Pre GE2025 John Heche: Nitamuunga Mkono Tundu Lissu, na nitagombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni jambo jema. Lakini kama atashinda Mbowe na yeye akashinda itakuwa ngumu sana kwa CDM. Angegombea kama mgombea huru, sio mgombea mwenza.

Sasa tusubiri tamko la Lema kumuunga mkono Lissu. Sidhani kama Msigwa atatia neno.

Amandla...
Vipi kama akishinda Lissu na Wenje, Hilo hujaliona?
 
Heche anapoteza muda. Mbowe ni chaguo la wapiga kura wa CHADEMA hakuna namna anaweza kushindwa na Lissu ambaye ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunamuunga mkono Mbowe.
Umeandika kimasikhara ila ndo ukweli wenyewe huo. Mbowe ni tembo mtini, kuna watu wamemuweka pale na hawako tayari kuona mtu wao anatoka!
 
Mimi Mbowe kwangu ni Baba wa Kisiasa, amenilea na hamheshimu sana.📌🔨
 
Kamanda, hata kama wewe uko ndani! Lakini sisi tulioko huku nje, tunaona moshi unaofuka kutoka huko ndani uliko.
Tumesema mara nyingi kwamba Chama chochote kilicho hai ni lazima kiwe na michuano kipindi cha Uchaguzi, huo ndio uhai wa Chama

Hivi wamekuambia kama mimi pia ni Mgombea?
 
Yaani kuigawa Chadema?.....
Ndio. Na Lissu hana resources na resilience za Mbowe. CDM itakayoingia katika uchaguzi Mkuu itakuwa imedhoofika. Hata kama Lissu na Mbowe watakubali yaishe. Kwa hali ilivyo CCM atashinda kirahisi.

Amandla...
 
Kwa mujibu wa UNABII na Mungu kile alichonionyesha ni kuwa kuwa Tundu lisu ataibuka kidedea ila kwa kusogeleana Sana . Sympathy vote ni nyingi Sana kwa Tundu lissu zitaibuka siku ya mwisho . Lissu anachotakiwa ni kulinda Kura zake , hili la hujuma ni kweli kabisa .
 
Ndio. Na Lissu hana resources na resilience za Mbowe. CDM itakayoingia katika uchaguzi Mkuu itakuwa imedhoofika. Hata kama Lissu na Mbowe watakubali yaishe. Kwa hali ilivyo CCM atashinda kirahisi.

Amandla...
Kwa maelezo haya inaonyesha unaamini huu uchaguzi utaigawa Chadema ila tambua lengo la uchaguzi sio hilo ila hilo linaweza kutokea kulingana na uchaguzi utakavyoendeshwa.

Kiufupi hali kama hii inasaidia kukuza demokrasia ndani ya chama hivyo haipaswi kuogopwa.
 
Mimi Mbowe kwangu ni Baba wa Kisiasa, amenilea na hamheshimu sana.📌🔨

kama ni hivyo tundu lisu kamuita (mbowe) fisadi na msaliti wa chama, je, haikuumi kwa mtu unamuheshimu kushushwa na kukejeriwa na tundu lisu ukichukulia kwamba anayeshutumiwa “amekulea kisiasa” ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…