Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Sheria ya Jamii Forum hakuna kutajana majina halisi.
Hata kama unamtambua anayetumia ID flani, usi mu expose.

Tutakufungia kwa kuvunja kanuni
Nimeomba any reference ya hizo sheria haujanipa halafu unamaanisha nini unavyotumia neno "tuta...." na wakati wewe ni member wa kawaida ?
 
Nimeomba any reference ya hizo sheria haujanipa halafu unamaanisha nini unavyotumia neno "tuta...." na wakati wewe ni member wa kawaida ?
Kwani huzioni sheria za Jamii Forum zilipoandikwa. Unaitumiaje platform bila kujua kanuni zake.

Halafu wewe sio member wa kawaida, uko special. Endelea kutaja majina halisi ya watu halafu sikilizia.
 
Hao sio waarabu ili wawe manabii wa Allah.
Nabii wa Allah ni Muhammad, Kwa sababu Mungu wa waarabu anaitwa Allah.
Na Mungu WA Wayahudi anaitwa Yehova/Yahweh/Jehova au Kwa kiswahi ni NIKO AMBAYE NIKO.
Ukitaka kujua maana ya ujinga waangalie wakristo wakijadili juu ya Dini.

Hao ni manabii sababu Allah alituma manabii katika kila Umma.

Maana ya Allah ni muabudiwa kwa Haki. Unaposema Mungu wa Waarabu Kisha ukasema ni Allah hapa umeandika uongo wa Wazi, sababu Allah ndiye aliyeumba mbingu na Ardhi na ni Mola wa viumbe wote.

Ukiwauliza Mayahudi juu ya Mola watakwambia ni yule aliyeumba mbingu na Ardhi, na haya ni majina tu kwa lugha ya watu husika ila anayekusudiwa ni Allah.

Leo ukimuuliza Mswahili Mungu ni nani atakwambia ni yule aliyeumba mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo.

Kwahiyo si sahihi kusema Mungu wa Waarabu huku maana ikiwa imeenea kote.
 
Daudi alimzaa Suleiman kwani ni uongo, Suleiman akamzaa Rehoboam na chain inaendelea
Andiko lenu limesema Yesu Kristo mwana wa Daudi.

Kingine hamna chain iliyoshikana katika hizo mlizo weka, hakuna chain inayofika kwa Yesu Kisha ikaruka mpaka kwa Daudi. Hapa lazima muwataje waliopo katikati mpaka kufika kwa Daudi.
 
Ukoo wa YESU huu hapa
Luka 3:23
<br>Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,

Luka 3:24
wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu,

Luka 3:25
wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai,

Luka 3:26
wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda,

Luka 3:27
wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,

Luka 3:28
wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri,

Luka 3:29
wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi,

Luka 3:30
wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,

Luka 3:31
wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi,

Luka 3:32
wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni,

Luka 3:33
wa Aminadabu, wa Aramu, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda,

Luka 3:34
wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori,

Luka 3:35
wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala,

Luka 3:36
wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki,

Luka 3:37
wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani,

Luka 3:38
wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.
Ndiyo maana nikasema hivi hakuna Chain hapa, Yusufu wa kwanza ndiyo huyo aliye muoa Mariam ?

Yusufu wa mstari wa 3:30 ni yupi ?

Yakobo alimzaa Yusufu huyu simuoni katika Chain.
 
Mbona ushapewa Aya kwenye Biblia lakini naona unakaza fuvu.
Kumbuka wasomaji na wafuatiliaji ni wengi hivyo usiwaangushe wanaoamini Quran.
Maana unapewa Aya unakataa sasa unataka tukupe Stori za kina Joti?
Sasa unanipaje ambazo waandishi wake hawajulikani Mzee ? Au unataka tufikiri kitoto kama mnavyofikiri nyinyi ? Yaani andiko lenu lolote ili niliamini lazima lokidhi vigezo hivi :

1. Lifanane na yale yaliyosemwa na Qur'aan au Hadithi za Mtume.

2. Kadhalika tuwajue waandishi wa hivyo vitabu na chain Yao ifike mpaka kwenye Primary Source, kama kwa Musa au kwa Yesu. Kinyume na hapo usiniwekee andiko sababu andiko Hilo linakuwq na sifa ya udhaifu na uongo.

Shukrani.
 
Kwa mujibu wa Quran Ibrahimu alikufa akiwa na miaka mingapi?

Ibrahimu Mungu wake Hakuwa Allah!
Ibrahim hajawahi kufika Saudia Arabia,
Na Allah hajawahi kufika Jerusalem Kwa wakati ule labda nyakati hizi Allah ndio kafika
Wewe ni mgalatia haumjui Mungu wa kweli na ndio maana katika post zako unataja miungu mingi mingi sijui Mungu wa Musa sijui Mungu wa wakristo ,sijui Mungu wa waislam

Ila tambua kuwa Mungu ni mmoja tu aliyeumba mbingu na nchi na ndio aliyemuumba Ibrahim, Yesu , wewe na mimi
Sasa je! Huyo Mungu wewe unamjua shida yako ndio ipo hapo

Hapo nabii Ibrahim na mwanawe Ismail wapo Saudi Arabia wanajenga msikiti wa makka

Kisha wakaomba Dua na mwisho kabisa wanamuomba Mungu alete mtume katika nchi ya Saud Arabia anayetokana na wao

Quran 2:127.
Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.

128.
Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

129.
Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
 
Ndiyo maana nikasema hivi hakuna Chain hapa, Yusufu wa kwanza ndiyo huyo aliye muoa Mariam ?

Yusufu wa mstari wa 3:30 ni yupi ?

Yakobo alimzaa Yusufu huyu simuoni katika Chain.
Yusuf si wako wengi kama ilivyo Muhammad wako wengi wanaoitwa Muhammad nimekuja gundua una upeo mdogo sana

Ajabu nin yusuph wako wengi ni jina tu hata Leo Kuna watu kibao wanaitwa yusuphu
 
Quran imeelezea vitabu ambavyo tayari vilikuwepo.
Jipya la Quran ni lipi?
Au hujui kila kitabu kinalengo lake kuu?
Kuelezea sio tatizo ni kweli imevielezea ila haina maana kuwa Qur'an ni mkusanyiko wa hivyo vitabu kama inavyosemwa kwa Biblia kuwa biblia ni mkusanyiko wa vitabu. Qur'an imeeleza vitu vingi sana.
 
3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.

Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.
Sijui kwanini mnabishana hili suala dogo sana, Muhammad kaja kipindi ambacho hivyo visa vyote vishatokea hivyo vinajulikana kwahiyo hakuwa akielezea kama kitu kipya kama ambavyo kuna kisa cha toka kuumbwa Adamu huko na hakuna aliyekuwepo iweje shida Muhammad kuelezea hivyo visa vyengine ndio ije hoja ya kwamba hakuwepo huko?
 
Andiko jipya la Quran kuwasaidia ni Majini kupitia Sura ya majini.
Hayo mengine, hakuna jipya
Basi kama hivyo waislamu na wakristo wangefanana mambo yao kama ibada zao n.k maana si hakuna fundisho jipya alilokuja nalo Muhamnad kwamba yote kakopy ?
 
Alivyo fanya Muhammad sio poa alitakiwa atoe acknowledgement
Yeye kafanya Plagiarism

Kaiba maandiko ya watu kafanya yake
Kafanya yake kvp? Hebu fafanua yapi aliyoyafanya yake?
 
Issa, Musa, Daudi, yusufu, yakobo, N.k ni waarabu?

Kama umefika Chuo kikuu basi utajua Dalili au sifa za Plagiarism.

1. Kachukua wahusika wa Wayahudi
Kamtoa Musa kwenye Torati ya Wayahudi kamuweka kwenye visa vyake vya Quran kisha kafanya modification
Kamchukua Daudi na Suleiman kwenye Zaburi kampachika kwenye kitabu chake cha Quran.
Kamchukua Yesu akampa jina Issa kwenye Injili akamuweka kwenye Quran yake.

Kachukua Yona kwenye Visa vya manabii wa kiyahudi, akamuita Yunus na kumuweka kwenye Quran.

2. Kaiba Visa vya Wayahudi alafu kafanya modification.
Mfano, kisa cha Yesu/Issa
Kisa cha Yusufu
Kisa cha Musa na Kina Daudi.

Kitu pekee nilichoona Muhammad hajafanya Fair ni kumuacha kumuiba Mungu WA Wayahudi aitwaye Yehova ambaye ndiye aliyesimamia shoo zote tangu Ibrahimu mpaka Yesu, akamuweka mungu wake wa kiarabu aliyekuwa anamuabudu pale kwenye Alkaba aitwaye Allah.
Neno kuiba si sahihi, mfano Qur'an inapinga suala la Yesu kufanywa Mungu na inapinga kwa Yesu kusulubiwa hivyo utaona kwenye kisa cha Yesu Qur'an inasahihisha yale yaliyopotoshwa na kueleza yaliyo sahihi. Sasa kama lengo lingekuwa ni kuiba tu hivyo visa basi vingeelezwa tu kama vilivyo kwenye biblia.

Na chengine hivyo visa sio hadithi za kuburudisha bali vina mazingatio ndani yake hivyo Qur'an imevielezea hivyo visa ili watu kupata kujifunza maana ni mambo ambayo yameshatokea ni visa vya manabii na waja wema na Muhammad ni katika manabii.

Qur'an imeeleza vitu vingi hivyo visa ni katika sehemu tu ya vitu vilivyomo kwenye Qur'an, sasa hoja za sijui kukopy au kuiba najiuliza iweje tena ajabu mtu anasema Qur'an hakuna jipya imekopy biblia kisa hivyo visa tu.
 
Nimecheka sana, Uislaamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allah kwa kumtii na kumpwekesha yeye peke yake pasi na kumshirikisha na yoyote na chochote.

Hika ilikuwepo na Ibrahim alihiji na ndiyo mjenzi wa Ile nule Msikiti wa Makka.

Tofauti iliyo kuwepo baina ya mitume Hawa ni Sheria ila Imani Yao ni Moja.

Uislamu umegawanyika sehemu juu mbili, Uislamu wa ujumla huu ni Ile Imani na Uislamu khasa ambao aliokuja nao Mtume kwa maana ya Sheria tofauti.

Hata Musa alikuwa ana Hiji na anafunga na alikuwa ana Sali kwa mujibu wa Sheria yake aliyo pewa na Allah.

Kuhusu suala la Shahada, Shahada yetu ya Leo haiwezi kuwa sawa na ya walio pita sababu kila umma ulipewa utaratibu wake na Sheria zake.

Kadhalika zaka walitoa.
Hizo sheria za Umma wa akina Ibrahim ziko wapi?

Hebu ongea kwa ushahidi, Hizo sheria za Umma wa kina Ibrahim, nikitaka kuziona/kuzisoma zinapatikana wapi?
 
Neno kuiba si sahihi, mfano Qur'an inapinga suala la Yesu kufanywa Mungu na inapinga kwa Yesu kusulubiwa hivyo utaona kwenye kisa cha Yesu Qur'an inasahihisha yale yaliyopotoshwa na kueleza yaliyo sahihi. Sasa kama lengo lingekuwa ni kuiba tu hivyo visa basi vingeelezwa tu kama vilivyo kwenye biblia.

Na chengine hivyo visa sio hadithi za kuburudisha bali vina mazingatio ndani yake hivyo Qur'an imevielezea hivyo visa ili watu kupata kujifunza maana ni mambo ambayo yameshatokea ni visa vya manabii na waja wema na Muhammad ni katika manabii.

Qur'an imeeleza vitu vingi hivyo visa ni katika sehemu tu ya vitu vilivyomo kwenye Qur'an, sasa hoja za sijui kukopy au kuiba najiuliza iweje tena ajabu mtu anasema Qur'an hakuna jipya imekopy biblia kisa hivyo visa tu.

Ukisema Quran inapinga Yesu kuwa Mungu kwani ni wapi Biblia iliwahi kusema Yesu ni Mungu?

Quran imeiba/imefanya plagiarism Kwa sababu haijatoa Credit kwenye vitabu ilivyochukua taarifa na wahusika wake.
Alafu ikafanya Forgery ili ionekane yenyewe ndio chanzo cha visa hivyo.

Neno kisa sio lazima iwe Stori ya kubuni au yakifasihi hata tukio la kweli linaweza kuwa kisa
 
Back
Top Bottom