Katika swala hili nimeona watu wengi wakijadili kwa mlengo wa kuwaonea huruma hao vijana waliotimuliwa JKT
Tukirudi nyuma, hii haikuwa ahadi ya kwanza kwa vijana wa JKT. Kuna wale waliojenga ukuta wa mererani nao pia walipewa ahadi Kama hii.
Tukitumia mfano huo wa waliojenga ukuta wa mererani tunaweza kujua Kama hao vijana walikurupuka au wameonewa
Kwanza inabidi tukubaliane kuwa jeshini au Taasisi yoyote wa namna yao ya kuajili watu wao. Haiwezekani ahadi itoke tu (tena kisiasa) halafu siku hiyo hiyo woooote wasajiliwe! Sidhani Kama huo ni utaratibu! Jeshi Kama jeshi wana vigezo vyao na taratibu zao lakini zaidi nao wanaajili kulingana na bajeti na uhitaji
Wale walioahidiwa baada ya kujenga ukuta wa mererani, sio kwamba baada ya kumaliza ujenzi wa ukuta basi kesho yake waliajiliwa na majeshi mbalimbali, HAPANAAA!
Kilichofanyika baada ya mkataba wao wa kujitolea kuisha wao waliendelea kubaki kwenye makambi mbalimbali ya JKT wakati wale ambao hawakuwa kwenye orodha ya ahadi ile walirudi nyumbani baada ya mkataba
Waliendelea kutumiwa bila malipo yoyote kusubilia utekelezaji wa ahadi waliyopewa mara pale kutakapokuwa na uhitaji na majeshi yetu na bajeti zitakaporuhusu kuajili nguvu kazi nyingine
Wapo walioshiriki kujenga hiyo hiyo ikulu katika hatua za mwanzo, wengine walijenga ukuta kule Kizuka TPDF na walikaa zaidi ya miaka mitatu baada ya ahadi ya Rais bila kuajiliwa na jeshi
Kulipotokea uhitaji wengi wao hadi sasa wamekwisha ajiliwa!
Nini nataka kusema?
Kuna watu walibeza kauli ya Ndugai juzi bungeni kuhusu vijana ya kutokuwa na uaminifu, lakini ile kauli si ya kubeza
Vijana wengi siku hizi ni wajuaji sana na wako speed mno!
Hawana subira wala hawana muda wa kutafakari kitu katika mapana yake
Wale vijana waliojenga ukuta wa mererani, Kuna vijana watatu nawafahamu walifikia hatua ya kutaka kukata tamaa!
Kwanza walikuwa graduate na mmoja wao alikuwa na mke na mtoto hivyo alifikia hatua ya kuona anapotezewa muda!
Katika kumpa moyo, swala pekee nilikuwa namuuliza ni "Kama unahis hawatawaajili, kwanini wamewabakiza kambini na wengine wameondolewa??
Hao vijana walikurupuka na hawafai kuwa wanajeshi.
Kwangu Mimi wangetimuliwa baada ya kugoma kurudishwa nyumbani kushinikiza kwamba waliahidiawa ajira na Rais ningekuwa upande wao kwa asilimia zote kwasababu ni ngumu sana jeshi kuja kuwachukua mtaani na kuwapa ajira, lakini hawakufukuzwa kambini! Walibakishwa kuendelea kusubiri ahadi wakati wale wengine wasio na ahadi walisharudi makwao
Ni kawaida majeshi kuwatumia sehemu mbalimbali pale wanapowahitaji ilimradi tu wako mikononi mwa jeshi na hakuna aliyesema ahadi waliyopewa ni batili!
Kwa hiyo wao walitaka wabaki hapo hapo chamwino hata Kama hamna kazi za kufanya??
Au walitaka kwasababu Rais katoa ahadi waajiriwe siku hiyo hiyo hata Kama hakuna uhitaji?? Wakiajiliwa wakakosa mshahara si utakuwa mgogoro mwingine!??
Tuwajengee vijana uwezo wa kupambanua mambo kwa kina kabla ya kuchukua hatua kwa mihemuko