Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 1,367
- 2,451
- Thread starter
- #81
Fuh
Takwimu za hivi majuzi zinaonyesha joto limeongezeka sana kwa viwango vya kutisha, katika sehemu mbalimbali duniani.
Here are some of the hottest recorded temperatures in 2024:
Ouargla, Algeria – 51.3°C
Basra, Iraq – 52.6°C
Ahvaz, Iran – 53.0°C
Kuwait City, Kuwait – 52.1°C
Jacobabad, Pakistan – 51.2°C
Delhi, India – 49.9°C
Phoenix, USA – 48.3°C
Seville, Spain – 47.6°C
Viwango hivyo vya joto lililopitiliza havijawahi kushuhudiwa tangu wanasayansi waanze kutunza record za viwango vya joto.
Wanasayansi wanasema ongezeko hili la joto linatokana na mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za binadamu, kama vile uzalishaji wa gesi joto kutoka viwandani na ukataji miti.
Biblia, iliishatabiri juu ya kuongezeka kwa joto. Katika Ufunuo wa Yohana 16:8-9 tunasoma juu ya mabakuli ya ghadhabu ya Mungu yatakayomwagwa juu ya jua...
"Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lake juu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watu kwa moto wake. Basi, watu wakaunguzwa vibaya sana; wakamtukana Mungu aliye na uwezo juu ya mabaa hayo. Lakini hawakutubu na kumtukuza Mungu."
Ni ajabu sana. Watu wanaunguzwa, badala ya kutubu dhambi ndio wanakazana kumtukana Mungu na kusema eti hayupo.
Joto hili kali si jambo la kawaida—wanasayansi wamethibitisha kuwa limeongezeka kwa kasi, na Biblia ilishatabiri nyakati hizi. Huu ni wakati mwafaka wa kutubu maovu na kumrudia Mungu, na kujiandaa kwa ujio wa Yesu Kristo(Ufunuo 22:12).
Chonde, chonde, kama hujaokoka, usisubiri hadi iwe too lateDuh