Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Kujua ni nini?Labda nikuulize,kila jambo unalolijua wewe kuwa ni kweli una uthibitisho wake?
Unajuaje unajua kweli na huoti njozi tu inayokufanya ufikiri unajua kweli?
Kwa mfano, watu wote walioishi kabla ya kujua atomic theory walijiona wamejua kwa uhakika kabisa kwamba chuma ni solid.
Kumbe chuma ni takriban 90% empty space. And that goes for any matter. According to atomic theory.
Watu walioishi kabla ya Einstein walifikiri time is absolute and universal.
Einstein akaja kutuonesha kwa relativity kwamba time ni relative and local.
Sasa wewe unajuaje chochote unachofikiri unajua unakijua kweli, na huna njozi tu kutokana na udogo wa mawazo yako?
Mimi nikikosa kujua kwa uthibitisho jambo lolote, hilo linathibitishaje Mungu yupo?
Thibitisha Mungu yupo.