Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Mwalimu alikuwa Nabii. Tunakukumbuka! RIP Baba Yetu
 
Katika hili alikosea sana, na hili lilitokana na kuwa na hofu ya mabadiliko ambayo wajamaa wengi wanayo.
Lakini mimi binafsi naamini kabisa huyu mzee alikuwa na nia njema sana na Tanzania yetu. Maana katika watu ambao wangeamua kutuuza wangefanikiwa basi huyu mzee angefanikiwa sana.
Alipoingiza multi part system alitakiwa asimamie mwenyewe mabadiliko makubwa ya katiba, maana huyu ndo alikuwa kiboko ya CCM....
 
Nyerere alikuwa ni kichwa cha kipekee. Hapa anawazunguzia wanasiasa na wakati ule ule wale wanajeshi ambao walitaka kumpindua mwaka 1964.
 
Hivi kipindi hicho kuna baadhi ya wana Siasa walikuwa wana hama vyama? Hakikuwa ni kipindi cha mfumo wa chama kimoja kweli? Au ulikuwa ni utabiri?
 
Nyerere akikuchukia anakutukana wazi wazi.
Kweli kabisa.... "unashauriwa na mke wako huko halafu unatuletea hapa.... hii hatuwezi kukubali kabisa "...... Aliwahi sikika akimpiga dongo rais mmoja at one time
 
Achana na hiyoo sasa, kuna kitabu alikiandika kabla ya kufa unaambiwa lilikuwa ni bomu moja baya sana.
Yule Mmakonde aliagiza kipigwe moto chote na wala kisitoke nje. Tena kuna baadhi ya maneno yake aliyoyasema miaka ya 1990's nilyasoma kwa mtu niliogopa na kusema kama watanzania watayasikia haya kuhusu Serikali basi wataumia sana na mtu kama Raisi Mkapa hawawezi kumpenda kamwe.
Mkuu hebu funguka....
 
Nimeisikiliza ile hotuba nikakiri jamaa alikuwa GREAT THINKER, mambo alihutubia miaka kibao iliyopita ila MALAYA wa kununulika ndo wanatokea sasa hivi! Pumbavua zao hao malaya malaya! Wakipewa chapaa tayari pichu magotini!!!
 
Kuna watu walihakikisha hafiki huko, wengine laana zishaanza kuwasumbua.
Huwa nikiwaza haya mambo napata sana kisirini na baadhi ya watu hapa nchini.
Tena nachafukwa zaidi roho pale unakuta linakuja lijinga hapa mtandaoni limelipwa vijihela kidogo huko linaanza kupiga ramli kuwasifia hawa wasaliti na familia zao hadi unajiuliza watanzania ni wajinga hivi ?
 
Mara nyingi lisemwalo lipo na kama halipo laja
 
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongea ukweli mtupu. Japo wahusika itawauma lakini ni vema wangejitakasa uovu huu. Ni aibu mtu uliyeaminiwa na wananchi kuwa malaya wa kisiasa. Aibu yao
 
Back
Top Bottom