Pre GE2025 John Heche: Nitamuunga Mkono Tundu Lissu, na nitagombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 John Heche: Nitamuunga Mkono Tundu Lissu, na nitagombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Natamani
1. Lissu - Mwenyekiti
2.Heche - M/mwenyekiti
3. Lema - Katibu mkuu
Hii combinenga ni noma, mboga moto ugali motoo!!.
Na ndio dawa ya ma ccm hiyo...sio mambo za busara sijui maridhiano halafu uchaguzi serikali za mitaa wanaleta uhuni!!.
 
US wanasheria kali za pesa kwa vyama na uchaguzi. Ni moja ya kesi inayomkabili Trump.
Sio kweli. Mahakama Kuu ya Marekani ililegeza sana masharti ya michango katika chaguzi. Uamuzi wa kesi ya Citizens United ilifungua milango kwa uanzishwaji wa PAC ambazo hazina limits katika uchangishaji na haziwajibiki kusema nani anazichangia. Wanasiasa na vyama vyote vina PAC.
Pesa za siri ni hatari kwa nchi maana zinaweza kutoka kwa maadui wa nchi au wananchi wenye malengo mabaya na nchi.
Shida ni nani ana define adui wa nchi. Kwa hali ilivyo sasa kuna wengine wanaweza kusema kuwa mpinzani wa CCM ni adui wa nchi. Unaposema kuwa mtu mwenye malengo mabaya na nchi atachangia kwa siri chama cha siasa itakuwa una maanisha kuwa kuna vyama vya siasa vina malengo mabaya na nchi.
Kufanya mapambano hakukupi uhalali wa kuvunja sheria. Ukifanya hivyo utaendelea hivyo hivyo hata ukiingia madarakani. Kama chama kinachangiwa na matajiri na si wananchi basi ni chama cha matajiri wachache na kikiingia madarakani kitasimamia maslahi ya hao matajiri.
Rostam Aziz, Mohammed Dewji wanaochangia CCM ni maskini? Matajiri hawafanani.

Amandla...
 
Watu wa kusini watawakilishwa na Lissu na Heche? Pengine na Lema? Ukiweka mbele ubaguzi hautakosa sababu. Hao watawakilisha vipi waislamu? Au wanawake?
Ni mchezo mbaya mnaocheza.

Amandla...
Hapa at least CHADEMA kitakuwa na sura ya Kitaifa endapo hawa miamba wawili watashinda; Tundu Lissu na John Heche.
Vinginevyo, CHADEMA kitaendelea kuonekana chama cha Kichagga.
 
Maccm mwanzo yalikua hayamtaki Mbowe eti ghafla amekua Rafiki yao.

Sasa ccm kaeni mkao sawa mnaletewa vyuma ,pale lissu, pale Heche, pale Lema .

Maoni yangu Milembe ipanuliwe haraka , sio mda tutakua na vichaa wengi sana kutoka Mbogamboga
 
kama ni hivyo tundu lisu kamuita (mbowe) fisadi na msaliti wa chama, je, haikuumi kwa mtu unamuheshimu kushushwa na kukejeriwa na tundu lisu ukichukulia kwamba anayeshutumiwa “amekulea kisiasa” ?
Heche anaangalia na kuzingatia zaidi maslahi ya chama.

Pia, siyo kwamba wanaompinga Mbowe kwa sasa wanamchukia au hawamheshimu, hapana, bali wanaona muda wa yeye kuongoza kwa ufanisi umepita
 
Heche anapoteza muda. Mbowe ni chaguo la wapiga kura wa CHADEMA hakuna namna anaweza kushindwa na Lissu ambaye ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunamuunga mkono Mbowe.
Ohoo! Hii ni ajabu kweli. Ngoma inapigwa Ufipa Street, halafu wanaoserebuka wako Lumumba Street!
 
Natamani
1. Lissu - Mwenyekiti
2.Heche - M/mwenyekiti
3. Lema - Katibu mkuu
 
Kwa akili zangu naona CCM wakilia na kusaga meno mara tu. Baada ya Lissu kushinda uenyekiti. Mbowe tayari wanammudu
Hapo ndipo mnapokosea. Chama chini ya Mbowe kili survive hata pale walipokuwa wana mbunge mmoja ( heshima zako Kenan) bungeni. Hata pale viongozi wao ( pamoja na Mwenyekiti)walipokuwa wanatiwa ndani kama kawa. Kili weza kukataa kupokea ruzuku kwa zaidi ya miaka miwili bila kutetereka. Ndio maana CCM inafanya kila namna Mbowe ashindwe maana wanajua kuwa ana uwezo wa kuijenga upya ( hao wote mnaowashabikia leo wanakiri walijengwa na Mbowe) CDM kama atashinda uchaguzi.

Unadhani CDM ya Lissu itaweza yote hayo? Kuna hata mmoja wao ana ubavu wa kuongoza maandamano yaliyokatazwa na dola? Mbowe alikuwa tayari na alifanya hivyo. Unadhani watanzania wako tayari kuingia barabarani kuitikia wito wa Lissu hata baada ya Polisi kuwaonya atakayetokeza atapigwa kipigo cha paka mwizi?

Sisi yetu macho.

Amandla...
 
Watu wa kusini watawakilishwa na Lissu na Heche? Pengine na Lema? Ukiweka mbele ubaguzi hautakosa sababu. Hao watawakilisha vipi waislamu? Au wanawake?
Ni mchezo mbaya mnaocheza.

Amandla...
Shida wanamuangalia Mbowe kama vile anawakilisha wachaga..

Wasilolijua ni kwamba wachaga wanafaidi zaidi CCM na wengi wanajinasibisha na CCM kulinda biashara zao..

Wawe wapole muda si mrefu chama kinaitwa cha Kikristo na chenye mfumo dume...

Washabiki ni watu hatari sana
 
Hapa at least CHADEMA kitakuwa na sura ya Kitaifa endapo hawa miamba wawili watashinda; Tundu Lissu na John Heche.
Vinginevyo, CHADEMA kitaendelea kuonekana chama cha Kichagga.

Na Balance ya Udini na Jinsia hapo vipi?

Mbowe hawakilish wachaga, wachaga wanafurahia zaid CCM kulinda biashara zao, kuanzia Siha mpaka Hedaru, wabunge ni CCM hadi mawaziri..

Hizi bla bla zimepitwa na wakati
 
Heche anapoteza muda. Mbowe ni chaguo la wapiga kura wa CHADEMA hakuna namna anaweza kushindwa na Lissu ambaye ni adui wa demokrasia na kirusi ndani ya chama rafiki CHADEMA. Sisi wanaCCM tunamuunga mkono Mbowe.
Wana CCM wakisikia jina la Lisu chupi zinaanza kuwapwaya ghafla
 
Back
Top Bottom