Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Bado sana tena sana maana mwezi uliopita tu walisema mchepuko (diversion) wa kubadilishwa mkondo wa mto umekamilika lakini hawakusema lini watahamisha hayo maji waanze kujenga ukuta wa Bwawa. Kazi kubwa na ya kitaalamu kabisa ni ujenzi wa huo ukuta utakaohimili nguvu ya maji ya mto na maji ya Bwawa likijaa na kuanza kuzalisha umeme wa Megawatt 2115 tunaoimbiwa kila siku. Megawatt 2115 ni Rated Capacity ya Bwawa mambo mengine yote yakiwa sawa ikiwa ni pamoja na maji kuwa ya kutosha wakati wote lakini, lisemwalo lipo kama halipo laja, inasemekana maji ya mto Rufiji yameanza kupungua na ukweli huo unaoneka wazi kwenye Tawi muhimu la Ruaha kuliko Bwawa la Mtera. Waziri alipokuwa pale akitoa maagizo labda toka juu utafikiri anaagiza watoto maeneo ya kwenda kuchungia mifugo lakini lugha ya mwili ya waliokuwa wanaagizwa, hasa wale Weupe, ilionyeshwa kuna matatizo makubwa kwenye utekelezaji wa Mradi na ni muda tu unasubiriwa Mkandarasi afungashe vilago aende zake. Awamu hii imefanya makosa mengi ya kijinga ya kuwalazimisha Makandarasi wakamilishe Miradi ndani ya muda mfupi kuliko uliokubaliwa kwenye Mikataba ndo maana Miradi mingi inatekelezwa chini ya viwango. Haihitaji PhD kujua kuwa hakuna Mkandarasi atatekeleza Mradi kwa muda mrefu kuliko ule ambao, kwa raslimali alizonazo angekamilisha, ili apate faida kubwa. Muda uliompa Tenda ambao uko kwenye Mkataba ndo ufuatwe na pande zote mbili.Bado sana
Lakini si anahabarisha wananchi?Kalemani tumemzoea kuwa ni Waziri anayependa kuongea kama wasanii wa bongo movie. Yeye alimradi apigwe picha na atokee kwenye TV.
Siamini kuwa STIGLERS gorge power project itakuwa imefikia hapo. Sioni tukipata umeme huo hata 2025, na hili Meko analijuwa na ndiyo maana kauli za kutaka kuongeza muda wa utawala zinapoanzia.
Ethiopia wamepigwa pini na Misri amabayo imesema mgawo wao w maji usipungue hata kidogo.Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Tatizo viongozi wetu wanatuchukulia kama mazobaBado sana tena sana maana mwezi uliopita tu walisema mchepuko (diversion) wa kubadilishwa mkondo wa mto umekamilika lakini hawakusema lini watahamisha hayo maji waanze kujenga ukuta wa Bwawa. Kazi kubwa na ya kitaalamu kabisa ni ujenzi wa huo ukuta utakaohimili nguvu ya maji ya mto na maji ya Bwawa likijaa na kuanza kuzalisha umeme wa Megawatt 2115 tunaoimbiwa kila siku. Waziri alipokuwa pale akitoa maagizo labda toka juu utafikiri anaagiza watoto maeneo ya kwenda kuchungia mifugo lakini lugha ya mwili ya waliokuwa wanaagizwa, hasa wale Weupe, ilionyeshwa kuna matatizo makubwa kwenye utekelezaji wa Mradi na ni muda tu unasubiriwa Mkandarasi afungashe vilago aende zake. Awamu hii imefanya makosa mengi ya kijinga ya kuwalazimisha Makandarasi wakamilishe Miradi ndani ya muda mfupi kuliko uliokubaliwa kwenye Mikataba ndo maana Miradi mingi inatekelezwa chini ya viwango. Haihitaji PhD kujua kuwa hakuna Mkandarasi atatekeleza Mradi kwa muda mrefu kuliko ule ambao, kwa raslimali alizonazo angekamilisha, ili apate faida kubwa. Muda uliompa Tenda ambao uko kwenye Mkataba ndo ufuatwe na pande zote mbili.
Juhudi zifanywe kupanda miti kuhufadhi vyanzo vya maji nyanda za juu kusini Iringa Njombe na Mbeya ambapo ndo chanzo cha mto Rufiji....la sivyo hali itakua tete sanaMto Ruaha ambao ni moja ya vyanzo vya Rufiji hali yake si nzuri kwa sasa...
TUSISAHAU PIA KAMPENI YA "nyumba ni choo" 😃😃😁😁🤣🤣🤣TANZANIA :- MAJI YA KUFUA UMEME JNHPP KUJAZWA NOVEMBA 2021
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 21 Februari, 2021 katika ziara yake kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere megawati 2115, amesema zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021.
Dkt. Kalemani amewaomba wadau mbalimbali hususani viongozi kuhakisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuweza kupata maji ya kutosha.
Akitoa wito kwa wananchi wote wanao lima maeneo ambapo kunavyanzo vya maji, Dkt. Kalemani amewaomba walime kilimo ambacho hakitaleta athari ya upatikanaji wa maji katika bwawa la Julius Nyerere, yatakayo tumika kuzalisha Megawati 2115.
Aidha, katika ziara hiyo ameagiza ufanisi wa kusimamia Mkandarasi usiku na mchana ili kuhakikisha anamaliza mradi kwa wakati.
"Mkandarasi ni lazima aongeze wafanyakazi na vifaa vyote vilivyo bandarini hakikisheni vinafika kwenye mradi na kufungwa kwa wakati".
Wewe ndio mtu pekee ambaye bado una energy ya kutosha ya kupinga Kila kitu.Huo utapeli unafanana na ule kuwa SGR Dar-Moro itaanza kazi Novemba 2019.
We naye do!!.Ngoja wataalam waje
Tena tunaambiwa ujenzi umefikia asilimia zaidi ya 70! ( Najua mkuu maeneo mengine huwa tunapishana, katika hili tumepisha kwenye matumizi ya neno utapeli tu!)Huo utapeli unafanana na ule kuwa SGR Dar-Moro itaanza kazi Novemba 2019.
Miaka 8!!! Yaani hakuna tone linakatiza kwenye tail race!! Hapo lazima uue ikolojia ya down stream! Jambo ambalo wahusika hawawezi kukubali.Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Bwawa la Ethiopia ni kwa sababu hawawezi kukomba maji yote kupeleka kwenye bwawa lao - kwa sababu ya Misri na Sudan. Inabidi wahakikishe hakuna uhaba wa maji down streem!Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Si kila kitu nitakijua mkuu.We naye do!!.
Mpaka kuwa Verified ni kuwa hata mada zako zipo verified tofauti na yangu, so kuandika stori pasipo kumuuliza waziri swali ni ujinga ujue!.
Kama umekopi sawa ila kama ulikuwepo kwenye hiyo ziara 🤬!.
Eti "ngoja wataalam waje"
Kama ww ulivyo na energy ya kusifia kila kitu. Ww huo muda hupati wa kufanya mambo mengine?Wewe ndio mtu pekee ambaye bado una energy ya kutosha ya kupinga Kila kitu.
Huo muda si ufanye mambo mengine mkuu