JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Chezeeni vingine, msichezee watu wanaojitolea maisha yao kutulinda.
Hawajitolei maisha yao kutulinda, wanalipwa ili kutulinda. Hii ni kazi waliyoamua wao kuomba ili waajiriwe kuifanya. Hivyo wanatekeleza majukumu yao.

Ni sawa na mwalimu anavyolipwa ili afundishe watoto wa mwanajeshi. Au daktari anavyolipwa ili aokoe maisha ya watu. Kama daktari hajalipwa, hawezi kuokoa maisha mtu.

Hata wanajeshi bila kulipwa, hawawezi kulinda usalama wa nchi. Acha watekeleze wajibu wao kwa mujibu wa katiba.
 
nimeamini siku moja tu inatosha kuprove ujuha wa professor
aliye jifanya mwerevu kwa miaka 100!
wewe ajuza kwa umri wako na heshima yako nusu kenda
uliyojitwalia kwa miongo mingi,unaipoteza kizembe
kwenye utawala wa Mama Abdul!

so sad!
😒😒
 
W

Wamenusa harufu ya mapigano yatakayochochewa na mapinduzi wameanza kujihami, ipo siku tu CCM na viongozi wenu mtalia na kusaga meno kwenye hii nchi.
 
Tatizo mnaongea sana tena Kwa matusi na kejeli.
Kiufupi tu
JF ni ndogo sana.
 
Nawashauri muwache kuongea kijinga, wakimtaka mtu hapa JF wana uwezo wa kumpata ndani ya muda mchache sana
Law enforcement ni jukumu la polisi sio jeshi. Labda kwa watumishi wa jeshi tu ndio wana vitengo vyao vya sheria na mahakama za jeshi.

Kwa wananchi, kama mtu kavunja sheria (mathalani kumiliki mavazi ya vyombo vya ulinzi na usalama), basi akamatwe na apelekwe mahakani apewe adhabu inayostahili.
 
So sad! Nchi ilipofikia inahitaji msaada mkubwa wa jeshi, lakini jamaa wanajiweka bize na vitu visivyo na msingi kabisa.
 
Hawana la kufanya hawa mbunga zinachukuliwa Wamasai wanafukuzwa wapo kimya. Jeshi taratibu linakwenda kuchukua nafasi ya kudharauliwa. Usishangae Slaa ama Mwambukisi wamekutwa na sare za jeshi. Ule mtaro wa kutoka bahari kuja Jangwani Magomeni kuchafu sana wanatakiwa kusafisha jiji. Ama wakalime mashamba ya Alizeti. Bogus maamuzi ya hili jeshi.
 
Bandari inauzwa wapo kimya wanapokea posho nono nono tu, madini na wanyama wetu kila kukicha vinaporwa, eti mkaanze kusaka nguo za mfanano na zao, nguo zenyewe za elf 5, nendeni Gabon huko mkaombe kazi!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Ujinga mtupu.Kizazi kinabadilika.Hivi kwa miaka ya 70s huko,ungekuta watu wanahojihoji kuhusu hilo suala?Mambo yanabadilika.
 
Wenzao wanapindua serikali huko wao wanasaka sare huku [emoji28]

I don't condone mapinduzi ila hii ni task ya kiboya sana.
Watapindua wapi wanakula michapati pale wanatoka vitambi tu[emoji3][emoji3] nina kishamba changu nimekosa pesa yakunilimia wakanisaidie kung'oa visiki tu.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kuingia mtaani sheria inawaruhusu? Au wanataka kuvunja Sheria ili washtakiwe

Sheria inawezekana haiwa ruhusu. Lakini sheria ipi? Kama ni hii Katiba ya JMT iliyoandikwa na mawazo ya watu 20 tu ambao walikuwa wananjua Nyerere JK na wakijua anataka nini na anayo matamanio gani katika kuliongoza Taifa.

Na katika kuandika kwao wakafikiria Taifa hili siku zote litaongozwa na Watu wanaofanana na Nyerere JK.

Sasa unategemea nini kama ikitokea wajeda wakaingia mtaani kwa maslahi mapana ya nchi ambayo haya onekani kutendewa haki na Katiba ya JMT???
 
Kwahiyo wakishampata?? Tulieni wanajeshi sio Mungu.!!!
 
That’s police work. Hilo, kama jinai zote zinazofanywa na raia, ni jukumu la kipolisi. JWTZ, ikibidi, wanatakiwa kuwasiliana na jeshi la polisi kuhusu mikakati ya kufanikisha kazi hiyo kwa ufanisi zaidi. Sio kuingia mitaani. Hiyo siyo state of emergency na Rais hajatangaza.

Ni nchi modeli ya “banana republic” tu ndio utaona jeshi linafanya kazi ya polisi. Nchi makini huwezi kuona wanajeshi waliovaa combat fatigues wanazagaa mitaani, kuzoeana, kupambana au kutishiana na raia. Ni aibu kwa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…