Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Kuna hujuma hapa,waziri mkuu aliunda tume kuhusu hizi Islamic schools kuchomwa Moto .serikali inabdi ifanye Mambo yake hapa lacvyo yacjekuwa kama Yale ya kibiti.
 
Mtoto miaka 6 anakaa bweni! Hii si sawa
Nakubaliana na wewe.

Ndio wazazi wana shughuli nyingi lakini kuwapeleka boarding school wakiwa katika umri mdogo hivyo ni kuwaonea, tena sana!!! Watu wanasahau kwamba wanapoamua kuwa na watoto moja ya jukumu wanalopata ni kulea na sio kutafuta hela tu na kuachia watu wengine malezi.

Mie bado sana kuona sababu za msingi za kumpeleka mtoto mdogo boarding school.🧐🧐
 
Hivi ujenzi wa hizi shule uchoraji wake unafanywa na wataalamu au ndio hivyo tu ??
Na emergency exit zinakuwepo?? NA huwa wanafanya drill ???
Hasa kwa watoto wadogo kama hawa unakuta Mlinzi anatoroka usiku kwenda kwenye pombe au kwa mchepuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…