Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Ongezea na hiyo hapo Ezekieli 24:14 uiosome pamoja na hiyo Yohana 14:6. Uwe ni wa kimila
au vyovyote vile utakavyo, maadamu umeumbwa hujajiumba na huna uwezo wa kujiumba.... Ukishajua kuna Mungu, na Mungu huyo kayaweka/kayapanda maadili mema moyoni mwako tangu kuzaliwa kwako basi na ijulikane kwamba tayari dhambi ina kuhusu. So kinachofuata hapo ni kutakiwa kujinyenyekeza kwa huyo Mungu wa Mbinguni ili Neema yake isikupitie pembeni.
Haya yote hayana maana ikiwa Yesu ni mmoja halafu nyie sio wamoja, kila kikundi kina mambo yake mfano wasabato wanawaita Roman katoliki ni wapagani, sasa wewe endelea kulala
 
[emoji3][emoji3][emoji3] ukiachana na nyuzi za kuchakatana na kula kimasihara , uzi wa mambo ya dini "nani yuko sahihi" huwa unakua mrefu balaa !! Anyway mimi pia huwa napata utata maana baada ya kufa pia tumehaidiwa zawadi mbalimbali , haya maisha tutakayoishi baada ya kufa yametofautiana pia Waislam wamehaidiwa , wakristu (ukisoma hasa unaweza kuona picha ya mbingu itakavyokua) wamehaidiwa ya kwao pia !!! Sasa kama dini zote zimetoka kwa Ibrahimu ina maana tutawekwa mbingu tofauti tofauti ? Mfano kwa wakristu itakua ni kumtukuza Bwana , tukiwa na hao wazee ishirini na nne ! Milele kwa Wenzetu mambo ni tofauti !!
 
Ni kutafuta nguvu ya imani tu hakuna kingine, viongozi wote wa dini ni lazima wasome theology na theology ni moja, na ni mojawapo ya nguzo ya imani katika dini zote.

Kwann dunia isingekua na dini moja tu na wapagani af iyo dini moja ndo ina hangaika kuwa lingania wapagani waingie kwenye dini ya kweli...
 
Hili haliwezi kutokea sababu na siyo lengo. Mfano wa watu wa dini ni mfano wa wewe unavyo mkana Mola, muda ambao humju Mola mwenyewe wala huna ushahidi. Hali hii ndivyo ilivyo mpaka kwetu tunao muamini Mola, kwamba wapo watu wanafata matamanio yao kwa makusudi na kuacha haki kwa makusudi na kuyakataa maandiko kwa makusudi.

Kwahiyo usijitoe katika hili, hali ya kuwa unachokifanya wewe ni kile kile wanachokifanya watu wa imani.

Kingine,wakana Mungu wote wana matatizo ya akili.

Shukrani.
Ulimuita kafiri Mokaze na wakati ni fellow muslim
 
1. Yesu akasema "Huwezi kufika Kwa baba yangu bila kupitia Mimi"

Yesu akasema "mama angu na ndugu zangu ni wale washikao mafundisho yangu na kuzitii amri zangu"

Ili ufike kwa Mungu lazima uokoke.

2. Waislamu "Mungu ni mmoja na yeyotee afananishaye Mungu na vitu vyengine afanya shiriki""

Mfanya shiriki yeye ni motoni.

Mungu ni mmoja na Mtume wake ni mmoja nae ni Mtume Mohammed S.A.W

Sasa kuna yule mtaka kufika peponi, huoni anachanganywa tu?

#YNWA
Mungu ni cheo Unaposema Mungu ni mmoja ni sawa na kusema Raisi duniani ni mmoja, Mungu wenu waislam anaitwa alla Mungu wa wa Kristo tunamwita JEHOVA mungu wa wahindi anaitwa krishina, sasa wewe unaposema mungu ni mmoja na mtume ni mmoja ambaye ni mhamedi uyo ni mungu wa waislamu, msingi wake ni babeli kwa waabudu mwezi na nyota na mawe kama lile lililopo makka
 
1. Utatu mtakatifu, hajafundisha mafundisho haya Yesu.

2. Kwani Wakristo mnamkubali mtime Nabii ? Mbona unauliza swali la kitoto sana na kupotezeana muda ?

Umekimbia kusema Mtume Muhamadi SAW ndiye Roho Mtakatifu.
 
Haya yote hayana maana ikiwa Yesu ni mmoja halafu nyie sio wamoja, kila kikundi kina mambo yake mfano wasabato wanawaita Roman katoliki ni wapagani, sasa wewe endelea kulala

Kwa amri ya Mungu Ibrahim alimtimua Hajiri na Mwanae Ishmaili unashangaa ni sasa? Mungu hakusubiri Magugu na ngano vimee pamoja . Alijua gugu ni lipi ambalo moyo wake uliekea kwa shetani huko kwa miungu ya mamaye Hajiri na kwamba hangeweza kurithi pamoja na yule ambaye moyo wake ulielekea kwa Mungu wa Agano na Baba yake Ibrahim . Yaani Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.
 
Mungu yupi wakati wenyewe mmeshindwa kuelewana kuwa ana vitabu 66 au 73?Mungu yupi huyo wa wasabato au Roman katoliki? mngekuwa mnamjua huyo Mungu mngekuwa kitu kimoja acha porojo
 
Scenario
Naomba ni declare interest "Mimi ni mkristo Tena Mlutheri".
Hivi lipokuja swala la kuwaaminisha hawa wasio amini Mungu yupo "Kwanini sisi Tunaoamini Mungu yupo TUSIWE NA SAUTI MOJA?"

Flash back
Nimekuwa nikisoma nyuzi nyingi tu juu ya wasio amini Mungu yupo wakitoa madini yao.
Lakini pia nimekuwa nikisoma juu ya wanaoamini Mungu yupo wakitoa madini yao pia.

The Problem
Ila mi binafsi nahisi Kuna tatizo kwa "Sisi Waamini Mungu"
We fungua Uzi wowote kwa wasioamini Mungu, utaona kila mwamini Mungu yupo anatoa ushahidi wake ambao ni tofauti na ushahidi wa mwengine.

Hebu soma ushahidi wa wakristo juu ya Mungu yupo?
Then soma ushahidi wa Waislamu juu ya Mungu yupo?

Utaona japo wote wanaoamini Mungu yupo ila kila side ina views zake na comments zake ambazo sometimes zinatofautiana kabisa yaani ZINAPINGANA.

We Waambie watoe view juu ya Mungu yupo kupitia Maandiko yaliyomtaja Yesu na Mtume Mohammed S.A.W utaona wako tofauti na kama hata wao ""Wanakinzana na kugombana kimawazo""

Sasa najiulizaga "Ikiwa kama sisi Tunaoamini Mungu yupo" tunazinguana..!! Tutawezaje kumuaminisha huyu ambae haamini Mungu yupo Akaamini?

The Paradox
Nina rafiki zangu wawili John (Mlokole - namwitaga baba Mchungaji) na Khadija (Sunni - huyu namwitaga ustadhati mzuri..!!!)

Hawa watu wawili kama wewe ukitaka kupata ""Confusion kichwani mwako"" we waulize swali kama ""ikiwa Imani ndio msingi mkuu wa kufata mafundisho ya Mungu ili twende peponi basi Motoni anaenda wa Imani gani?""

Atakachokujibu baba Mchungaji ni tofauti kabisaa na ustadhati wangu mzuri..!!!

What is Behind?
Sasa huwa najiuliza
1. Mungu hajui huu mkanganyiko alionao Khadija na John juu yake?

2. Huyu Mungu atawachoma wakina Khadija au wakina John kwasababu kati yao mmoja anatumia njia isiyofaa kumfata yeye (Haya ndio mawazo ya John na Khadija, huyu shika Biblia huyu shika Quran)...??

3. Huwa najiulizaga ""Kwanini Mungu asitoe tu one statement ili kutoa one truth true..!!""
Maana ukitaka kujua juu ya Habari za Mungu na Pepo, na Jehanamu basi John atakufundisha hivi na Khadija vile...!!!! Yaani tofauti Tena kwa kupingana kabisaaa.

Kwanini Mungu asiseme yeye mwenyewe "Kundi hili ndio lipo sahihi na nyie wotee nifateni kwa staili ya kundi hili"

Conclusion
Kama sisi " Waamini Mungu yupo" tumeshindwa kuelewana na wenyewe kuwa Mungu ni wa upande gani, Je kuwaaminisha ""Wasioamini Mungu yupo"" ya kwamba ""Mungu anataka Mafundisho ya kina John au Khadija"" Tutaweza kweli??

Mi nafikiria sisi Tunaoamini Mungu tukae kikao..!!! tuelewane kwanza then ndio tuwafate wasio amini Mungu ndio ""TUWAPE HABARI ZA MUNGU""

#YNWA
Tangu nimeanza kusoma hizi thread za atheists na deitists sijawahi kutana na mada poa kama hii

Leo ukumbi ni wa deitists,siye atheists tukae kando
 
Kuanza kuhoji tu undani wa hizo dini zenu inaonesha tayr akil yako imeanza kufanya kazi kutoka kwenye vifungo vya iman za kishenz ambazo zlikuja kuiharibu akili ya mtu mweusi.

Kwa wengine wa imani zenu ni kufuru kuuliza ama kuhoji maswal kama yako maana utaonekana mpagani na mtu asiyemuogopa huyo Mungu wa peponi sjui mbinguni.

Kimsingi imani na dini zote si sahihi maana ukifuatilia zote kiundan zinamakosa na zote zipo chini ya lengo moja na muanzilishi mmoja aliekuwa na targets zake kwa jamii fulani.

Kiuhalisia dini zote asili yake ni imani za kishirikina ambazo ziliabudiwa na mababu wa kiafrika ya kale yaani misri na sehem zingine baran Africa, na baada ya ujio wa races za watu weupe na kuanza kustaharabika wakazicopy hizo imani na kuzistaharabisha kwa kubadili histories, majina na wahusika wa hizo imani na ndipo ujio wa dini na misahafu ukaanzia hapo.

Uwez sema asiemuamini Allah atachomwa moto wakat hiyo dini imaenza juzi tu miaka ya 1400 iliyopita, na kabla yake kuna maelfu ya imani zilikuwepo kabla yake.

Na huwez sema asiyemuamn yesu atachomwa moto wakat kbla ya miaka 2000 kuna wakina Osiris, azazel, Krishna waliwai kuwepo kabla yake na walikuwa na miujiza kama ya huyo yesu na hawa ndio origin copies za stories za jesus ambao nao asili yao ni miungu ya waafrika wa kale.

Hakuna ukwel ktk dini ndiomaana mnapingana ninyi kwa ninyi.

Ni bora usiamin dini na miungu yake, kulko kuwa mpumbavu usiyejua nini unachokiabudu na kuipa sifa jamii fulani iliyokuletea uo upuuzi.

Mungu yupo lkn si huyo mnaemuabdu ktk magenge yenu ya dini.

Muumba wa kweli hana haja na dini ili umjue, bali kufuata sheria za uumbaji, upendo kwa viumbe wake na kutii sheria za , jamii yako unayokuzunguka.

Mbingu na motoni hazipo na hazitowai kuwepo maana ziliundwa na hao wana dini ili kuwatisha watu na kuwafanya waoga na watumwa wa imani.

Mtakesha kusubiri ujio wa hivyo viumbe vyenu na havitorudiii maana havijawai kuwepo.

Kupinga mafundisho ya dini isiwe kigezo cha kumuita mtu mpagani, maana hata wew unakuwa mpagani kwa kuikana imani ya uafrica na kukumbatia imani za mtu mweupe ambazo ni uongo na copy ya ile origin ya imani za babu zako.
View attachment 2201191
Ahahhahh

Huyo wa tatu anafurahisha
 
Soma comment za juu hapo wakristo na waislamu kila mtu ANAVUTIA KWAKE.

Sisi Waamini Mungu na wao Wakanaji nani ana matatizo ya akili?

Wakanaji wotee wanasauti moja "Mungu Hayupo" mbona sisi Waamini "Kila mtu ana lake?" Huoni sisi ndio wenye matatizo?

#YNWA
Kweli wao wenye matatizo
 
Ni kutafuta nguvu ya imani tu hakuna kingine, viongozi wote wa dini ni lazima wasome theology na theology ni moja, na ni mojawapo ya nguzo ya imani katika dini zote.
Theologia siyo moja kuna aina tano za theology duniani kwa hiyo tofauti hazitakaa ziishe.
 
Scenario
Naomba ni declare interest "Mimi ni mkristo Tena Mlutheri".
Hivi lipokuja swala la kuwaaminisha hawa wasio amini Mungu yupo "Kwanini sisi Tunaoamini Mungu yupo TUSIWE NA SAUTI MOJA?"

Flash back
Nimekuwa nikisoma nyuzi nyingi tu juu ya wasio amini Mungu yupo wakitoa madini yao.
Lakini pia nimekuwa nikisoma juu ya wanaoamini Mungu yupo wakitoa madini yao pia.

The Problem
Ila mi binafsi nahisi Kuna tatizo kwa "Sisi Waamini Mungu"
We fungua Uzi wowote kwa wasioamini Mungu, utaona kila mwamini Mungu yupo anatoa ushahidi wake ambao ni tofauti na ushahidi wa mwengine.

Hebu soma ushahidi wa wakristo juu ya Mungu yupo?
Then soma ushahidi wa Waislamu juu ya Mungu yupo?

Utaona japo wote wanaoamini Mungu yupo ila kila side ina views zake na comments zake ambazo sometimes zinatofautiana kabisa yaani ZINAPINGANA.

We Waambie watoe view juu ya Mungu yupo kupitia Maandiko yaliyomtaja Yesu na Mtume Mohammed S.A.W utaona wako tofauti na kama hata wao ""Wanakinzana na kugombana kimawazo""

Sasa najiulizaga "Ikiwa kama sisi Tunaoamini Mungu yupo" tunazinguana..!! Tutawezaje kumuaminisha huyu ambae haamini Mungu yupo Akaamini?

The Paradox
Nina rafiki zangu wawili John (Mlokole - namwitaga baba Mchungaji) na Khadija (Sunni - huyu namwitaga ustadhati mzuri..!!!)

Hawa watu wawili kama wewe ukitaka kupata ""Confusion kichwani mwako"" we waulize swali kama ""ikiwa Imani ndio msingi mkuu wa kufata mafundisho ya Mungu ili twende peponi basi Motoni anaenda wa Imani gani?""

Atakachokujibu baba Mchungaji ni tofauti kabisaa na ustadhati wangu mzuri..!!!

What is Behind?
Sasa huwa najiuliza
1. Mungu hajui huu mkanganyiko alionao Khadija na John juu yake?

2. Huyu Mungu atawachoma wakina Khadija au wakina John kwasababu kati yao mmoja anatumia njia isiyofaa kumfata yeye (Haya ndio mawazo ya John na Khadija, huyu shika Biblia huyu shika Quran)...??

3. Huwa najiulizaga ""Kwanini Mungu asitoe tu one statement ili kutoa one truth true..!!""
Maana ukitaka kujua juu ya Habari za Mungu na Pepo, na Jehanamu basi John atakufundisha hivi na Khadija vile...!!!! Yaani tofauti Tena kwa kupingana kabisaaa.

Kwanini Mungu asiseme yeye mwenyewe "Kundi hili ndio lipo sahihi na nyie wotee nifateni kwa staili ya kundi hili"

Conclusion
Kama sisi " Waamini Mungu yupo" tumeshindwa kuelewana na wenyewe kuwa Mungu ni wa upande gani, Je kuwaaminisha ""Wasioamini Mungu yupo"" ya kwamba ""Mungu anataka Mafundisho ya kina John au Khadija"" Tutaweza kweli??

Mi nafikiria sisi Tunaoamini Mungu tukae kikao..!!! tuelewane kwanza then ndio tuwafate wasio amini Mungu ndio ""TUWAPE HABARI ZA MUNGU""

#YNWA
kama kundi ni ngumu kuondoa tofauti
Kila kundi lina misimamo yake migumu.
Hapa ni kila mtu mmojammoja kujifunza hizi dini zoote then ufanye uchaguzi
 
Haya yote hayana maana ikiwa Yesu ni mmoja halafu nyie sio wamoja, kila kikundi kina mambo yake mfano wasabato wanawaita Roman katoliki ni wapagani, sasa wewe endelea kulala

Ulisha sikia wapi hii tofauti imefanya Neno la Mungu/Injili ya Bwana Yesu isi hubiriwe? Huoni hata wewe imekufanya ujiingize uzungumzie hiyo tofauti na kwa kufanya hivyo jiwe nalo kwa kutokujua linazungumzia Habari Njema kwa watu wote ya Bwana Yesu.
 
Ulisha sikia wapi hii tofauti imefanya Neno la Mungu/Injili ya Bwana Yesu isi hubitrwe? Huoni hata wewe imekufanya ujiingize uzungumzie hiyo tofauti na kwa kufanya hivyo jiwe nalo kwa kutokujua linazungumzia habari njema kwa watu wote ya Bwana Yesu.
Injili ipi wakati wenyewe hamuelewi, ndio maana wote mnadai kumuamini Yesu huku wengine mkiitana wapagani
 
Back
Top Bottom