South Africa hawawezi kupigana katika hiyo misitu ya Congo kuwashinda Rwanda, SA hawewezi kupigana na jeshi la Rwanda DRC au Rwanda yenyewe wakatoboa bila kupata msaada wa Tanzania na Uganda kufunga mipaka yake na Rwanda.
Kwani hasa vita itapiganiwa wapi? Yaani ili SA apigane na Rwanda na pia ili Rwanda ipige SA?
 
Kagame anatoa wapi ujasiri wa kumvimbia Ramaphosa?
 
Wanajeshi wa SA watanyooshwa sana kwenye misitu ya Congo, hawajawahi hata kupigana vitu kubwa kama wanajeshi wa Rwanda ambao vita ni maisha yao.
Huna historia ya SANDF, although wao vita vyao wamepigana sana kusini mwa jangwa la sahara. Na ni wataala wa bush wars. Popular vita ni border war 1966 - 1989, ziko nyingine walizoshiriki before hapo. Lakin pia kuna mission under kofia ya UN

So kusema hawana uzeofu, maybe hufaham historia
 
Putin hajawahi kuwa Tanzania miaka minne kufundisha sijui watu gani. Soma miaka hiyo Putin alikuwa wapi, na umri gani, akifanya nini.
 
Hiyo border war ya SA na Namibia ilikuwa vita vya jeshi la makaburu halafu ni bush war(vita vya vichakani) sio vita vya msituni kama msitu wa Ikweta mashariki ya DRC. Wanajeshi wa SA wakiingia mashariki ya Congo wakipigwa mvua moja tu wanaugua homa wanaanza kutetemeka kama kuku wenye mdondo/kideri.
 
Jibu ni ndio. Ila ulipokosea, kuhusu matokeo. Nani ataibuka mashindi?!
 
Kuhusu kuuza silaha;

South Africa kuna kiwanda cha makombora yatumikayo kwenye mizinga ya masafa marefu na mafupi, ardhini na majini. Rheinmetall Denel Munition.

Kiwanda kinauza bidhaa zake duniani kote, hasa nchi za umoja wa NATO.

Pia Wana tengeneza na kuuza general purpose machine gun, inatumika na Kenya pamoja na nchi za Amerika ya kusini.

Pia ni watengenezaji na wauzaji wa Armoured personnel carriers (APC), zinazotumika nchi nyingi barani Africa na nje, mfano: Uganda, DRC, Nigeria, Egypt, UK, Sweden etc.
 
Naomba kuuliza.., Hivi wa Tutsi wa Congo ni watu wa Rwanda au ni Watu wa Congo ?; Nadhani Congo ikae na watu wao wote (ikiwemo hao Watusi na nchi nyingine ziache kuwaingilia Congo na kuiba rasilimali zao ikiwemo Uganda, Rwanda na Mataifa ya nje.
Hiyo ndio loophole anayoitumia PK kuingiza jeshi lake huko wanajichanganya na Tutsi wa Kongo,akiulizwa anadai M23 ni raia wa Kongo kumbe sasa ni mixer(Congolese Tutsi + Rwandese Tutsi = M23).

Watutsi hawaachani kamwe.

PK anadhani watu ni wapumbavu kumbe wanamchora tu,kitamlamba muda si mob.
 
Okay PK ana makosa (kama walivyo Waganda na Mataifa yote ya nje yanayoingia na kuiba) ila swali langu bado lipo palepale Watutsi wa Congo ni wa Congo au Wanyarwanda ?

 
Mungu akitaka kukupa anguko anakutia kwanza kiburi
 
Ni wa Kongo mkuu.
 

View: https://www.instagram.com/reel/DFcfQU-T000/?igsh=MXQ3N2g1eDZxM25ycA==
 
Rwanda ni kama glass ilivunjika ika unganishwa na gundi mkigusa tu wana vunjana ndani wao kwa wao ..Too bad na Tz wapo wakati CDF ana toa warning kuhusu mamluki chura kiziwi alikua ana tabasamu tu ana waza atarudi lini Tunguu Zanzibar
 
Nakuunga mkono asilimia 1000 kwani madaraka kupita kiasi hulevya kupita kiasi. Kagame akumbushe kilichompata nduli Idi Amin alipoichokoza na kuichokonoa Tanzania. Awaulize wareno kilichowapata Angola na Msumbiji.Kagame

Nakuunga mkono asilimia 1000 kwani madaraka kupita kiasi hulevya kupita kiasi. Kagame akumbushe kilichompata nduli Idi Amin alipoichokoza na kuichokonoa Tanzania. Awaulize wareno kilichowapata Angola na Msumbiji.
KAGAME anaugonjwa, psych condition inaitwa MEGALOMANIA (Megalomaniac is someone who has an unnaturally strong wish for power and control, or thinks that they are much more important and powerful than they really are), SADF wanauwezo wa ku obliterate Rwanda kwa wiki moja bila boots kugusa arithi.
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemuonya Rais Cyril Ramaphosa akisema Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepotosha mazungumzo yao ya Faragha waliofanya na kusema kama Afrika Kusini inataka makabiliano basi Rwanda iko tayari kujibu.

Katika waraka wake mzito alioandika kwenye Mtandao wake wa X, Rais Kagame amesema alifanya mazungumzo mawili wiki hii na mapema jana na Rais Ramaphosa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC, akisema kuwa kile kilichosemwa na maafisa wa Afrika Kusini na Rais Ramaphosa mwenyewe kuhusu mazungumzo yao kwenye vyombo vya habari kimejaa upotoshaji mwingi.

Rais Kagame amesema ikiwa maneno yanaweza kubadilika kiasi hicho kutoka kwenye mazungumzo hadi kwenye tamko la umma, inasema mengi kuhusu jinsi masuala haya muhimu yanavyoshughulikiwa.

Rais Kagame amesema ikiwa Afrika Kusini inataka kuchangia suluhisho la amani huko Mashariki mwa DRC hilo ni jambo jema, lakini haina nafasi ya kuchukua jukumu la mpatanishi au msuluhishi. Na iwapo Afrika Kusini itataka makabiliano, Rwanda iko tayari kujibu hilo.
 
Ukweli tu esemwe rwanda si Ile sababu ni kua na uongoz Bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…