TANZIA Kahama: Watu 19 wafariki dunia kwenye ajali inayohusisha trekta, hiace na lorry!

Poleni sana ndugu jamaa na marafiki. Trekta trekta ndiyo zao
 
Hiance zinazidi kuchinja kanda ya ziwa
Katika kumbukumbu yangu hii ni ajali ya pili kwenye eneo hilo 1998 ilitokea kama hio Haice iliingia nyuma ya Lori la mkaa lisilokuwa na taa wala riflekta.
 
Nakala aipate kinana
Nyie team Mazombie kwahiyo saa nne usiku kwa mazingira hayo ya tukio kulikuwa na trafiki isipokuwa baada tu ya Kinana kutoa kauli?
Umejifanya kuzisahau ajali zingine za nyuma?
Au una kichwa cha panzi?
 
70% ya ajali zinasababishwa na mwendo kasi
 
Huyo dereva alikua amelewa, trekta zimekuwepo miaka na miaka, trekta ni visible inaonekana hata kama haina taa. Wenzetu wana kitu wanaiita "Random alcohol test" kwa madereva, hii ikija kwetu itasaidia kupunguza ajali kwa asilimia kubwa sana.
 
Ni nadra sana kukuta tela la trekta lina taa za nyuma,kwa hapa bongo nadra sana....hivyo yangepigwa marufuku tu kutembea usiku.
Lamda kama Sheria zimebadilika lakini nachojua haya ruhusiwi barabarani usiku
 
Mimi huwa na Drive Malori na huwa nahakikisha Bulb za taa za nyuma na Trela zinafanya kazi

Na wakati wa usiku huwa napaki nje ya Barabara au kwenye Bus stop.

Ikitokea dharura ninapanga majani kwa mita mia au zaidi pande zote pamoja na Triangle inayitakiwa kisheria japokuwa huwa inapepeperuka.

Labda aje Dereva mlevi ndio anaweza kuingia.
 
Hizi ajali pasipo madereva wenyewe kuacha kuendesha kwa mwendo kasi haziwezi kwisha, hatuwezi kutegemea askari wa usalama barabarani kila siku waokoe maisha yetu kama abiria ndani ya mabasi hatuwaambii madereva ukweli wapunguze mwendo.
Muda huo huenda abiria wote walikuwa wamesinzia.
 
Mwendo kasi,mwendo kasi,mwendo kasi na leseni za kufoji zitatumaliza dah!
 
trafik wawepo usiku na wengine mchana wapeane shift... Achaneni na maneno ya kinana hayana research [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo hatujui tunataka Nini?
 
madereva wanasahaugi kwamba wamebeba roho za watu
 
Mwendo kasi,mwendo kasi,mwendo kasi na leseni za kufoji zitatumaliza dah!
Hapo utakuwa huwatendei haki Madereva waliohusika ambao wawili ni Marehemu makosa yamesababishwa na mwenye Trekta kuingia Barabara kuu ya Dar Kigali bila taa za nyuma wala riflekta.

Huyu wa Hiace anarpiga kazi usiku huenda alikuwa anaiba ruti ili kuepukana na Matrafiki mchana na huenda ana familia na anasomesha na lazima waende choo kubwa.
 
Huyo dereva alikua amelewa, trekta zimekuwepo miaka na miaka, trekta ni visible inaonekana hata kama haina taa. Wenzetu wana kitu wanaiita "Random alcohol test" kwa madereva, hii ikija kwetu itasaidia kupunguza ajali kwa asilimia kubwa sana.
Hujui unachosema wewe... au pengine hujawahi kuendesha gari usiku.
 
Mungu awafariji wafiwa wote. AMEN
 
Kinana kashasema trafick watolewe barabarani haya ndio wanayataka Acha tuvune tulichopanda juzi nimepanda basi NBS Kutoka Tabora mpk dodoma basi halijasimamishwa ili hali lilijaza watu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…