Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Kagera: Watoto 10 wamefariki na 6 kujeruhiwa baada ya shule Msingi Islamic Byamungu kuwaka moto

Hiv kulikon haya matukio kutokea mara kwa mara?
IMG-20200914-WA0002.jpeg
 
Kuna hujuma hapa,waziri mkuu aliunda tume kuhusu hizi Islamic schools kuchomwa Moto .serikali inabdi ifanye Mambo yake hapa lacvyo yacjekuwa kama Yale ya kibiti.
 
Mtoto miaka 6 anakaa bweni! Hii si sawa
Nakubaliana na wewe.

Ndio wazazi wana shughuli nyingi lakini kuwapeleka boarding school wakiwa katika umri mdogo hivyo ni kuwaonea, tena sana!!! Watu wanasahau kwamba wanapoamua kuwa na watoto moja ya jukumu wanalopata ni kulea na sio kutafuta hela tu na kuachia watu wengine malezi.

Mie bado sana kuona sababu za msingi za kumpeleka mtoto mdogo boarding school.🧐🧐
 
Watoto 10 wamefariki na sita kujeruhiwa vibaya kufuatia moto ulioteketeza bweni la wavulana shule ya Msingi Islamic Byamungu iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera. Hadi sasa chanzo moto huo hakijajulikana.

Watoto waliopoteza maisha ni wa umri wa miaka sita hadi 12.

Taarifa zaidi inakuja...


Wanafunzi 10 wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya bweni la shule yao ya Byamungu English Medium Primary School iliyoko wilayani Kyerwa kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo ambalo chanzo cha moto hakijajulikana

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesitisha shughuli za malazi katika shule hiyo kwa muda.’’ Nachukua hatua nyingine za ziada, hatua ya kwanza na ya awali kabisa tunasitisha huduma za malazi katika shule hii watoto wote waliokuwa wakilala katika huduma ya hosteli au bweni huduma hiyo sasa imesitishwa mbaka itakavyoelekezwa vinginevyo’’, amesema Brigedia Jenerali Marco Gaguti alipotembelea eneo la tukio.

Amesema Sambamba na ameelekeza kamati za usalama za ngazi zote kataika mkoa wa kagera kufanya mapitio upya ya shule zinazotoa malazi, kuhakiki kwamba shule hizo kama zinavyo vibali halali vya serikali na ubora wa majengo yanayotumiwa na wanafunzi, na kuangalia mifumo ya uzimaji moto na kujiokoa inapo.

Amesisitza kuwa kama sifa hizo hazitakua zimekidhi basi hatua zichukuliwe za kufungia huduma hizo katika shule husika.

Awali Mwenyekiti wa kijiji Bw. Munaraka Muhammod aliwaomba watu walioko katibu na Itera wafike kusaidia kuuzima moto huo uliowaka kuanzia jana usiku .

Chanzo za ajali baado hakijajulikana.
Hivi ujenzi wa hizi shule uchoraji wake unafanywa na wataalamu au ndio hivyo tu ??
Na emergency exit zinakuwepo?? NA huwa wanafanya drill ???
Hasa kwa watoto wadogo kama hawa unakuta Mlinzi anatoroka usiku kwenda kwenye pombe au kwa mchepuko
 
Back
Top Bottom