Jua Kali latawala Tanzania: Hali ya Hewa kila Mkoa na Uzoefu wako ni upi?

Kanda ya Kati hali ya hewa inakuwa nzuri kuanzia saa 5 usiku mpaka saa 1 asubuhi. Jua kali linawaka saa 2 asubuhi mpaka 11 jioni.

Kanda ya Kati inajulikana kwa hali ya ukame na jua kali ila mwaka huu vimeambatana na joto kali. ☀️🥵
 
Joto kali huu ni mwaka wa njaa. Mahindi yamekauka shambani. Unga kilo 1 ni 1400-1500. Kwa hali ilivyo unga utafika 2000 kwa kilo hadi 3000 kwa kilo.



Huu ni mwaka wa njaa. Laana ya kutesa na kuteka watu inaitafuna nchi, watu wanafanya uchawa mpaka kwenye nyumba za ibada. Mnasababisha nchi ikose chakula
Mabilioni yanayoenda kwenye uchawa yangeenda kwenye umwagiliaji
 
Napitia Iringa sasa hivi mvua inanyesha/inatonya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…