Job Ndugai ndani ya Western Wall of Jerusalemu

Job Ndugai ndani ya Western Wall of Jerusalemu

Jamaa mjanja. Kaenda kufuata baraka. Jamaa nimeanza kumkubali. Dhambi zake zote zimesamehewa. Nami natamani ningepata iyo fursa. Yani jamaa kabahatika kuwa kama myahudi. Kumbe inawezekana ukawa myahudi.

Hongera sana Job.

STRUGGLE MAN Bwana Utam
Slavery mentality, aliyewadanganya hilo taifa ni teule aliwaharibu akili....anyway huna haki ya kumsemea dhambi zake maana nawew unazo zako.

Waafrika amkeni, hakuna taifa teule duniani litokanalo na ngozi nyeupe.

Hayo majitu mnayoyapa thamani ya uteule ni majizi kama majizi mengine.

Kufuata Miungu ya wayahudi&waarabu ndio huku mnazidi kuharibikiwa akili kufikiria mambo ya msingi
 
View attachment 2264752Wayahudi si wabaguzi ni watu pouwa sana.
Utakuwa umewajua juzi wew, em fanya utafute pesa na upate nauli uende huko jerusalem, hakika utakalofanyiwa huko hata ushuhuda humu hutoleta, maana muonacho ktk media ni tofaut na reality, hiyo mijitu mnayoita wayahudi, ni watu wenye roho mbaya, ubaguzi mkubwa, kubwa kulko ushoga kwao ni kipaumbele, jiandae kuolewa
 
EeeeenHeeeee!

Niliposoma kichwa cha habari ya mada yako nikadhani ni utani!

Lakini sasa nimeiona picha. Hii haiwezi kuwa ya 'photoshop'!

Nchi hii tuna waigizaji kwelikweli.

Huyu bwana kavuna bila jasho miaka yake yote ya ubunge na uspika, huku uwezo wa kufanya lolote la maana akiwa hana.
Sasa anafaidi matunda aliyopewa na CCM.
Wewe ulishafanya lipi la maana? Mnapenda kulalama tu kichwani zero!
 
Hicho kinachotokea hapo ni upepo wa baitul maqdis upande wa pili.Kwa sababu kwa mayahudi hakuna baraka yoyote.Na ukitaka majibu ya uhakika ni lazima uende alkaaba iliyopo Makkah.Kuna ndugu yangu alikata tamaa kupata watoto.Alipokwenda Makkah na kumshtakia Mungu sasa ana watoto wa,mejaa nyumba.
Imani yako inakutuma hivyo, lakini Mwenyeenzi Mungu mwingi wa rehema na kweli, aliye umba dunia yote, hapatikani Yerusalemu na Makka tu! Yupo kila mahali, ameijaza dunia yote! Anawapa watu wote wamwombao na kumwamini popote thawabu! Siyo ndugu yako tu, mimi nimemwomba nikiwa hapa Rau Madukani na amenijazia watoto nyumba tele! Sasa hivi namlilia ada tu!
 
Hata akitubu vipi. Dhuluma alizo mfanyia Lissu na Watanzania kwa ujumla kwa kuiba kura na covids hakuna jinsi Mungu ata punguza hasira juu yake.
Arudi kwanza kwa Watanzania kuomba msamaha ndipo aka tubu kwa Mungu
Hata maandiko yana sema kapatane kwanza na ndugu yako.
Yule ni mzee ni shetani sn
 
Wewe ulishafanya lipi la maana? Mnapenda kulalama tu kichwani zero!
Huyo mtu wako, Ndugai, au kama ni wewe mwenyewe, hana kitu kichwani, hili liko wazi.

Sasa ukiniuliza mimi nilishafanya nini; anza na kuelewa kwamba nina uwezo wa kutambua ubovu mkubwa alionao Ndugai, hiyo ni hatua moja zaidi yake.
 
Nahisi watu hutenda maovu kwa sababu wanajua watasamehewa, ingetakiwa kusiwe na msamaha kwenye makosa ya makusudi, ingepunguza watu kutenda makosa, mtu anapofanya makosa afu anaenda kutubu ni kama kejeli kwa mtoa msamaha
Katika Doctrine za Kikristo iko hivyo, ambayo ni tofauti na Islamic Doctrine
In Islam ukifanya dhambi kama ya kutosali au kutofunga hapo UNAWEZA kuomba msamaha/toba Allah akakusamehe kwa sababu hiyo dhambi ni kati yake na wewe
Ila dhambi yoyote ambayo inahusisha haki ya mtu mwingine hiyo lazima umuombe msamaha Mungu mwenyewe pamoja na mtu ambaye haki yake inahusika ktk dhambi hiyo
Kama umedanganya au umeiba ili usamehewe pamoja na kumuomba Mungu msamaha, lakini haukamiliki mpaka umuombe msamaha yule uliyemuibia/uliyemdanganya

Katika Doctrine ya Kikristo mtu kama Hitler anaweza akamalizana na Mungu bila kujali Wahanga aliyowalostisha
 
Kaenda kushuhudia Yesu na mkewe mariamu walipozaliwa 🙂🙂🙂

Jamaa alijisahau sana, haya ma vyeo ya Duniani huwa hayana maana katika ulimwengu wa kiroho - kakosa amani ya roho kaamua kwenda kutubu --- haisaidii; Toba ya kweli anza kutuomba sisi watanzania kwanza, ya pili muombe Lissu.


 
Back
Top Bottom