Kagame: Rwanda is ready for a confrontation with South Africa if necessary!
Vita ni strategy, administration na logistics na zote hizo ni pesa mingi, vita sio mechi ya yanga na simba pale shamba la bibi!
 
Umepiga kwenye mshono, siku mabeberu yanayompanda nyuma yakimchoka na kumbwaga,.. atapigwa ashangae...maana kipigo kitaanzia ndani...🚮🚮
Hakuna mabeberu wowote wanaomsaidia Kagame kwenye hizi mishe zake, ni kwamba hawajali tu hizo vurugu za Congo.
 
Naomba kuuliza.., Hivi wa Tutsi wa Congo ni watu wa Rwanda au ni Watu wa Congo ?; Nadhani Congo ikae na watu wao wote (ikiwemo hao Watusi na nchi nyingine ziache kuwaingilia Congo na kuiba rasilimali zao ikiwemo Uganda, Rwanda na Mataifa ya nje.
 
Anachotafuta huyu mzee ni kupigwa kama ngomaa😂😂😂😂😂😂😂
 
SA ndiyo wanao fanya mazoez ya kivita na russia, china.. Kagame ana siri nying za kijasus kuhusu jesh la SA.. ISRAEL alimkalisha Iran
Kwamba majeshi mengine haya siri za rwanda sababu wanafanya nao mazoezi?

Come on, if SA kwa uzoefu na ukubwa wake wa jeshi akiamua serious ku invade rwanda they can.

But then kila vita inasababu na outcome, why wavamie?
 
Experience muhimu kwenye uwanja wa mapambano. Rwanda ni kanchi kadogo lakini mtiti wake sio wa kitoto.
Naifananisha na Israel
Uko sahihi, Drc nchi kubwa sana lakini inahangaishwa na Rwanda kanchi kadogo sana kweli kagame ni Netanyahu wa Kanda hii
 
Come on, if SA kwa uzoefu na ukubwa wake wa jeshi akiamua serious ku invade rwanda they can.
SA itaivamia Rwanda kupitia wapi ifanikiwe?? SA akiwa anasogeza hata wanajeshi buku tu kupeleka DRC au Burundi kuvamia Rwanda, Kagame anaanza na hao watakaoutumika kama base.
 
Punguzeni kula ugolo vijana.

Wewe ukimjua mwakinyo anapigana orthodox na udhaifu wake ni upande wa kushoto ndiyo utafanya uanze kumchimba mikwara kisa unajua udhaifu wake wakati kiuhalisia hauna uwezo wowote wa kusimama na mwakinyo kwenye ring.au ubovu wa Manchester united ndiyo coastal union aanze mikwara na kumkazia kwamba wakikutana man u atakula nyingi?

Rwanda amazie South Africa ambae anatengeneza silaha zake za kivita na anaziuza hadi nchi zilizoendelea huko mambele. Nyie watu asee!!

Wabongo hivi mmekuwaje?
NYie madogo hamjui kitu. Vita ni pamoja na nidhamu ya wanajeshi. SA hawana jeshi la maana. Kagame ana watu wana nidhamu. Usione SA kubwa lakini inaweza kuwa kubwa Jinga. Angalia Israel na Iran au maadui zake utaelewa. South Africa inauza silaha gani nchi zilizoendelea kwa wingi? Unadhani Kagame kuongea hivyo ameropoka au hajui athari yake? Wanajeshi wa SA. wanaweka silaha chini wanaondoka. Hawana nidhamu kabisa.
 
SA itaivamia Rwanda kupitia wapi ifanikiwe?? SA akiwa anasogeza hata wanajeshi buku tu kupeleka DRC au Burundi kuvamia Rwanda, Kagame anaanza na hao watakaoutumika kama base.
Hawa madogo hawaelewi mbinu za Kivita. Kagame anaifahamu vizuri Congo hao wa South ni wageni
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemuonya Rais Cyril Ramaphosa akisema Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepotosha mazungumzo yao ya Faragha waliofanya na kusema kama Afrika Kusini inataka makabiliano basi Rwanda iko tayari kujibu.

Katika waraka wake mzito alioandika kwenye Mtandao wake wa X, Rais Kagame amesema alifanya mazungumzo mawili wiki hii na mapema jana na Rais Ramaphosa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC, akisema kuwa kile kilichosemwa na maafisa wa Afrika Kusini na Rais Ramaphosa mwenyewe kuhusu mazungumzo yao kwenye vyombo vya habari kimejaa upotoshaji mwingi.

Rais Kagame amesema ikiwa maneno yanaweza kubadilika kiasi hicho kutoka kwenye mazungumzo hadi kwenye tamko la umma, inasema mengi kuhusu jinsi masuala haya muhimu yanavyoshughulikiwa.

Rais Kagame amesema ikiwa Afrika Kusini inataka kuchangia suluhisho la amani huko Mashariki mwa DRC hilo ni jambo jema, lakini haina nafasi ya kuchukua jukumu la mpatanishi au msuluhishi. Na iwapo Afrika Kusini itataka makabiliano, Rwanda iko tayari kujibu hilo.

#KitengeUpdates

View attachment 3218375
Ndio... Kagame anaweza kufanya hayo aliyotishia.

Kagame bado ni kipenzi cha mabeberu, hilo linamhakikishia Uhuru wa kufanya lolote.......wakumzuia Kagame kwa Sasa ni hao mabeberu tu (US & UK).

T14 Armata
 
Wanajeshi wa SA watanyooshwa sana kwenye misitu ya Congo, hawajawahi hata kupigana vitu kubwa kama wanajeshi wa Rwanda ambao vita ni maisha yao.
Kuwa muelewa mkuu vita ya msituni saivi hazina nafasi tena.....saivi ni Drone na Ndege .....

Na pia ujue vita ni uchumi GDP ya Rwanda ni USD 14.3 Bil huku GDP ya Sout africa ni zaidi ha USD 400 bil Pato jumla la Rwanda ni sawa na Bajeti ya wizara ya afya ya South Africa .....

Grow up mr.
 
Kuwa muelewa mkuu vita ya msituni saivi hazina nafasi tena.....saivi ni Drone na Ndege .....
Huwezi kukamata eneo kwa kurusha drones na ndege, wanaokamata maeneo katika vita ni askari wa miguu(infantry).
 
Uganda ya Iddi Amin ilikuwa kituko, jeshi lake lilikuwa na mkusanyiko wa wahuni na jokers tu. Tanzania ikipigana na Uganda ya leo usifikiri itakuwa kama ilivyokuwa enzi za Iddi Amini, vita vinaweza kwenda hata miaka 20.
Hakuna mabadiliko makubwa sana ni kawaida tu na sisi pia tumebadilika maana tz na jeshi la 1980 sio la sasa bwashee..
 
Back
Top Bottom