Asiesikia la mkuu huvunjika guu, hakuna marefu yasio na ncha, safari 1 huanzisha nyingine, za mwizi 40, Simba mwenda Pole ndio hula..., Za kuambiwa changanya na Zako,msije mkasema hakukumbushwa
Kula chuma hiko
---
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema siku saba zilizotolewa kusalimisha mavazi yanayofanania na sare za jeshi kwa hiari zimeisha, hivyo jeshi litaingia kuzisaka nguo hizo kwa wananchi.
Kaimu mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema jeshi halina utani katika suala hilo, kwani katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 na kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa.
“Muda wao wa kusalimisha kwa hiari umeisha, kama mtu atakuwa hajasalimisha basi tutazifuata wenyewe, na mtindo upi tutatumia kuzichukua kwa wananchi tunajua wenyewe,” amesema Kamanda Ilonda.
Ameongeza kuwa sheria inakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ au zinazofanana na sare hizo bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.
Nchi inawajinga wengi sana, yani hawa jwtz wamekosa jambo LA maana LA kufanya, wanaona kusaka nguo zinazofanana na za jeshi ni jambo LA maana sana!
Yaani mtu ni luteni, kwa elimu yote aliyonayo, mchango wake anaoutoa kwa nchi ni kusaka raia wanaovaa nguo kama za jeshi!? Akili za matope kabisa,
Badala ya kuwaza jinsi ya kutatua changamoto kwenye nchi, mfano wakiweka mkakati wa kutumia vijana wa jkt, wafungwa, tekunolojia kuzalisha sukari na ngano ya kutosha, tusiagize tena kutoka nje, jwtz ifahamike Afrika nzima kwa ku miriki kiwanda cha kuzalisha sukari, mafuta, ngano!
Mnaingia MOU na sekta binafsi, tuna kuwa na akiba ya nafska ya kulisha Afrika nzima!
Au kubadilisha matumizi ya kuni na kuwa gesi kwenye magereza yote,
Au kwenda mbali zaidi kuanzisha karakana ya kuzalisha vitu vya IT, au assembling plant ya magari,
Kwenye branches za majeshi kuna, Airwing,navy, na army(infantry), sasa hv imeongezeka Cyber na space, bongo zipo? Hawa Kenge wanachowaza ni kupiga watu mitama na kunyangsnya leso na kaptura, akili finyu kabisa,
Mwanajeshi tena unakuta wapo zaidi ya mmoja, mnatesa raia, na mnaona ufahari kabisa!
Hii ndio shida ya ku recruit failures wa form four.
Stupid kabisa. Yanaenenda kama mambuzi