Kama Biblia ni kitabu cha kutungwa, nani alikitunga na chanzo na kusudio lake ni nini?

Biblia & Quran ni vitabu vya hadithi vilivyotungwa
Ndiyo tunataka kumjua/kwajua waliotunga hicho kitabu?
Kuna mtu analazimishwa kuamini Biblia??
 
Hakuna kitabu Cha mungu kinachoitwa biblia vitabu vinavo julikana ni 4 na vilishushwa Kwa kila zama
1.Zaburi
2.Torati
3.Injili
4.Quran
Endeleeni kufata wazungu na warabu mkija kujua ukweli wa dunia inavoeenda mmechelewa
Qur'an si ni ya Muarabu?
Yaani mpaka mnakariri Arabic language ili muisome Qur'an. Au ile ni lugha gani?
 
Umetuambia ni utamaduni wa watu wa Asia.Hapo hapo unamalizia kwa kuwahusisha wazungu na biblia!Kwa nini wazungu wasambaze tamaduni za Asia na waziache za kwao?Biblia haina tamaduni za kizungu hata moja.Kwa jinsi wazungu walivyo na nguvu za kueneza mambo yao,kweli walishindwa kutunga kitabu chenye mkusanyiko wa tamaduni zao wakisambaze duniani!!
 
Hakuna kitabu Cha mungu kinachoitwa biblia vitabu vinavo julikana ni 4 na vilishushwa Kwa kila zama
1.Zaburi
2.Torati
3.Injili
4.Quran
Endeleeni kufata wazungu na warabu mkija kujua ukweli wa dunia inavoeenda mmechelewa
Inaonesha jinsi gani ulivyo na akili ndogo ya kuchanganua mambo.Unashindwa kuelewa mkusanyiko wa vitabu hivyo ndo unaitwa biblia!!Haya niambie;Mzungu ametunga kitabu gani katika vitabu vinavyounda biblia?(torati,zaburi,injili).
 
Hosea 9:5

Mtafanya nini katika siku ya mkutano wa idi, na katika siku ya karamu ya Bwana?
Kwa hiyo ikitajwa idi basi unachanganyikiwa kabisa sio?Lugha ndo inakuchanganya wewe sio?Idi ni neno la kiarabu,linalomaanisha 'sikukuu'.Wazungu-holiday,waarabu-idi,waswahili-sikukuu.Na hiyo ni kwa sababu kiswahili ni mchanganyiko wa kibantu,kiarabu kwa sana na Lugha za ulaya kidogo.Hiyo idi unayoiona hapo Ina jina lake.Ni idi ya vibanda:yaani sikukuu ya vibanda.Sasa nyie mna sikukuu ya vibanda?Nyie mna sikukuu ya kuchinja,kufuturu,kuzaliwa mtume.Sasa ungetoa Aya inayotaja sikukuu hizo za kuchinja kufuturu,n.k mnazozisherehekea ndugu zetu wa mama mdogo.Hapo tungekuelewa.Nyie ni wapinga torati,hilo like wazi.
 
Hata biblia nayo imesheheni contradiction nyingi tu.

Uwepo wa contradiction hizo zinaonyesha kabisa kuwa si kitabu cha Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.
sasa we unaamini nini kati ya biblia na qur an? Tatizo wengi hawajui kuchambua maudhui ya biblia wanaishia kuona contradiction tu
 
Warumi watunge biblia halafu waweke mambo ya Asia wayaache ya kwao!Si ungeona biblia imejaa ibada za sanamu na Misa za wafu humo?Ungeona amemtaja papa kama mungu na mtakatifu wa dunia?Ungeona jumapili ndiyo siku ya sabato,iliyotengwa rasmi kwa ajili ya ibada badala ya jumamosi?Ungeona nguruwe ni mnyama mtakatifu kwa kuliwa?Ungeona aya zinazowatambulisha Warumi kuwa ni taifa teule?Au tukubaliane kuwa wayahudi wanapendwa na dunia nzima kiasi kwamba hadi wametungiwa kitabu kinachowaelezea wao ni taifa teule.Hapa ni jamii forum.Home of great thinker.Hebu jaribu kuthink big ktk hili
 
Habari ya yesu sio utamaduni wa mzungu?

Watu wanasali jumapili, huo sio utamaduni wa mzungu?
 
sasa we unaamini nini kati ya biblia na qur an? Tatizo wengi hawajui kuchambua maudhui ya biblia wanaishia kuona contradiction tu
Kwanini unadhani naamini kati ya biblia na quran tu, si kitabu kingine?
 
Umechanganya mambo, ili kuyajadili vizuri ngoja tuyachambuwe:

Maana ya biblia naijuwa na hilo neno limetokana na kigiriki au siyo?

Sasa nakuuliza, huyo "roho mtakatifu" alimuongoza mwandishi wa kitabu kama ni mkusanyiko wa vitabu vingi"?
kabla ya kuendelea na mjadala hebu chukua biblia, naamini utapata ziko nyingi kwenye maduka ya vitabu. Nakushauri uchukue biblia ya The Holy Bible in Kiswahili, 1952 Union Version, usome kwanza dibaji halafu rudi na hoja yako. Nadhani utakuwa umepata mwanga kukujibu swali lako.
 
Kwanini unadhani naamini kati ya biblia na quran tu, si kitabu kingine?
unatakiwa upigwe injili mpaka ulainike, una moyo mgumu usioamini, moyo wa jiwe badala ya moyo wa nyama. Tuseme we ni mpagani/kafiri/mshenzi usiyeamini neno la Mungu?
 
Hakuna kitabu Cha mungu kinachoitwa biblia vitabu vinavo julikana ni 4 na vilishushwa Kwa kila zama
1.Zaburi
2.Torati
3.Injili
4.Quran
Endeleeni kufata wazungu na warabu mkija kujua ukweli wa dunia inavoeenda mmechelewa

Alikuwa anashusha nani na kwa maandishi ya aina gani? Na katika ukubwa wa ulimwengu huu hata huko China, Urusi, New Zelsnd mbona havikushushwa?
 
Hakuna kitabu Cha mungu kinachoitwa biblia vitabu vinavo julikana ni 4 na vilishushwa Kwa kila zama
1.Zaburi
2.Torati
3.Injili
4.Quran
Endeleeni kufata wazungu na warabu mkija kujua ukweli wa dunia inavoeenda mmechelewa

Na alishushiwa nani na kwa elimu ipi ya kujua kusoma na kuandika, maana watu wengi walikuwa hawajui kusoma na kuandika na walikuwa sanaishi na popo huko misituni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…