JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama mbona wapo kwa maelfu mitaani na hakuna tabu yeyote.
 
Fursa kwa vijana na beti watakao ingia mwaka huu lazima watoboe.
 
Mimi nimeshangaa sana vijana hao kujipanga kufanya maandamano bila intelijensia ya jeshi kuwabaini mapema na kuwadhibiti.Hivi jeshi letu siku hizo likoje?
 
Dawa ni moja tu, piga pini bidhaa zote toka China, shusha bei ya umeme, uone kama kuna mtu atakosa ajira nchi hii
Akipiga Pini hizo bidhaa za China, wewe utatazizalisha na kukidhi mahitaji sokoni? Sukari tu ya Kilombero na Mtibwa imetushinda kushusha Bei, alizeti tu mafuta yake hayashikiki fikiria tena
 
Jambo jingine linalonishangaza ni kuwa vijana hawajui kuwa kuingia jeshini ni kusaini kuwa wakati wowote upo tayari kufa kwa risasi au bomu. Wao nadhani wanafikiri kujiunga na jeshi ni kwenda kula bata ndiyo maana wanalazimisha kuajiliwa.
 
Sasa mtaani wanaenda kufanya nini ?
Kwani wewe unafanya n mtaani au yule mtoto wa dada yako anafanya nn mtaani.? Kwani jkt wamefundisha intake(operation) ngapi na sio wote walipata ajira. Je wamekua magaidi? Acheni mawazo mgando kutaka tu kuonesha mna huruma na vijana hao.
 
Mtoa maada uelewe kuwa lengo la JKT ni mafunzo ya ukakamavu, uzalendo na kujitegemea (ndio maana unafunzwa shughuli kama kilimo n.k).

Pili element muhimu ya kwanza ya askari yeyote ni UTII na NIDHAMU. KUGOMA ni kinyume kabisa na maadili ya askari. Kuruta mwenye tabia hizi hatakiwi kabisa kuwa jeshini.

Huwezi fuga muasi jeshini kwa kuhofia eti watakuwa magaidi. Hawa ni magaidi tayari. Btw, recruitment ya isis sio kama kampuni ya mlinzi. Usidhani jeshi halijui juu ya hofu hii na kuna monitoring kubwa juu ya hao isis.

btw, mbona kuna jkt kibao wako mtaani miaka yote.
 
Kwani wewe unafanya n mtaani au yule mtoto wa dada yako anafanya nn mtaani.? Kwani jkt wamefundisha intake(operation) ngapi na sio wote walipata ajira. Je wamekua magaidi? Acheni mawazo mgando kutaka tu kuonesha mna huruma na vijana hao.

Afuu huu ni uchochezi pia ndyo maana nikamuuliza huko ISS unakosema watajiunga unawasemea ?? Kama wao hawana wazo hilo watafanya shughli zingine
 
Hawakuwa jeshini bado walikuwa mgambo tu hao.
Kwa tabia walizoonyesha ni hatari zaidi wakiajiriwa jeshini.
 
Hawakuwa jeshini bado walikuwa mgambo tu hao.
Kwa tabia walizoonyesha ni hatari zaidi wakiajiriwa jeshini.

Hakika hawakuiva katika mafunzo yao bora wameonyesha rangi zao mapema wangeingia kwa system ingekuja kuleta shida badae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…