hamlioni hili???Tuangalie pande zote za shillingi. Tangu Mhe. hayati Magufuli awaahidi kuwa wataajiriwa imepita muda mrefu na mpaka sasa hawaajariwa. Natumaini wamefuatilia sana ili waajiriwe lakini Serikali bado ilikaa kimya. Kama Hayati Rais alitamka waajiriwe ni kwa nini hawajaariwa?. Natumaini kusubiri kwao ndo imeleta enough is enough.
Shida kubwa wengine wanaongea bila kuangalia uhalisia wa mambo na hawajui kinachoendelea kisa uongo uongo adi jeshini. Makosa ya namna ya kuajiri vijana toka jkt ilianza baada ya uongozi wa awamu ya tano kuingia.
Vijana wanapmaliza mafunzo ya miezi sita ya awali walikua wanatawanyishwa kwenye makambi mbalimbali yaliyopo chini ya jwtz kwa ajili ya uzalishaji mali na ulinzi kama sehemu ya malezi.
Wakiwa kwenye makambi ya malezi ndipo jeshi..magereza..usalama..bot..takukuru n.k wanakwenda kufanya recruitment wa vijana hawa kulingana na sifa wanazohitaji pindi wakiwa na uhitaji na kwa kwenda kwenye makambi yote ya malezi.
Shida ikaanzia kipindi cha magufuli; yeye alitoa amri wa kuajiriwa waliojenga Ukuta Marerani lakini waliokua wanalima mpunga Chita..wanaolinda mipaka huko Kigoma na Uganda na Rwanda hakuona kama wanasifa ya kuajiriwa..waliokua wanalima mahindi huko Mgambo Tanga hakuona kama wanastahili kuajiriwa sijui alifikiri wote waje Mererani kujenga ukuta bila kuwepo mgawanyo wa ki majukumu.
CDF na mkuu wa jkt wakajikalia kimya bila kuona kuna upendeleo kwenye ajira.
Watu wenye uwezo wakawapanyika vijana wao humo humo na ikawa rushwa ndani ya jeshi.
Ujenzi ulipoanza tena Chamwino stori ikawa ile ile waajiriwe wanaojenga ukuta..hao CDF na mkuu wa jkt wakawa kimya tu; vijana waliopo makambi ya mbali wakawa na vilio mbona wanaajiriwa wa Dodoma tu? then wenye michongo wakafanya wanavyojua vijana wao wakaja nao Dodoma kwenye ujenzi.
Uchaguzi ulipowadia pia wanachukuliwa vijana kwenda kuaribu uchaguzi kwa upendeleo huohuo kua wataajiriwa.
Sasa leo wanawaona kama wanaketa uasi. Swali ni je kwanini hawakushauri Magufuli kipindi hicho kuhusu ajira? wamwambie kua wao wanataratibu zao za kuwapatia vijana wa jkt ajira?
Mambo ni mengi ngoja niishie hapa.