Kagame: Rwanda is ready for a confrontation with South Africa if necessary!
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemuonya Rais Cyril Ramaphosa akisema Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepotosha mazungumzo yao ya Faragha waliofanya na kusema kama Afrika Kusini inataka makabiliano basi Rwanda iko tayari kujibu.

Katika waraka wake mzito alioandika kwenye Mtandao wake wa X, Rais Kagame amesema alifanya mazungumzo mawili wiki hii na mapema jana na Rais Ramaphosa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC, akisema kuwa kile kilichosemwa na maafisa wa Afrika Kusini na Rais Ramaphosa mwenyewe kuhusu mazungumzo yao kwenye vyombo vya habari kimejaa upotoshaji mwingi.

Rais Kagame amesema ikiwa maneno yanaweza kubadilika kiasi hicho kutoka kwenye mazungumzo hadi kwenye tamko la umma, inasema mengi kuhusu jinsi masuala haya muhimu yanavyoshughulikiwa.

Rais Kagame amesema ikiwa Afrika Kusini inataka kuchangia suluhisho la amani huko Mashariki mwa DRC hilo ni jambo jema, lakini haina nafasi ya kuchukua jukumu la mpatanishi au msuluhishi. Na iwapo Afrika Kusini itataka makabiliano, Rwanda iko tayari kujibu hilo.

#KitengeUpdates

View attachment 3218375
Anaweza vizuri tuu,Jeshi la South Africa ni dhaifu ndio maana amekoromewa na Kagame 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFcIdLYCRle/?igsh=ODdiNTFscXFiaGJx
 
Majeshi ya Rwanda hayana uwezo wa kuyashinda Majeshi ya Afrika ya Kusini katika medani za kivita ubavu huo Rwanda haina.
Acha upuuzi wako,nani ana uzoefu wa kupigana vita kati ya Jeshi la Rwanda na South Africa?

Kuwa na vifaa tuu haitoshi,medani unazo?

Huoni Israel imeshindwa kuwamaliza Hamas?
 
Vita ni teknologia, Rwanda hana ubavu wa kupambana na South Africa. Rwanda hana Air defensive yeyote, ukirusha ata jiwe linaingia na kupiga popote pale. Ni mkwara mbuzi tu
Kwa nini hiyo teknolonia isizuie Wasouth 13 waliofyekwa ?
 
Experience muhimu kwenye uwanja wa mapambano. Rwanda ni kanchi kadogo lakini mtiti wake sio wa kitoto.
Naifananisha na Israel
Humu vijana wanaongozwa na ushabiki zaidi, wanafikri vita ni kurusha mabomu tu! Sasa sijui hao SA watarusha mabomu mangapi kwenye misitu ya Congo wawamalize Wanajeshi wote wa Rwanda maana hao wanajeshi wa SA wakiingia misitu ya Congo lazima wapoteane tu na kazi ya Rwanda itakuwa kuwaokota kama kuku wenye kideri.
 
Ikiwa nchi kubwa kama uganda haikufikisha miezi 7 tukaweka hadi rais wetu sembuse hiyo wilaya.
Uganda ya Iddi Amin ilikuwa kituko, jeshi lake lilikuwa na mkusanyiko wa wahuni na jokers tu. Tanzania ikipigana na Uganda ya leo usifikiri itakuwa kama ilivyokuwa enzi za Iddi Amini, vita vinaweza kwenda hata miaka 20.
 
Vita ni teknologia, Rwanda hana ubavu wa kupambana na South Africa. Rwanda hana Air defensive yeyote, ukirusha ata jiwe linaingia na kupiga popote pale. Ni mkwara mbuzi tu
Mbona Saudi Arabia wameshindwa kuwatuliza Houthi wa Yemen?
Mbona Wamarekani walikimbizwa mchaka mchaka na Vietcong huko vietnam?
 
Kagame ni yule dogo Fulani mtaani nunda ana mikwara na watu wanamgwaya kwa mikwara yake,ila siku Kuna mtu msiyemtarajia akamchoka na mikwara yake hapo kitaa akapiga kama Ngoma.

Huyo PAKA ni overrated sana,mikwara ndiyo mingi.
Umepiga kwenye mshono, siku mabeberu yanayompanda nyuma yakimchoka na kumbwaga,.. atapigwa ashangae...maana kipigo kitaanzia ndani...🚮🚮
 
Back
Top Bottom