Kama Kifo ni mpango wa Mungu basi Mungu wenu atakuwa katili sana, mnawezaje kuwa nae?

Kifo siyo kibaya mara zote. Imagine watu kama kina Hitler, Idd Amin, Magufuli, Mobutu wangekuwa wanaishi milele.

Duniani pangegeuka Jehannum
Mungu alishindwa kuumba dunia ambayo haiwezekani kuwa na kifo na pia haiwezekani kuwa na watu wabaya?
 
Ina maana alipokuwa anamuumba huyo malaika hakujua kuwa atakuja kuasi na kuwa shetani atakayetuingiza dhambini, kifo na hatimaye kututenga naye Baba yetu muumba? Alijua hakujua? Jibu hili swali kwa ndiyo/hapana mengine yote puuzia !!!
Ina maana alipokuwa anamuumba huyo malaika hakujua kuwa atakuja kuasi na kuwa shetani atakayetuingiza dhambini, kifo na hatimaye kututenga naye Baba yetu muumba? Alijua hakujua? Jibu hili swali kwa ndiyo/hapana mengine yote puuzia !!!
hapana
 
Mungu mwenye upendo sana,huruma sana na mwenye uwezo wa kufanya kila kitu alishindwa vipi kumzuia binadamu asile hilo tunda?Upendo wake uko wapi?Huruma yake iko wapi?Uwezo wake uliotukuka uko wapi?
unajua maana ya uhuru wa kuchagua?
 
Wakati mungu anamuumba adam alikua tayari anauwezo wa kujua yajayo kabla hayajatokea, alikuwa na upendo wote na uwezo wote au hivyo vitu alikuja kuwa navyo baadaye baada ya kufanya uumbaji?
nikuambia hakujua unaweza nipa ushahidi alijua?
ukiwa na nguvu sio kila kitu unanyanyua
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
waroma 1:19 kwa sababu mambo yanayoweza kujulikana kuhusu Mungu yako wazi kabisa kati yao, kwa maana Mungu aliyaweka wazi kwao. 20 Kwa maana sifa zake zisizoonekana, zinaonekana waziwazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu na kuendelea, kwa sababu zinaeleweka kupitia vitu vilivyoumbwa, yaani, nguvu zake za milele na Uungu, hivi kwamba hawana sababu ya kujitetea.
 
Haya jibu sasa swali nililokuuliza.
 
NINAWEZA ila inabidi ukubali kwanza kua inawezekana yupo ndio ntakuthibitishia, kwasababu wewe hukatai with absolute certainty kwamba hayupo, bado una wasiwasi
"Absolute certainty" ni nini? Unajuaje kwamba ipo kweli na si njozi tu ya kufikirika?
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Umehubiri Biblia.

Sijaomba mahubiri. Kwetu kanisani nimeyasikia mahubiri tangu tumboni mwa mama yangu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Mungu yupo ni imani na Mungu hayupo ni imani. Hakuna mwenye ukweli basi tuheshimiane, subiri wakati wa mwisho roho itaondoka kwenda kuanzisha maisha kwa mfumo mwingine nawe ufutike katika uso wa dunia.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Roho ni nini?

Unaweza kuthibitisha roho ipo kweli na si hadithi ya kufikirika tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…