Kalemani: Zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021

Kalemani: Zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021

Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?

Mkuu wangu,tatizo la Tanzania kama si Afrika WATAALAM hawapewi nafasi badala yake WANASIASA wanajingiza kutoa taarifa ambazo hawana ujuzi wowote zaidi ya kubwabwaja mbele ya makamera.

Habari kama hii ya kujaza maji bwawa ilitakiwa kutolewa na eng msimamizi wa mradi si kalemani mwanasheria na mwanasiasa anayebebwa na sehemu anayotoka mkuu wa nchi.Huyu Kalemani angetakiwa kuendelea kutoa taarifa za ujenzi wa uwanja wa ndege CHATO au maendeleo ya hifadhi ya CHATO eg wale Simba waliopelekwa CHATO kutokea Serengeti wameongezeka au idadi ya watalii waliotembelea CHATO imeongezeka na nk.

Matamko mengi ni uchimvi ambao wala hatuna habari nao.
 
Bado sana
Bado sana tena sana maana mwezi uliopita tu walisema mchepuko (diversion) wa kubadilishwa mkondo wa mto umekamilika lakini hawakusema lini watahamisha hayo maji waanze kujenga ukuta wa Bwawa. Kazi kubwa na ya kitaalamu kabisa ni ujenzi wa huo ukuta utakaohimili nguvu ya maji ya mto na maji ya Bwawa likijaa na kuanza kuzalisha umeme wa Megawatt 2115 tunaoimbiwa kila siku. Megawatt 2115 ni Rated Capacity ya Bwawa mambo mengine yote yakiwa sawa ikiwa ni pamoja na maji kuwa ya kutosha wakati wote lakini, lisemwalo lipo kama halipo laja, inasemekana maji ya mto Rufiji yameanza kupungua na ukweli huo unaoneka wazi kwenye Tawi muhimu la Ruaha kuliko Bwawa la Mtera. Waziri alipokuwa pale akitoa maagizo labda toka juu utafikiri anaagiza watoto maeneo ya kwenda kuchungia mifugo lakini lugha ya mwili ya waliokuwa wanaagizwa, hasa wale Weupe, ilionyeshwa kuna matatizo makubwa kwenye utekelezaji wa Mradi na ni muda tu unasubiriwa Mkandarasi afungashe vilago aende zake. Awamu hii imefanya makosa mengi ya kijinga ya kuwalazimisha Makandarasi wakamilishe Miradi ndani ya muda mfupi kuliko uliokubaliwa kwenye Mikataba ndo maana Miradi mingi inatekelezwa chini ya viwango. Haihitaji PhD kujua kuwa hakuna Mkandarasi atatekeleza Mradi kwa muda mrefu kuliko ule ambao, kwa raslimali alizonazo angekamilisha, ili apate faida kubwa. Muda uliompa Tenda ambao uko kwenye Mkataba ndo ufuatwe na pande zote mbili.
 
Kalemani tumemzoea kuwa ni Waziri anayependa kuongea kama wasanii wa bongo movie. Yeye alimradi apigwe picha na atokee kwenye TV.

Siamini kuwa STIGLERS gorge power project itakuwa imefikia hapo. Sioni tukipata umeme huo hata 2025, na hili Meko analijuwa na ndiyo maana kauli za kutaka kuongeza muda wa utawala zinapoanzia.
Lakini si anahabarisha wananchi?
 
Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Ethiopia wamepigwa pini na Misri amabayo imesema mgawo wao w maji usipungue hata kidogo.
Ndio maana watajaza hilo bwawa kidogokidogo.
Siye hatuna Misri.
 
Bado sana tena sana maana mwezi uliopita tu walisema mchepuko (diversion) wa kubadilishwa mkondo wa mto umekamilika lakini hawakusema lini watahamisha hayo maji waanze kujenga ukuta wa Bwawa. Kazi kubwa na ya kitaalamu kabisa ni ujenzi wa huo ukuta utakaohimili nguvu ya maji ya mto na maji ya Bwawa likijaa na kuanza kuzalisha umeme wa Megawatt 2115 tunaoimbiwa kila siku. Waziri alipokuwa pale akitoa maagizo labda toka juu utafikiri anaagiza watoto maeneo ya kwenda kuchungia mifugo lakini lugha ya mwili ya waliokuwa wanaagizwa, hasa wale Weupe, ilionyeshwa kuna matatizo makubwa kwenye utekelezaji wa Mradi na ni muda tu unasubiriwa Mkandarasi afungashe vilago aende zake. Awamu hii imefanya makosa mengi ya kijinga ya kuwalazimisha Makandarasi wakamilishe Miradi ndani ya muda mfupi kuliko uliokubaliwa kwenye Mikataba ndo maana Miradi mingi inatekelezwa chini ya viwango. Haihitaji PhD kujua kuwa hakuna Mkandarasi atatekeleza Mradi kwa muda mrefu kuliko ule ambao, kwa raslimali alizonazo angekamilisha, ili apate faida kubwa. Muda uliompa Tenda ambao uko kwenye Mkataba ndo ufuatwe na pande zote mbili.
Tatizo viongozi wetu wanatuchukulia kama mazoba
 
Wale mashabiki wa ..,......puppet wa Belgium .....wanabisha .....kwamba mradi hautaisha
 
Mto Ruaha ambao ni moja ya vyanzo vya Rufiji hali yake si nzuri kwa sasa...
Juhudi zifanywe kupanda miti kuhufadhi vyanzo vya maji nyanda za juu kusini Iringa Njombe na Mbeya ambapo ndo chanzo cha mto Rufiji....la sivyo hali itakua tete sana
 
TANZANIA :- MAJI YA KUFUA UMEME JNHPP KUJAZWA NOVEMBA 2021

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 21 Februari, 2021 katika ziara yake kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere megawati 2115, amesema zoezi la kujaza maji ya kufua umeme katika bwawa litaanza 15 Novemba 2021.

Dkt. Kalemani amewaomba wadau mbalimbali hususani viongozi kuhakisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuweza kupata maji ya kutosha.

Akitoa wito kwa wananchi wote wanao lima maeneo ambapo kunavyanzo vya maji, Dkt. Kalemani amewaomba walime kilimo ambacho hakitaleta athari ya upatikanaji wa maji katika bwawa la Julius Nyerere, yatakayo tumika kuzalisha Megawati 2115.

Aidha, katika ziara hiyo ameagiza ufanisi wa kusimamia Mkandarasi usiku na mchana ili kuhakikisha anamaliza mradi kwa wakati.

"Mkandarasi ni lazima aongeze wafanyakazi na vifaa vyote vilivyo bandarini hakikisheni vinafika kwenye mradi na kufungwa kwa wakati".
TUSISAHAU PIA KAMPENI YA "nyumba ni choo" 😃😃😁😁🤣🤣🤣
 
Huo utapeli unafanana na ule kuwa SGR Dar-Moro itaanza kazi Novemba 2019.
Wewe ndio mtu pekee ambaye bado una energy ya kutosha ya kupinga Kila kitu.

Huo muda si ufanye mambo mengine mkuu
 
Ngoja wataalam waje
We naye do!!.

Mpaka kuwa Verified ni kuwa hata mada zako zipo verified tofauti na yangu, so kuandika stori pasipo kumuuliza waziri swali ni ujinga ujue!.

Kama umekopi sawa ila kama ulikuwepo kwenye hiyo ziara 🤬!.

Eti "ngoja wataalam waje"
 
Huo utapeli unafanana na ule kuwa SGR Dar-Moro itaanza kazi Novemba 2019.
Tena tunaambiwa ujenzi umefikia asilimia zaidi ya 70! ( Najua mkuu maeneo mengine huwa tunapishana, katika hili tumepisha kwenye matumizi ya neno utapeli tu!)
 
Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Miaka 8!!! Yaani hakuna tone linakatiza kwenye tail race!! Hapo lazima uue ikolojia ya down stream! Jambo ambalo wahusika hawawezi kukubali.
 
Nyie jengeni tu kimyakimya mkishaanza kuzalisha umeme mtatushtua. Hizo kauli hazipishani sana na za SGR dar ....moro 2019
 
Bwawa la Ethiopia litajazwa kwa muda wa miaka 8 mpaka 12 sasa hili letu watatumia week ngapi?
Bwawa la Ethiopia ni kwa sababu hawawezi kukomba maji yote kupeleka kwenye bwawa lao - kwa sababu ya Misri na Sudan. Inabidi wahakikishe hakuna uhaba wa maji down streem!
Lakini kwetu hilo hitaji halipo. Tutajaza maji mpaka yajae ndipo yatiririke yenyewe kwenda baharini.
 
We naye do!!.

Mpaka kuwa Verified ni kuwa hata mada zako zipo verified tofauti na yangu, so kuandika stori pasipo kumuuliza waziri swali ni ujinga ujue!.

Kama umekopi sawa ila kama ulikuwepo kwenye hiyo ziara 🤬!.

Eti "ngoja wataalam waje"
Si kila kitu nitakijua mkuu.
Mengine nitategemea msaada
 
Back
Top Bottom