Tetesi: Kama hili ni kweli, basi nakubaliana na Lissu kuhusu Dkt. Slaa

Tetesi: Kama hili ni kweli, basi nakubaliana na Lissu kuhusu Dkt. Slaa

Hii Nchi imekuwa ya hovyo sana.
Mwananchi kupata habari imekuwa ni kwa hisani ya Ccm.
Magazeti yote kwa sasa yanatoa habari kwa maelekezo ya Nape. Redio, Tv woote ni ushuzi mtupu
Jf nayo imejaa wanaojiita chawa wa mama ilimradi kuvuruga watu tu.
Ndio maana TEC walitumia njia mbadala kufikisha waraka wao na ukafika vyema.
Mkuu hapa ulipo comment nahisi umepotea, maana ulichoandika kipo nje ya hoja inayojadiliwa hapa.

Mada ni kuhusu jinsi Lisu alivyozuia Dr Slaa kurudi Chadema kutokana na kukisaliti chama chao, na pia kufurahia jinsi Lisu alivyopigwa risasi na baadae Mbowe kuwekwa ndani kwa uhaini.

Sasa hayo uliyoandika hapa hayaendani na kinachojadiliwa.

Ni bora ungeyaanzishia uzi wake watu wacomment.
 
Hivi Josephine,ndiye aliyesababisha Slaa wachane na Rose!?
Inasemekana babu baada ya kuchovya ndo akaingia mazima na matokeo yake ndoa chali.

Sasa anatamani siku zirudi nyuma, ila ndo basi tena hilo haliwezekani.
 
Hakuna siku Dk Slaa aliniumiza kama siku ile pale Serena alipokwenda kuwaga mboga... Matokeo yake akarudia yaleyale ya zamani! Siku nilijua anaenda kummaliza Lowasa ! na CHADEMA!
Ni kweli kwenye Siasa hakuna Urafiki au Uadui wa kudumu.
! Ila alipokejeli hata kuumizwa Kwa Lissu au kufungwa Kwa Mbowe ...mhhhh hapana!
Yani Dr Slaa sio tu msaliti, bali ni katili kabisa aisee.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakuu kuna habari ambayo nimeipata leo kutoka kwa mtu ambae yupo karibu zaidi na kiongozi fulani wa chama cha demokrasia na maendeleo, wengi mnakiita Chadema.

Ni hivi.. inasemekana baada ya Dkt. Slaa kuvuliwa hadhi yake ya ubalozi jana, kitu cha kwanza alichofanya ni kumpigia simu mwenyekiti wake wa chama wa zamani ili kumuomba wakutane nae haraka iwezekanavyo.

Mwenyekiti alipotaka kujua sababu ya yeye (dokta) kutaka kukutana nae ilhali wanaweza kuongea tu kwenye simu wakamaliza, Dr akamwambia kwamba anaomba wakutane nae ili amuombe msamaha kwa usaliti aliyoufanya mwaka 2015, na pia kumuomba msamaha kuhusu ile kauli aliyoitoa wakati ule Mbowe akiwa kafungwa kwa kesi ya uhaini.

Mwenyekiti alivyosikia hivyo akamuuliza kama lengo lake haswa ni kuomba msamaha au alikuwa na lingine la zaidi. Maana kama msamaha tayari atakuwa ameshaomba kupitia kauli yake ile aliyosema au anaweza kuomba tu hapo hapo simuni wakasameheana yakaisha.

Dokta akasema lengo sio msamaha peke yake, bali anataka pia arudi chamani kupitia kukutana kwao huko.

Ndo mwenyekiti akamwambia kama una lengo la kutaka kurudi chamani basi ngoja niongee na baadhi ya viongozi wenzangu ili nisikie na wao maoni yao kabla hatujakutana. Kisha mwenyekiti akampigia makamu kumueleza kile alichoambiwa na dokta.

Aisee baada ya makamu kusikia habari za dokta kwanza akapandisha pumzi na kushusha, after that kilichobakia ilikuwa ni kumshambulia dokta na kumwambia mwenyekiti kwamba huyo dokta sio mtu tena wa kumkaribisha chamani maana hana moyo wa kweli wa kupigania mabadiliko nchini, yeye ana moyo tu wa kupigania tumbo lake na familia yake.

Makamu akatahadharisha kwamba ikiwa mwenyekiti atashupaza shingo na kumruhusu kujiunga upya na chama, basi mwaka 2025 kama chama hakitatimiza lengo lake la kutaka achaguliwe kugombea uraisi basi mwenyekiti huyo na chama kwa ujumla wajiandae kukutana na yale waliyokutana nayo mwaka 2015.

Makamu alisema kwamba ni mara kumi ingekuwa ni Zito ambae hakuwahi kuonesha kufurahishwa na yale yaliowakuta wapinzani wenzake mbali mbali, kuliko huyu mzee ambae hakuonesha utu hata kidogo kipindi mwenzake alipopigwa risasi na kupambania uhai wake.

Mwenyekiti baada ya kusikia maoni ya makamu wake akawapigia wengine ambao nao hawakupendezewa na uamuzi wa dokta huyo kurudi chamani.

Baada ya hapo mwenyekiti akarudi kwa simu ya dokta na kumwambia kwamba mimi nimekusamehe, lkn swala la wewe kurudi chamani kwa sasa hivi sahau.

Mwenyekiti akakata simu huku akimuacha dokta akikosa la kufanya.

Ama kweli kifo cha nyani miti yote hutereza.
Kwa sasa kila anapojaribu kushikilia dokta anaanguka.

Jioni njema.
Hata Lissu na Mbowe wakisoma hili andiko na wenyewe watashangaa sana, hakika umejua kuwabunia maneno kwa kiwango cha juu mno😂😂😂😂😂
 
Si tu ni uongo Mr p but hakuna kitu kama hicho kuwepo kwa senior kama Dr slaa, unaweza kuniokota mm kwa ignorance yangu ya uhaba wa elimu ya technology but kwa Dr? A big No. Aje na hoja mpya
Moyo wa mtu msitu ndugu yangu. Muda mungine vile umdhaniavyo mwenzako sivyo vile alivyokuwa.

Ndomaana kuna msemo unaosema "usiusemee moyo wa mwenzako".

I hope umenielewa.
 
Hata Lissu na Mbowe wakisoma hili andiko na wenyewe watashangaa sana, hakika umejua kuwabunia maneno kwa kiwango cha juu mno😂😂😂😂😂
Amna sikubuni mkuu. Nimeandika uhalisia wa kile kilichopewa 🤣🤣🤣
 
CHADEMA acheni unafiki,Mbowe ndiyo Msaliti,bila Mbowe kwa kushirikiana na JK kumleta Lowasa CHADEMA ili agombee Urais,Dr Slaa asingeondoka.
Muwe na soni sometimes,Dr Slaa arudi bila Masharti,kama hamtaki basi na Mbowe akae pembeni maana alikaribisha fisadi kugombea Urais kinyume na ajenda ya kupinga ufisadi ya CHADEMA!
Huyo fisadi yupo wapi kwa Sasa? Na mtoto wake kapewa ubunge. Wewe ndio mnafiki
 
Hivi wewe na hadithi zako hizi uwa hujisikii kuwa hata wajinga kuna siku moja watajua unazitunga mwenyewe na kuwa hazina hata chembe ndogo sana ya ukweli?

Naona hapo chini umepewa 'likes' na wengine hata kutoa "nzuri"

Ina maana kuna wajinga ambao unaweza kutumia kipaji chako hiki cha kutunga hadithi na ukapata mlo wa kila siku kutokana na kazi hiyo.
Nadhani amepewa likes kutokana na jinsi alivyo Tunga hadithi inayoakaisi ukweli. Yani hata Kama ametunga ila scenario inafanana na ukweli asilimia 90%
 
Dr Slaa ni project 101, CCM wanamtumia kuwasambaratisha wapinzani, walimtumia mwanzo na hawasiti kumtumia sasa. Mambo yote kuhusu Dr ni maigizo mpaka huko TEC yanaingia.
Huwa mnapenda kuipa sifa CCM kwa mambo ambayo haina uwezo nayo. Eti project 101. Kiburi Cha CCM kipo kwenye Dola basi. Hizi zingine porojo.
 
Huu upumbavu ulioleta hapa jukwaani ni mafala wenzako ndio watakupongeza

Slaa ninaemjua mimi hawezi fanya huo ujinga,kawa balozi bila kadi ya CCM,haiitaji chadema tena,yeye ni mwanaharakati huru kabisa
Slaa anaihitaji CHADEMA kuliko kitu chochote.
 
Shida Dr Slaa aliongea mengi Sana kiasi Cha kutokuaminika Tena.
Alijua ataendelea kuwa katika nafasi aliyokuwa nayo milele 😂😂
Sasa jumba limemuangukia, hana pakukwepea mvua 🤣🤣
 
Back
Top Bottom