Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Kama kipato chako ni chini ya milioni Tano kwa mwezi wewe ni Maskini

Bora ya wazungu wanatumia kipimo, ila wewe unatumia hisia zako alafu unataka watu wakuamini maisha sio marahis hivyo
Unasafari ndefu sana kifikra sababu unaishi kwenye fantasy world

Hao wazuñgu waliokufundisha gdp waliposema chini ya dola moja ni Umaskini walitumia kipimo gani kama sio mtazamo wao. Ili ujue umekariri
 
Milioni tano kwa mwezi ni kama 160,000 kwa siku, huwezi kumudu milo mitatu Serena Hotel, bado ni masikini wa kutupwa
Huo ni ukweli mtupu. Una 5M kwa mwezi halafu unaishi kwenye hotel ya nyota tano kwa maana unakula, unalala na unakunywa katika hoteli hiyo. Hapo unautafuta umasikini kwa kuishi maisha ambayo yapo juu ya kipato chako. Lakini kwa wale ambao wanaishi maisha ya kawaida hutwo tuela tunatosha kwa kubadilisha mboga, malazi na kinywaji bila wasiwasi.
 
Serena hotel sio SI unit ya mlo, pale unalipia na majengo, ila kwa 160K unaweza nunua vitu ukapika home milo mitatu mizuri sana, + kuajiri mpish special wa familia mwenye cheti kabisa hahaha
Tena na chenji inabaki kabisa
 
Zinaitwa maskini kwa kutumia gdp per capita income kipindi cha magufuli gdp per capita ilipanda tukaondoka kwenye nchi maskini kipindi cha samia gdp per capita imeshuka tumerudi tena kwenye kundi la nchi maskini

Nimeshangaa sana na hiki ulikua hukijui hivi huko shuleni mnasomaga au mnasukuma siku ziende
Hujui gdp per capita ndo kipimo cha kujua nchi ni maskini au tajiri na bado hujui aiseeee
Wew ndio hujui, lini tumeshuka ? Latest gdp per Capital ya Tz ni ngapi ?
 
Hapana mkuu wapo wengi sana wanapata zaidi ya hiyo, wanasiasa wenye vyeo, wanajeshi wenye vyeo, watumishi wa kwenye mashirika na mamlaka za serikali kwenye vyeo, watumishi wa taasisi na kampuni kubwa binafsi wenye vyeo, wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa, nk

Muelekezechuyo ndugu yako tofauti ya Umaskini na ufukara huenda hata haelewi nini kinazungumziwa hapa
chaneee
 
Back
Top Bottom