Pre GE2025 John Heche: Nitamuunga Mkono Tundu Lissu, na nitagombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 John Heche: Nitamuunga Mkono Tundu Lissu, na nitagombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Itakuwa ngumu maana kuna upande umeishatangaza wazi kuwa wataona uchaguzi ni wa haki pale tu mgombea wao akishinda. Akishindwa itakuwa kwa sababu tu ya hujma. Na wachochea moto wapo sana.

Amandla...
 
Ukiwa mwanaharakat sana hata problem solving skills zako zinakua low. Trust me ukitaka kuprove chukua mtu yoyote aliekua mwanachama sana alafu mpatie uongoz uone atavyokua anapuyanga
 
Vyama hivi vilisajiliwa kwa ajili ya kupumbaza wananchi sasa wananchi wanakata kutumia hivi vyama kuondoa kujiletea mabadiliko kimbembe
 
Heche anapoteza muda. Mbowe ni chaguo la wapiga kura wa CHADEMA hakuna namna anaweza kushindwa na Lissu ambaye ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunamuunga mkono Mbowe.
CHAMA TAWALA
 
Tumesema mara nyingi kwamba Chama chochote kilicho hai ni lazima kiwe na michuano kipindi cha Uchaguzi, huo ndio uhai wa Chama

Hivi wamekuambia kama mimi pia ni Mgombea?
Unagombea cheo gani? Natamani kujua. Uwiii
 
Natamani
1. Lissu - Mwenyekiti
2.Heche - M/mwenyekiti
3. Lema - Katibu mkuu
Chama tawala kitakua busy sanaaaaa. Yan ccm kitaondoa zile taka taka zoote zilizojaa pale lumumba na uvccm iweke watu wenye akil sasa. Maana kwasasa chadema imejifia ndio maana ccm wala hawa panic
 
Kama anakopata hela Mbowe ni siri au hakufahamiki hiyo ni hatari kuliko kutokuwa na pesa.
Hata Marekani sio donors wote wanawekwa hadharani. Wanaweza kujua wachache lakini sio wote. Na wakiacha kuchangia hamna atayewalazimisha. Hasa ukizingatia kuwa humo humo CDM kuna watu wanapeleka taarifa upande wa pili. Taarifa zinazoweza kutumiwa na TRA n.k. kuwashughulikia.

CDM bila pesa kitakuwa kama Chaumma. Si umeona pamoja na kusema sana kuwa wanamuona Lissu kama mkombozi wao, michango ya kumnunulia gari inavyosua sua. Sasa wakiambiwa zinahitajika milioni 100 kila mwezi za kuendesha chama wataweza?

Amandla...
 
Wakuu mmesikia huko? John Heche rasmi ametangaza kumuunga mkono Tundu Lissu na atagombea Umakamu Mwenyekiti wa Chama.

Heche ameongeza "Mimi Mbowe kwangu ni Baba wa Kisiasa, amenilea na hamheshimu sana. Tunakwenda kwenye uchaguzi na tutakushinda katika uchaguzi huu. Mimi namuunga mkono Tundu Lissu na nimeamua kuchukua Fomu ili nikamsaidie Mwenyekiti kujenga Chama chetu. CHADEMA ni tegemeo la wananchi. Kwa rafiki yangu Wenje, tumefika hapa kwa sababu yako."
View attachment 3193009
Hapa at least CHADEMA kitakuwa na sura ya Kitaifa endapo hawa miamba wawili watashinda; Tundu Lissu na John Heche.
Vinginevyo, CHADEMA kitaendelea kuonekana chama cha Kichagga.
 
Wakuu mmesikia huko? John Heche rasmi ametangaza kumuunga mkono Tundu Lissu na atagombea Umakamu Mwenyekiti wa Chama.

Heche ameongeza "Mimi Mbowe kwangu ni Baba wa Kisiasa, amenilea na hamheshimu sana. Tunakwenda kwenye uchaguzi na tutakushinda katika uchaguzi huu. Mimi namuunga mkono Tundu Lissu na nimeamua kuchukua Fomu ili nikamsaidie Mwenyekiti kujenga Chama chetu. CHADEMA ni tegemeo la wananchi. Kwa rafiki yangu Wenje, tumefika hapa kwa sababu yako."
View attachment 3193009
Kwa team hii ya lissu+heche ikishinda, Lumumba hakutakalika kamwee
 
Chadema wamepata fursa nyingine ya kukirudisha chama kwa Wananchi baada ya wapiga kura kupoteza imani.
Lissu na Heche wanaweza kukinusuru chama ila sidhani kama Sultan Mbowe atakubali kunyang'anywa kitegauchumi chake...ngoja tuone.
..Chadema ikiwapa nguvu heche na lissu, itakuwa imeongeza nguvu na ushawishi mwingi Sana kwa umma
 
Hata Marekani sio donors wote wanawekwa hadharani. Wanaweza kujua wachache lakini sio wote. Na wakiacha kuchangia hamna atayewalazimisha. Hasa ukizingatia kuwa humo humo CDM kuna watu wanapeleka taarifa upande wa pili. Taarifa zinazoweza kutumiwa na TRA n.k. kuwashughulikia.

CDM bila pesa kitakuwa kama Chaumma. Si umeona pamoja na kusema sana kuwa wanamuona Lissu kama mkombozi wao, michango ya kumnunulia gari inavyosua sua. Sasa wakiambiwa zinahitajika milioni 100 kila mwezi za kuendesha chama wataweza?

Amandla...
US wanasheria kali za pesa kwa vyama na uchaguzi. Ni moja ya kesi inayomkabili Trump. Pesa za siri ni hatari kwa nchi maana zinaweza kutoka kwa maadui wa nchi au wananchi wenye malengo mabaya na nchi. Kufanya mapambano hakukupi uhalali wa kuvunja sheria. Ukifanya hivyo utaendelea hivyo hivyo hata ukiingia madarakani. Kama chama kinachangiwa na matajiri na si wananchi basi ni chama cha matajiri wachache na kikiingia madarakani kitasimamia maslahi ya hao matajiri.
 
Itakuwa ngumu maana kuna upande umeishatangaza wazi kuwa wataona uchaguzi ni wa haki pale tu mgombea wao akishinda. Akishindwa itakuwa kwa sababu tu ya hujma. Na wachochea moto wapo sana.

Amandla...
..Uchaguzi huu unafuatilia na watu wengi sana, chadema waionyeshe Dunia kivitendo wanachokisimamia...uchaguzi huru, wa haki
 
Chama Dola kimeshashinda mapema mno
huyo tundulisu labda atawavusha 2030
 
Kila la heri kwake
Kumbe upo upande huu wa Lissu. Mimi huwa namwita ni muujiza unaotembea. Risasi zaidi 30 na bado aliokoka. Mpeni uongozi japo kwa miaka 5. Tunaowaunga mkono- ambao sio wanachama wa chama chochote cha siasa tupo wengi mtaani. Tunapenda kuona nchi yetu inakuwa na upinzani imara, ili kuifanya CCM isijisahau. Utafika mwaka mtakapokuwa na nguvu zaidi mtashika usukani wa nchi moja kwa moja.
 
Hujui dunia ,Wenje anatakiwa kufukuzwa uanachama mara moja alitaka kujeruhi chama ila kimemramba , na ataishi maisha yasiyokua na amani ,chama ambacho watu wamepoteza mpaka ndugu zao leo mjinga mmoja anakiumiza , Fukuzia mbali

Back
Top Bottom