JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Asiesikia la mkuu huvunjika guu, hakuna marefu yasio na ncha, safari 1 huanzisha nyingine, za mwizi 40, Simba mwenda Pole ndio hula..., Za kuambiwa changanya na Zako,msije mkasema hakukumbushwa
Kula chuma hiko
---

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema siku saba zilizotolewa kusalimisha mavazi yanayofanania na sare za jeshi kwa hiari zimeisha, hivyo jeshi litaingia kuzisaka nguo hizo kwa wananchi.

Kaimu mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema jeshi halina utani katika suala hilo, kwani katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 na kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa.

“Muda wao wa kusalimisha kwa hiari umeisha, kama mtu atakuwa hajasalimisha basi tutazifuata wenyewe, na mtindo upi tutatumia kuzichukua kwa wananchi tunajua wenyewe,” amesema Kamanda Ilonda.

Ameongeza kuwa sheria inakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ au zinazofanana na sare hizo bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.
Itoshe kusema ni wapvmbavu
 
Hapana sio njaa Mkuu, TRUST me!!

Hapa kuna gem inachezwa hapa!!

Tumia akili,wait for a few days!!
Hakuna kitu hapo. CCM ina mizizi kila sehemu hapa nchini wana green card hao ni wanachama wa kufa na kupona wa kijani.

Mifumo ya kikomunisti sometimes ni ya kifala sana ina haribu security kabisa inakuwa loyal to the party first before country.

Walking dead country.
 
Back
Top Bottom