Jumba la kifahari la Mwenyekiti Mbowe lazua maswali ndani ya CHADEMA
Kama makonda ana majumba ya kifahari na familia yake ilikuwa masikini, tunajua maisha ya makonda aliisha kwakumlamba visigino Riz1. Leo tunashangaa mtoto wa Aikael ambaye baba yake alifadhili harakati za Nyerere?.
 
Jumba la kifahari la Mbowe.
image_search_1699945374368.jpg

Mama yake Alphonce Mawazo kwenye nyumba ya Udongo.
image_search_1699945310064.jpg

image_search_1699945276981.jpg

Lazima tujifunze kitu hapa.
 

Attachments

  • image_search_1699945374368.jpg
    image_search_1699945374368.jpg
    159.4 KB · Views: 1
Hizi picha zina somo kubwa sana

Watu tumeingiza ushabiki na mapenzi binafsi badala ya kujenga hoja
 
Mbowe ameishi kwenye nyumba nzuri kabla ya wazazi wako kukutana.(kabla ya CDM kuanzishwa)
Sasa unataka Mbowe asiwe na nyumba nzuri kwa kuwa mama yake Mawazo ana nyumba mbovu?

Tujiulize nani alimuua Alphonce Mawazo?
Aliyemuua Mawazo ndio kamsababishia maisha magumu mama yake Mawazo.
Maana Mawazo alikuwa anapambania familia yake na naamini hadi leo huyo mama angekuwa anaishi nyumba nzuri sana endapo Mawazo angekuwa hai.

Mleta mada tumia hata akili za mumeo kama zako zimeisha muda wake.(expired)
 
Jumba la kifahari la Mbowe.
View attachment 2813278
Mama yake Alphonce Mawazo kwenye nyumba ya Udongo.
View attachment 2813276
View attachment 2813281
Lazima tujifunze kitu hapa.
Baba yake Mbowe kamhifadhi mwasisi wa chama chenu. Kamlisha na kumuonyesha bafu la kuoga liko wapi, huku akiwa amejifunga taulo kiunoni na huyo mwasisi wa chama chenu akiwa amekunja mikono kwa heshima. Na nauli alikuwa anamuomba anapewa na anatoa shukrani za kutosha.

Tena Mbowe alikuwa hajazaliwa ila angekuwa amezaliwa kipindi kile mwasisi wa chama chako anaenda kwao, yawezekana Mbowe angemfinya na kumwambia toka kwetu na asifanywe chochote.
 
Ameandika Dr. Sisimizi

Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika ndani ya CHADEMA kufuatia baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kuona nyumba ya kifahari anayoishi Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambayo ameijenga hivi karibuni huko Machame.

View attachment 2812700

Sintofahamu hiyo imekuja baada ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu kupokea taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe weekend hii aliwaita baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu (Heche, Lema na Msigwa) kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa nyumba hiyo mpya ya Mbowe ambayo ameijenga kwa miezi 3 tu.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu wamehoji Mwenyekiti Mbowe amepata wapi hela za kujenga nyumba ya kisasa ya ghorofa kwa miezi 3 tu, tena wakati ambao shughuli za chama zimekwama kuendelea kwa kisingizio kuwa ruzuku imeisha mpaka watakapoingiziwa tena Disemba 2023.

Hoja yao inaonekana ina mashiku kwa sababu, ndani ya CHADEMA wenye mamlaka ya kuidhinisha pesa kutolewa (Signatories) ni watatu tu Mwenyekiti Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salim Mwalimu na Mjumbe wa Baraza la Udhamini Mzee Mtei.

Hii inaonesha bado hakuna kuaminiana baina ya Mwenyekiti Mbowe na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ukiwatoa wale wanaokula nao sahani moja (Lema, Msigwa, Heche, na Salim Mwalimu) na wengi wanachojiuliza inawezekanaje Chama kikose hela ya mafuta ya Chopa halafu Mwenyekiti anazindua nyumba yenye thamani ya Milioni 500.

Ndugu zangu tuendelea kufuatilia kwa karibu, ndani ya CHADEMA kuna Bundi anazengea na muda si mrefu tutaanza kusikia vilio vya kuomboleza kwa sababu najua Tundu Lissu hawezi kukaa na kuyafumbia macho yanayoendelea mule ndani.
Nani kaleta haya makopo jamani!
 
Kuna watu wenye mawazo na fikra za hovyo kabisa!
Hivi hii nyumba ina maajabu gani? Mlizunguka kuona nyingine kule migombana?
Mngezunguka kuona nyingine msingeleta huu upuuzi kuona hii nyumba ni maajabu migombani!
 
Hizi ndizo huitwa siasa za maji machafu. Halafu kuna watu wazima wanazisherehekea kabisa. Ukiwa mwana CCM lazima ujitoe ufahamu?
 
Jumba la kifahari la Mbowe.
View attachment 2813278
Mama yake Alphonce Mawazo kwenye nyumba ya Udongo.
View attachment 2813276
View attachment 2813281
Lazima tujifunze kitu hapa.
Labda mleta mada atusaidie nia hasa ya kulinganisha nyumba ya Mbowe na makazi ya mamake A. Mawazo.
Mbowe kazaliwa familia tajiri, Mawazo kazaliwa familia kawaida kama watanzania wengi. Sii kazi ya Mbowe kuwanyanyua masikini wa taifa hili, sababu Hana dhamana yoyote katika muktadha huo. Ni wajibu wa serikali inayokusanya kodi kuweka mipango na sera zitakazowawezesha wananchi kuinua hali zao za maisha. Sijui kwanini uone Mbowe anaishi maisha ya kifahari, ushindwe kuona maisha wanayoishi wale waliofasadi nchi hii- kina Samia, kikwete, mwingulu, familia za kina magufuli, mkapa etc.
 
Back
Top Bottom