Kabendera, Kitabu pekee hakina nguvu ya kumfanyia Mtu Character Assassination kwenye nchi Maskini hasa za Afrika

Watanzania wengi waliishi kwa unafiki kwasababu ya mfumo aliouweka haikuwa rahisi watu ku reveal hisia zao hadharani.

Lakini bado naungana na wewe kuwa watu walikuwa wanampenda (ila napinga factor ya kusema walikuwa ni wengi)

Kuna watu wamepata kazi kwenye mifumo ambayo iliharibiwa na connection.

Kuna watu walidhurumiwa na watu wenye nguvu lakini kupitia yeye haki zao zililipwa.

Kiukweli amefanya mengi kuigusa jamii na hilo nitakuwa mjinga kama nitapinga.

Kama binadamu nakubali kuwa alikuwa na mapungufu yake na pia alikuwa na mazuri yake.

Lakini katika mapungufu ya binadamu kuna mzani ambao mapungufu hayo tunayapima na kuangalia ni kwa kiasi gani tunaweza kuya ignore na ku move on na mazuri.

Mfano tunaweza kutambua kuwa ndoa zina changamoto na hizo changamoto zinakuja kwa mapungufu ya binadamu.

Mume ambaye alikuwa anamjali sana mke wake kwa kufanya kila kitu cha kumridhisha ikiwemo kumnunulia zawadi mbalimbali ili awe na furaha.

Then siku ikatokea mke amezidisha chumvi kwenye chakula halafu reaction ya mume ikawa ni kumgombeza kwa ukali.

Wote tukisimuliwa hicho kisa basi katika mizani ya mapungufu ya binadamu tunaweza kuona hiyo kama ni sehemu ya weakness ya mwanaume na pengine tukamshauri mwanamke a-move on.

Lakini kama story hiyo ikawa mume kuishia kumchinja na kisu mke wake kwasababu ya kuzidisha chumvi, hatuwezi kusema ni mapungufu ya binadamu kwa kitendo hicho.

Na kwamba tunapaswa kuachana na mabaya hayo na kukumbuka mazuri ya huyo mwanaume kwa jinsi alivyompa zawadi mbalimbali mke wake hadi kwenye siku ya birthday yake.

Hiyo haiwezi kuwa sawa

Lazima tukubaliane kuna viwango vya ubaya ambavyo mtu ukivifanya unakuwa umevuka mstari. Watu hawawezi kuona thamani ya yale mazuri uliyoyafanya.

Magufuli kama kweli alihusika na hayo mauaji tena kwa mkono wake basi hoja ya kusema alisaidia sijui kupata lami itakuwa ni ujinga unless huyo aliyeuliwa ithibitishwe alikuwa jambazi aliyehatarisha maisha ya raisi kwa wakati huo.

Nje na hapo utabaki kuwa utetezi irrational tu. Na ukitaka kujua how it feels jiweke kwenye nafasi za familia za hao wahanga kisha pima hoja za kuonesha mazuri ya JPM kama zitakuwa valid kwako.
 
Sio kila Jambo linahitaji Takwimu. Ninyi wenye Elimu za kukariri ndio maana hata mambo madogo yanawashinda.


Unazungumzia authority ipi?


Wewe unapojadili hapa unanifahamu?
Hapa JF forum tunajadili ideals hatujadili Personality za mtu

Ideals behind ,Hujasoma kitabu na huna takwimu yeyote ile

Haiwezekani kila mtu akiota ndoto anaandika mambo ya kufikirika .Tunahijadi takwimu

Kama huna takwimu huna haki ya kuongea na yale unayoongea yanabaki hadithi kama hadithi tu
 
Kuna mambo hayahitaji takwimu wala Tafiti.
Magufuli ni habari nyingine kwa Watanzania waliowengi. Kwao ni kama Nabii.

Sisemi kishabiki nazungumzia ukweli uliopo

Magufuli yupo kaburini mwaka wa pili ama wa mwaka wa tatu huu, bado watu waanahangaika Na kivuli chake.

Namna sahihi ya kumfuta Magufuli Ni kuua miradi yote aliyopigania kama SGR, Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power, Kigongo-Busisi Bridge, Magufuli Bridge (Posta-Masaki), Flights kutaja miradi michache...ikiwa hii miradi itaendelea kuishi, hakuna andiko litamchafua Magufuli
 
Usipende kuandika mambo kwa ujumla jumla hapa JF

Una uhakika watanzania wengi ni maskini au wewe ndiwe maskini?

😲😲
Ndio maana nilikuuliza unaishi Tanzania?
Kama hujui Watanzania wengi ni Maskini basi ninajadili na special number
Unaposema watanzania hawajui kiingereza ,Usiandike kwa ujumla jumla .labda watu wako wa karibu ndio hawajui kiingereza
😂😂
Kama hujui Kingereza ni changamoto kwa Watanzania wengi na Hapa nazungumzia zaidi ya 90% kingereza kinawapiga chenga

Dunia ya teknolojia leo unaweza tafsiri kichina ,kijerumani kwa lugha yako.Wewe hutumii AI ?Hicho kitabu ndani ya AI ni siku ngapi unasoma kwa kiswahili?
Sisi wenzako biashara zetu zinaendeshwa na teknolojia hasa za mawasiliano, simu janja.
Kwa uelewa wako ni Watanzania wangapi wana simu janja? Nikikuambia hawafiki Milioni 15 utabisha,

Sasa watu wa degree baadhi Yao hawajui kutumia email tuu bado huoni tuko nyuma? Wewe unaleta mambo ya AI hapa
Kwa mujibu wa wizara ya elimu ,Elimu ni bure na watoto wanajifunza kiingereza toka shule ya msingi au ule mtihani wa kiingereza wanafunzi wanajibu kwa kiswahili

😂😂😂

Mambo ya Elimu achana nayo Mkuu. Huko unaenda matawi ya juu ambayo huwezi kuyarukia.
 

Magufuli alifanya yote: Mema alifanya, tena vizuri hasa.
Mabaya pia alifanya, kwa kishindo.

Magufuli hakuwa vuguvugu...
 

Kwako Takwimu ni nini?
 

Mimi binafsi sikuvutiwa na Siasa za Magufuli ila hiyo haimaanishi hakuna mazuri ambayo hakufanya hasa ya miundombinu.

Lakini tukija kwenye suala la kupendwa, Watanzania wengi walimpenda Magufuli.
 
Umechambua vizuri Ila kuhusu Magufuli kupendwa sana hii sio kweli

Magufuli ndo rais Pekee alipokufa watu walikesha bar kunywa na kula .

Japo Mimi nilikuwa namkubali Ila watz wengi walikuwa hawampendi .
Takwimu zake inawezekana ziko sahihi kwasababu watanzania wengi ni watu wa kipato cha kawaida na wachache ndio ambao wako na kipato cha kati.

JPM alikua anakubalika sana na wanachi wa kipato cha kawaida kwasababu mambo mengi yanayozungumzwa aliyafanya hayakuwa yanawagusa wao moja kwa moja ila wao walikua wanaguswa na matokeo ya miradi iliyokua inafanyika na hatua zilizokua zinachukuliwa kwenye mambo kadha wa kadha.
 

Kwa Watanzania wengi Magufuli ni Nabii.
Hata ungeua miradi yote bado wao wanamuamini na kumpenda.

Hapo mpaka kizazi hiki kiishe
 
Hakuna mwenye akili timamu aliyekuwa anampenda yule mzee,sisi ndani ya chama pia tulimchukia
 

Mimi binafsi sikuwa na mkubali
Lakini nakuambia hivi, chunguzi zangu tangu Akiwa HAI na sasa hayupo, Magufuli anapendwa Sana na watu wengi(Watanzania wa Tabaka la chini)
 
Kwa Watanzania wengi Magufuli ni Nabii.
Hata ungeua miradi yote bado wao wanamuamini na kumpenda.

Hapo mpaka kizazi hiki kiishe
Magufuli ni nabii labda kwenu nyie wakristo wachache, maana mnapachikana tu vyeo vya unabii,hakuwa na sifa hizo hata robo
 
Sijui kama atakuelewa, ila umemjibu kwa kiwango cha juu kabisa.
 
..Ukweli ni ukweli tu hata ikipingwa

Ukweli ukikataliwa hugeuka kuwa Uongo na uongo ukikubaliwa huwa Ukweli.

Ukweli ni ishu ya kifalsafa lakini pia ukweli ni ishu ya kimahesabu
Lakini pia ukweli ni ishu ya kisayansi.

Mfano, watu wanasema siku hubadilika saa sita za usiku, na wengine wanasema siku hubadilika saa 12 jioni. Yupo hapo anasema kweli na yupi anasema Uongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…