Kagame: Rwanda is ready for a confrontation with South Africa if necessary!
maana yake wanajeshi wa FARDC waliojisalimisha ndo wanaenda kufungwa,

Mercenaries huenda wakaachiwa.

ila Tanzania tumekosea sana kutowekeza kule kivita, DRC pakiwaka sisi twaumia zaidi
 
Rwanda Iko ni dhaifu ikiwa Tanzania na Uganda wataamua kufunga mipaka kwa muda kumpa onyo.
Lakini vita na utajiri wa Congo una maslahi kwa wengi ndalni na .nje ya congo ndio maana Hilo eneo Lina matatizo kila siku
So tutarajie Kongo kuendelea kuwa failed state

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemuonya Rais Cyril Ramaphosa akisema Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepotosha mazungumzo yao ya Faragha waliofanya na kusema kama Afrika Kusini inataka makabiliano basi Rwanda iko tayari kujibu.

Katika waraka wake mzito alioandika kwenye Mtandao wake wa X, Rais Kagame amesema alifanya mazungumzo mawili wiki hii na mapema jana na Rais Ramaphosa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC, akisema kuwa kile kilichosemwa na maafisa wa Afrika Kusini na Rais Ramaphosa mwenyewe kuhusu mazungumzo yao kwenye vyombo vya habari kimejaa upotoshaji mwingi.

Rais Kagame amesema ikiwa maneno yanaweza kubadilika kiasi hicho kutoka kwenye mazungumzo hadi kwenye tamko la umma, inasema mengi kuhusu jinsi masuala haya muhimu yanavyoshughulikiwa.

Rais Kagame amesema ikiwa Afrika Kusini inataka kuchangia suluhisho la amani huko Mashariki mwa DRC hilo ni jambo jema, lakini haina nafasi ya kuchukua jukumu la mpatanishi au msuluhishi. Na iwapo Afrika Kusini itataka makabiliano, Rwanda iko tayari kujibu hilo.

#KitengeUpdates

View attachment 3218375
Kasema Rwanda ipo teyari muda wowote kwa mapambano.
#Anyday
 
embu amtunishie misuli Trump namna hiyo
Umemsahau mapema kiduku, mpaka trump ikabid afunge safari kwenda kwa kiduku wayajenge

Kagame kamdomo katamponza Hana uwezo wa kupiga souz hata kwa sekunde

Souz jesh la anga wanavifaa Bora sana
Tanzania tu akichokoza anaamka amekufa
 
PAKA bwana anataka battle na big boyz 😹
Watampiga km ngoma we muache avimbe bichwa.!!
 
Anaweza kuwapiga vizuri sana, wanajeshi wa South Africa hawewezi kupigana kwenye hiyo terrain kuwazidi Wanyaruwanda.
SOuthafrica anamtandika rwanda vizuri sana maana ndio most advanced jeshi kwa africa ila kwa kilichotokea congo sandf hawapo equiped kwakuwa lengo siyo ku attaack bali kulinda na kutetea maslahi ya congo ,ndio maana wananchi wa southafrica wanaishinikiza serikali yao iwape silaha wanajeshi wao waliowapelwka congo kwakuwa adui yani m23 na rwanda wamekuwa wakiwa target makusudi ,
Rwanda uwezo wake ni mdogo sana ukilinganisha na nchi kama tanzania, nigeria au southafrica, sema wana asili ya ukorofi
 
Kuilinganisha South Africa na Rwanda ni sawa na Kulinganisha Landcruiser na Passo
Rwanda haina uwezo wowote wa kuipiga South Africa labda uwezo wa kuotea na kurusha bomu kama alshabab. Mji mmoja tu kama Cape town au Johannesburg au hata Durban, una nguvu ya uchumi kuliko nchi nzima ya Rwanda
Kwani Rwanda itaenda kupigania vita huko Africa Kusini??
 
Nadhani Rwanda watu wanamuacha kutokana na machafuko yaliyotokea pale, ushajiuliza leo Kagame akitoka pale ile nchi itakuwaje? Sasa leo Msouth aamue vita na Rwanda unategemea nini kitatokea pale?
Ulicho sema ndio usahihi wenyewe; Rwanda inahurumiwa tu kutokana na matukio ya mauaji ambayo dunia iliwatelekeza bila kuwasaidia. Hata USA siyo kwamba wanawapenda Rwanda au wanafaidika na kitu chochote bali ni huruma tu kwa nchi ndogo ambayo huko nyuma watu wake waliuana mchana kweupe bila kusaidiwa na dunia.

Ipo siku akina Samantha wanao tumiwa na Rwanda kubembeleza Washington watachoka ama hawatasikilizwa na wakubwa wa USA. Waswahili wanasema ukibebwa bebeka, dunia inabadilika na mataifa makubwa yana changamoto nyingi hivi sasa kutokana na migogoro inayo wagusa moja kwa moja kuwa mingi kwa hiyo ipo siku wanaweza wakapuuza madai ya Rwanda.

Majibu ya Kagame kwa viongozi wenzake ni sawa na majibu ya mtoto yatima ambaye anafanya makosa mengi kwa walezi kwa vile anajua hawezi chapwa, na akichapwa walezi watesemwa vibaya na majirani. Kagame anajua kabisa Tanzania na South Africa wakipenda wanaweza kumwondoa madarakani hata kesho. Lakini vile vile anajua nchi hizi haziwezi fanya hivyo sababu zitaonekana kama mlezi anaye mnyanyasa mtoto yatima. Kwa hiyo tunao mlaumu Rais wetu Samia kwa kumuendekeza Kagame tukumbuke nafasi ya Tanzania kwa Rwanda ni kama mzazi. Tanzania inachoweza kufanya ni kumfinya kwa siri watu wasijue. Nàamini Rais Samia na Kagame kila siku wanazungumza, Europe na USA nao lazima watakuwa wanaongea na viongozi wa Tanzania kuwaomba waivumilie Rwanda.
 
SOuthafrica anamtandika rwanda vizuri sana maana ndio most advanced jeshi kwa africa ila kwa kilichotokea congo sandf hawapo equiped kwakuwa lengo siyo ku attaack bali kulinda na kutetea maslahi ya congo ,ndio maana wananchi wa southafrica wanaishinikiza serikali yao iwape silaha wanajeshi wao waliowapelwka congo kwakuwa adui yani m23 na rwanda wamekuwa wakiwa target makusudi ,
Rwanda uwezo wake ni mdogo sana ukilinganisha na nchi kama tanzania, nigeria au southafrica, sema wana asili ya ukorofi
South Africa hawawezi kupigana katika hiyo misitu ya Congo kuwashinda Rwanda, SA hawewezi kupigana na jeshi la Rwanda DRC au Rwanda yenyewe wakatoboa bila kupata msaada wa Tanzania na Uganda kufunga mipaka yake na Rwanda.
 
Wanajeshi wa SA watanyooshwa sana kwenye misitu ya Congo, hawajawahi hata kupigana vitu kubwa kama wanajeshi wa Rwanda ambao vita ni maisha yao.
Experience muhimu kwenye uwanja wa mapambano. Rwanda ni kanchi kadogo lakini mtiti wake sio wa kitoto.
Naifananisha na Israel
 
Back
Top Bottom