TANZIA Kahama: Watu 19 wafariki dunia kwenye ajali inayohusisha trekta, hiace na lorry!

Hiace ilikua imebeba watu 31.

Mpaka mchana huu wamekufa 17 (mwingine kaongezeka asubuhi hii saa nne).

Ambao wanapumulia mashine ni 14.
 
Ile ajali ya Pandambili miaka ya nyuma iliyisababisha mpaka Mabasi yasuruhusiwe kutembea usiku ilisababishwa na Trekta lililokuwa limepaki barabarani.
 
Dah, Mola awapokee na awapumzishe mahali pema peponi ndugu zetu. Inasikitisha sana
 
Tinde to Kahama huwa najimwaga sana. Hamna speed bumps.
 
siyo tu kiduku, vinywele vichafu vimejaa vumbi vimesokotwa, sijui ndo wanaita kiduku msokoto na kisuruali kina matobo magotini na mapajani, baadhi ya boda wapuuzi sana asee.
 
Hiyo barabara hadi unafika Nzega ni kuwa makini sana kama unadrive usiku kuna matela ya Punda mengi haswa msimu wa mavuno.

Nakumbuka gari moja dogo IT lililokuwa likiendeshwa na dereva mruanda ililparamia Tela la Punda na kuua Dreva wa Punda na Mruanda na Punda wawili.

Karibu na Tinde Junction.
 
Wewe unalaumu bila kusoma habari hadi mwisho...

Hilo gari kubwa lilikuwa limepaki tu.
Trekta ni gari dogo??
Umeambiwa ni Trekta kwenye kisa hiki
Glopu ya shilingi 1000 inasababisha mauti ya watu wengi
Trekta ni nini na ww?

Na sio trekta tu magari mengi ya mizigo hasa ya mitaani humu ni choka mbaya, ukianza na hizo trekta, gari za mchanga, baadhi ya gari za taka hazinaga alama yoyote ile.
 
Hizi ajali pasipo madereva wenyewe kuacha kuendesha kwa mwendo kasi haziwezi kwisha, hatuwezi kutegemea askari wa usalama barabarani kila siku waokoe maisha yetu kama abiria ndani ya mabasi hatuwaambii madereva ukweli wapunguze mwendo.
Sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…