Mchuano na mabidilishano ya maneno yameibuka mitandaoni hasa akaunti ya Kigogo na Halima kuhusu wabunge wa viti maalum
Kigogo anadai Halima ni moja ya watu wanaosimamia wabunge wa viti maalum wapeleke majina NEC kwa ajili ya kupitishwa huku Halima akikataa tuhuma hizo na kumtaka Kigogo aende kwa waliomtuma.
Kuhusu msimamo wa CHADEMA uliotolewa na John Mnyika ni kwamba hakuna mbunge wa viti maalum aliyepitishwa na chama na kupelekwa NEC ila wanadai NEC wanaandaa majina yao kwa shinikizo kutoka CCM.
Mjadala wa wabunge wa viti maaalum umechukua sura mpya na kuonekana wa muhimu hasa na wanachama wa chama Tawala.
Akaunti nyingi za wanaccm katika mitandao ya kijamii zinawashauri CHADEMA kuteua wabunge wa viti maaalum jambo linalotafsiriwa na wanachadema Kama mtego wa kupata wajumbe wa kamati mbili muhimu bungeni zinazopaswa kuongozwa na upinzani.
Baadhi ya wachambuzi wanaamini CHADEMA kuteua viti maalumu ni kuwasaliti wananchi kwani Uchaguzi uliopita ulionekana kuwa si huru wa haki.
Wanaoamini katika imani tofauti nao wanaona kuwa kuendelea kuruhusu wabunge wa upinzani waingie bungeni ni kuwasaliti waliopo mahabusu, magereza, mahospitalini na uhamishoni na waliopoteza maisha bila hatia.
Upo umuhimu wa viongozi wetu kuchagua utu na kuachana na tamaa za madaraka na fedha, wanawake wameteseka katika harakati za siasa na si sahihi wakajitokeza kusaliti maumivu yao waliopata kutoka kwa hao wanaowaona leo ni wamuhimu. Hawatakufa njaa wavumilie.