JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Mnaoandika hovyo msifikiri JF haina limit ya kuwalinda.

Nawashauri muwache kuongea kijinga, wakimtaka mtu hapa JF wana uwezo wa kumpata ndani ya muda mchache sana.

Eleweni kuwa hii mitandao hakuna pakujificha na hakuna kinachofutika hata wewe ukifuta.

Chezeeni vingine, msichezee watu wanaojitolea maisha yao kutulinda.
Anakulinda wewe na mama ako [emoji57]
 
wanajeshi wenzao wa korea kaskazini wako bize mitandaoni wanaiba dollars wao wanahangaika na madela yenye rangi madoa madoa, kwanini nao wasiwe kazini kuhakisha dollars zinapatikana benki kuu, ila sera za maccm zimefanya wajeda kuchanganyikiwa badala ya kudesign silaha na kuwauzia russia wao wako bize na midosho facken kabisa.
 
Asiesikia la mkuu huvunjika guu, hakuna marefu yasio na ncha, safari 1 huanzisha nyingine, za mwizi 40, Simba mwenda Pole ndio hula..., Za kuambiwa changanya na Zako,msije mkasema hakukumbushwa
Kula chuma hiko
---

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema siku saba zilizotolewa kusalimisha mavazi yanayofanania na sare za jeshi kwa hiari zimeisha, hivyo jeshi litaingia kuzisaka nguo hizo kwa wananchi.

Kaimu mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema jeshi halina utani katika suala hilo, kwani katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 na kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa.

“Muda wao wa kusalimisha kwa hiari umeisha, kama mtu atakuwa hajasalimisha basi tutazifuata wenyewe, na mtindo upi tutatumia kuzichukua kwa wananchi tunajua wenyewe,” amesema Kamanda Ilonda.

Ameongeza kuwa sheria inakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ au zinazofanana na sare hizo bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.
Kama wamekosa kazi za kufanya, kwanini wasijitolee kwenda kufanya kazi kwenye ujenzi wa bwawa la umeme la nyerere kule au kwenye mradi wa SGR ili hiyo miradi ikamilike kwa wakati? wachukue hata magreda ya jeshi wakachonge barabara za vijijini, wakulima wapate njia za kufikisha mazao masokoni, tunyanyue uchumi wa taifa.

Kuna kazi nyingi sana za kujitolea, lakini wao hawazioni, wako bize kuhangaika na mavazi. Aibu kubwa sana kwa taifa.
 
Mbibi kwa mkwara tu. Too old to threaten us. At your advanced age you should be busy arranging your burial arrangements and clarifying your will.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Somalia ni pamoto kule.Mtu akienda,kurudi ni majaaliwa.Sasa BATTLE kama hizo,hazitiliwi maanani,badala yake anakunjwa na kupigwa mitama,mtanzania ambaye hajajifunza hata matumizi ya silaha wala ngumi.Na huyo mtanzania,akipigwa,aliyempiga anaonekana MWAMBA,wakati aliyepigwa hana mafunzo yoyote.Somalia kule baadhi wana mafunzo,ndo inatakiwa mtu aonyeshe UMWAMBA kwa wale wasomali.
Wa Tz munaogopa mitama🤣
 
wanajeshi wenzao wa korea kaskazini wako bize mitandaoni wanaiba dollars wao wanahangaika na madela yenye rangi madoa madoa, kwanini nao wasiwe kazini kuhakisha dollars zinapatikana benki kuu, ila sera za maccm zimefanya wajeda kuchanganyikiwa badala ya kudesign silaha na kuwauzia russia wao wako bize na midosho facken kabisa.
Kile kiwanda cha jeshi ya nyumbu sijui kiliishia wapi? [emoji3][emoji3] nakumbuka enzi za mwalim, kiwanda kiliwahi kuzalisha magari pale.
 
Sheria inawezekana haiwa ruhusu. Lakini sheria ipi? Kama ni hii Katiba ya JMT iliyoandikwa na mawazo ya watu 20 tu ambao walikuwa wananjua Nyerere JK na wakijua anataka nini na anayo matamanio gani katika kuliongoza Taifa.

Na katika kuandika kwao wakafikiria Taifa hili siku zote litaongozwa na Watu wanaofanana na Nyerere JK.

Sasa unategemea nini kama ikitokea wajeda wakaingia mtaani kwa maslahi mapana ya nchi ambayo haya onekani kutendewa haki na Katiba ya JMT???
Naunga mkono hoja
 
Kile kiwanda cha jeshi ya nyumbu sijui kiliishia wapi? [emoji3][emoji3] nakumbuka enzi za mwalim, kiwanda kiliwahi kuzalisha magari pale.
Ni nani atanunua Gari linaitwa nyumbu,
I wonder aliyekianzisha alimaanisha nn🤣
 
akili yangu ya darasa la nne B inaniambia ule upepo wa zile coup de tat zilizotokea west afrika umeleta hofu kwa deep state ya ccm.

wameona walitumie jeshi liingie mtaani kupandikiza mbegu ya uoga miongoni mwa watz. hiyo ya uniform ni kisingizio tu.

kingine ni issues ya dp world,nimeona kuna wanaharakati wanazungumzia sana maandamano.
 
Asiesikia la mkuu huvunjika guu, hakuna marefu yasio na ncha, safari 1 huanzisha nyingine, za mwizi 40, Simba mwenda Pole ndio hula..., Za kuambiwa changanya na Zako,msije mkasema hakukumbushwa
Kula chuma hiko
---

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema siku saba zilizotolewa kusalimisha mavazi yanayofanania na sare za jeshi kwa hiari zimeisha, hivyo jeshi litaingia kuzisaka nguo hizo kwa wananchi.

Kaimu mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema jeshi halina utani katika suala hilo, kwani katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 na kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa.

“Muda wao wa kusalimisha kwa hiari umeisha, kama mtu atakuwa hajasalimisha basi tutazifuata wenyewe, na mtindo upi tutatumia kuzichukua kwa wananchi tunajua wenyewe,” amesema Kamanda Ilonda.

Ameongeza kuwa sheria inakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ au zinazofanana na sare hizo bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.
Naziona dalili za mwanzo mwanzo kabisa za Jeshi kuchukua Nchi kutoka mikononi mwa Wanasiasa!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kama ni kweli huyo Kaimu Mkurugenzi kasema haya basi ni dhahiri wa kufukuzwa kazi mara moja !
Kazi ya jeshi si kusachi na kukamata raia hiyo ni kazi ya polisi ndio wanaopewa mamlaka hayo na katiba ya nchi hii.
Huyu aondolewe kazini mara moja.Nadhani sasa anavuka mipaka
Ni mjinga sana na analitia aibu jeshi letu
 
Week iliyopitwa jeshi walitoa mkwara wanamtafuta aliyewasingizia kuwa wameongezewa mshahara , ivi walimpata?
 
akili yangu ya darasa la nne B inaniambia ule upepo wa zile coup de tat zilizotokea west afrika umeleta hofu kwa deep state ya ccm.

wameona walitumie jeshi liingie mtaani kupandikiza mbegu ya uoga miongoni mwa watz. hiyo ya uniform ni kisingizio tu.

kingine ni issues ya dp world,nimeona kuna wanaharakati wanazungumzia sana maandamano.
Coup de tat Ina fanywa na wanachi? Kwani

Iyo ni jeshi tena low ranked offer ndiyo wanafanya maana mkuu wa majeshi Hana njaa hawezi fanya
 
Back
Top Bottom